Katika mchakato wa kujaza fomu ya usajili wa ndoa ambayo ni hati rasmi ya serikali wanandoa watarajiwa hujaza kipengere kinachoainisha muundo wa ndoa itakayofungwa yaani MONOGAMY au POLYGAMY, kipengere hiki ni mkataba baina ya wanandoa mbele ya msajili wa ndoa tarajiwa baada ya hapo wote watatu yaani (Mume, Mke na kasisi, Imam au DC) watasaini makubaliano hayo, sasa ukiachilia mbali huu mtindo wa kufanya mambo kienyeji unaoedelea ktk jamii, kimsingi huwezi kuanzisha mkataba juu ya mwingine bila kwanza kutanzua ule wa awali kisheria, hivyo endapo Mume atabadili dini na kutaka kuingia ktk mfumo wa imani ya ndoa za polygamy ni lazima ajaze fomu ya makubaliano mengine sambamba na Imani yake mpya.