Nimeamua kuondoka kwa kaka na kujitegemea

Alooo hama kabisa umri huo ni wa kujitegemea kabisa ,ukitoka hapo amini akili ya maisha itafunguka..umri huo sio wa kugongea kaka na shemeji akupe dawa ya meno uswaki..
Nimekuelewa kaka nitafanya hivo
 
Wana wa Israel waliianza safari kwa Imani miujiza ndo ikafuata, nenda kafanikiwe sana mwana kwetu, ila sasa, kwa nini unaanza na kuhama? Hatua ya kwanza ni ku hustle kutwa na kurudi tu kulala kwa bro, waondoka giza, warudi giza, utengeneze msingi kwanza
 
Hapana kaka naona nikihama jumla itanipa spirit zaidi ya kupambana maana kudaiwa kodi lazima akili ichangamke
 
Hapo sasa ndio umekua na akili. Nao walikupuuza sababu waliona huna akili unategemea za kwao. Hapo hata kukusaidia wanaweza
Sawa kaka nashukuru kwa kunitia moyo
 
Hapana kaka naona nikihama jumla itanipa spirit zaidi ya kupambana maana kudaiwa kodi lazima akili ichangamke

Unaharibu, una sababu nyingi sana za kuwa na hiyo spirit, sio kwenda kujifesa, haya maisha sio mepesi. Bila mkakati utarudi kwa aibu.

Unauzaje simu uende kupanga? Huo ni wendawazimu, simu ni ya muhimu sana kwenye harakati zako za mahangaiko.
 
Unaharibu, una sababu nyingi sana za kuwa na hiyo spirit, sio kwenda kujifesa, haya maisha sio mepesi. Bila mkakati utarudi kwa aibu.
Kaka naamini mungu atanisimamia wacha tu nichukue haya maamuzi ni ngumu lakini naamini nitaweza
 
Unaharibu, una sababu nyingi sana za kuwa na hiyo spirit, sio kwenda kujifesa, haya maisha sio mepesi. Bila mkakati utarudi kwa aibu.

Unauzaje simu uende kupanga? Huo ni wendawazimu, simu ni ya muhimu sana kwenye harakati zako za mahangaiko.
Nitanunua kiswaswadu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…