Nimeamua kupaki gari nitumie usafiri wa umma

Nimeamua kupaki gari nitumie usafiri wa umma

Ruti gani hiyo isiyo na magari dar hii??
Ruti gani isiyo na bajaji?

Labda uwe unaishi ndani ndani huko labda ukifika gomz upande daladala, uje upande boda tena ...

Na asubuhi ukiwahi nauli ni rafiki na bei ileile kwenye daladala.

Anaetumia laki 4 ni pesa tu zinamuwasha au kafuga kitambi so usafiri wa umma unampa tabu
Kila mtu anatumia ambacho anakimudu. Daladala zinatesa asikuambie mtu. Mnabanana kama mahindi halafu kupatikana shida sana asubuhi.
Nilijaribu mara mojamoja kutumia daladala nikaona loh kwanini nijitese na maisha yenyewe haya.
 
wanao kaa mbagala, gongo la mboto na chanika wanafanya kazi posta na masaki japo wanalipa nauli lakini garama ya hiyo nauli kwa siku ni sawa na wanao miliki magari tu....nauli kwa mwezi laki4 mshahara laki7
Mkuu [emoji16] hata kama unakuchukia Chanika au mbagala hii too much ...nauli laki nne kweli??
Cc RRONDO
 
Kutokana na vyuma kukaza, ikanilzaimu kupiga hesabu zangu vzuri. Ninapokaa mpaka ofisini ni takribani km 10, nikienda na kurudi naweza tumia wastani wa lita nne hadi tano kutokana na hizi foleni.

Lita nne ni almost 12k to 15k. Nikitumia usafiri wa public kama bajaji natumia wastani wa 1500 kwenda na 1500 kurudi yaani 3k nenda rudi.

Sasa why nitumie 15k+ wakati naweza tumia 3k na nikafanikisha jambo langu? Nimeamua kupaki gari labda kama mafuta yatashuka bei kidogo.

Bora mpungue barabarani, ili foleni nazo zipungue...
 
Mi mwenyewe niliwahi kupiga hesabu nikagundua Kuhudumia gari ni kama unahudumia familia ya mke na watoto 3 , pikipiki mafuta ya 10k unapata lita 3 na kidogo unazunguka nayo kichizi, hata gharama ya kumlipa bodaboda ni kubwa sana nikilinganisha na mizunguko yangu
 
unaongea kirahisi sana,

utaganda kituoni hadi asubuhi kwa hizo nauli zako....


nauli ni kuanzia elfu2..
huwezi rudi na chenchi kwenye elf10
hapo hujala wala kuacha kitu home
Km unamke anaweza fungasha bites za kula vinavyoweka nutrients nyingi km mayai and nyama but they are in form of bites ,panda bajaji yako utasave vitu vjngi sn
 
Back
Top Bottom