Nimeamua kuondoka kwa kaka na kujitegemea

Nimeamua kuondoka kwa kaka na kujitegemea

Alooo hama kabisa umri huo ni wa kujitegemea kabisa ,ukitoka hapo amini akili ya maisha itafunguka..umri huo sio wa kugongea kaka na shemeji akupe dawa ya meno uswaki..
Nimekuelewa kaka nitafanya hivo
 
Habari za muda wakuu jana niliomba ushauri kuhusu kuhama kwa kaka yangu.

Kiukweli najilaumu sana kuchelewa kuanza maisha kwa sababu ya kusubili ahadi za ndugu toka nikiwa na miaka 23 nimekuwa nikiahidiwa msaada na mbaya zaidi mimi ndio nilikuwa nipo nyumbani na mama huko mkoani, Nimekuwa pale kwa miaka mingi huku ndugu zangu wakiwa dar.

Kila wakija walikuwa ni watu wa kuniahidi kunisaidia jambo ambalo limenifanya kubweteka.

Nimeishi hapo mpaka pale kaka yangu alipokuja kunichukua mwishoni mwa 2019 yeye pia baada ya kunileta ajajitoa kwa dhati kwa ajili ya kunipa msingi bora japo uwezo wake kifedha c haba na kaajili watu wengi ila mimi amekuwa akiniunganisha kwenye kazi za kuangaika sana mpaka sasa sina maendeleo yoyote nafsi inaniuma sana maana nimechelewa sana kuanza kujitegemea now nina miaka 32 kiukweli naona aibu kuendelea kubaki hapa kwa bro.

Sina msingi wala mtaji ila niluchoamua from now nikuuza simu yangu na kwenda kupanga mengine yatajulikana mbele ya safari najua ni uamuzi mgumu lakini nimeamua kwa moyo wa dhati kwenda kujitegemea.

Nimechelewa sana nafsi inaniuma mno sina furaha kwakweli ila nilichoamua ndicho hicho. Na hakuna kurudisha mpira kwa kipa naenda kuhastle kiukweli.

Naombeni baraka zenu ndugu zangu.

Wana wa Israel waliianza safari kwa Imani miujiza ndo ikafuata, nenda kafanikiwe sana mwana kwetu, ila sasa, kwa nini unaanza na kuhama? Hatua ya kwanza ni ku hustle kutwa na kurudi tu kulala kwa bro, waondoka giza, warudi giza, utengeneze msingi kwanza
 
Hapana kaka naona nikihama jumla itanipa spirit zaidi ya kupambana maana kudaiwa kodi lazima akili ichangamke
 
Hapana kaka naona nikihama jumla itanipa spirit zaidi ya kupambana maana kudaiwa kodi lazima akili ichangamke

Unaharibu, una sababu nyingi sana za kuwa na hiyo spirit, sio kwenda kujifesa, haya maisha sio mepesi. Bila mkakati utarudi kwa aibu.

Unauzaje simu uende kupanga? Huo ni wendawazimu, simu ni ya muhimu sana kwenye harakati zako za mahangaiko.
 
Unaharibu, una sababu nyingi sana za kuwa na hiyo spirit, sio kwenda kujifesa, haya maisha sio mepesi. Bila mkakati utarudi kwa aibu.
Kaka naamini mungu atanisimamia wacha tu nichukue haya maamuzi ni ngumu lakini naamini nitaweza
 
Unaharibu, una sababu nyingi sana za kuwa na hiyo spirit, sio kwenda kujifesa, haya maisha sio mepesi. Bila mkakati utarudi kwa aibu.

Unauzaje simu uende kupanga? Huo ni wendawazimu, simu ni ya muhimu sana kwenye harakati zako za mahangaiko.
Nitanunua kiswaswadu mkuu
 
Back
Top Bottom