Nimeamua sasa kuachana na ualimu na kwenda kusoma

Nimeamua sasa kuachana na ualimu na kwenda kusoma

Mkuu,
Unajua mchakato wa kuhama TAMISEMI?!! Tuanzie hapo..
Mkuu, ninavyojua Mimi nikishasoma either uhasibu au IT, napeleka cheti change kwa afsa utumishi kuangalia wapi Kuna uhaba ndani ya halmashauri, kama Kuna uhaba basi kufanyiwa re-categorization ni rahisi, nilipo Mimi uhaba ni mkubwa tu sio kwa IT, hata wahasibu na Sheria pia, ndio maana IT, Pamoja na wanasheria hata wakifanyiwa recategorization hawashushwi daraja hata kama ukiwa E unaendelea hukohuko.
 
kama ulikuwa unakunja laki tano kwa mwezi karume ni kitu gani kilikusukuma uache hiyo kazi yenye pesa mpaka kuamua kuomba ajira za TAMISEMI? hiyo milioni 15 umeipataje pataje mkuu huko kwenye kazi yako ya ualimu? pia unataka ukasomee IT ili upangiwe kwingine hivi unaijua sheria ya ajira za TAMISEMI kweli? maisha ni popote mkuu mtaji wako ni afya njema na akili ya kuona fursa pia mfano wa kijiwe cha kahawa kwa huo mtaji ni biashara kubwa sana sema huwezi kuelew
Dah Yani niwekeze million 15 kwa kijiwe cha kahawa mkuu, kua serious basi.
 
Wakuu baada ya kuchakata mawazo mengi sana, kuanzisha biashara au kwenda kusoma, Kwa Sasa Sina familia yoyote age miaka 26. Nimeweza na kung'amua mambo yafuatayo.

Kigoma ni sehemu ngumu kidogo kwa kufanya biashara nimeona hii hela yangu million 15 niiweke bank kwanza isije kupotea, nimewaza nikasome kitu gani ili nichomoke huku nimewaza vitu vitatu kwa uzoefu wenu naombeni muweze kunisaidia kuchakata, najua watanifanyia re-categorization lakini ni njia ya Mimi kufika ninapotaka kwenda nikimbie kidogo kwenye kushika chaki.

Nina passion kubwa ya kusoma information technology mkoa niliopo kuna uhaba mkubwa wa IT, halmashauri na mkoani pia, lakini ugumu unakuja kwenye ruhusa nimeanza kazi na degree, Nina miaka miwili kazini, then ruhusa wanatoa baada ya kukaa miaka 3 kazini, pia kwa sababu nimeanza na degree watanipa miaka 2 ya kwenda kusoma masters.

Plan A ya kwenda kusoma IT ikifeli, nimeona course ambazo open university wanatoa uwezo wa kusoma nikiwa kituo cha kazi ninao, nimewaza vitu viwili business administration (accounting) au bachelor of science in food nutrition and dietetics, nimejaribu kuchunguza OUT hawatoi bachelor ya I.T.
form six nilipata division 2 point 11. Vipi wakuu kwenu hipi itakua ni Bora zaidi?
Bora achana na ualimu kabisa kwa kuwa hufai! Yaani mwalimu uliyesomea ualimu unaandika ........ "hipi itakua" ...... badala ya ....."ipi itakuwa...
Hakika hakuna walimu siku hizi bora ondoka tu usiharibu watoto wetu.
Pack and go!
 
Kuepuka Mil 15 yako kupotea kindezi nenda kasome..
Ila unaenda kusoma ili iweje, na mbaya zaidi mpaka sasa hujui ukasome nini unataka ushauriwe!!

Kama unaenda soma ili uende kuajiriwa tena naona kama ni kama unauzinguka mbuyu tu, labda ungeenda kusoma kile kitu ambacho utajiajiri kwa namna moja au nyingine.
 
kama ulikuwa unakunja laki tano kwa mwezi karume ni kitu gani kilikusukuma uache hiyo kazi yenye pesa mpaka kuamua kuomba ajira za TAMISEMI? hiyo milioni 15 umeipataje pataje mkuu huko kwenye kazi yako ya ualimu? pia unataka ukasomee IT ili upangiwe kwingine hivi unaijua sheria ya ajira za TAMISEMI kweli? maisha ni popote mkuu mtaji wako ni afya njema na akili ya kuona fursa pia mfano wa kijiwe cha kahawa kwa huo mtaji ni biashara kubwa sana sema huwezi kuelew
Ngona nikujibu, family background niliyotoka sio nzuri, then kwa mtaji wa 1.5M ili upate faida ya laki tano inaitaji commitment kubwa mno, sijui nikuelekezaje lakini nilikua naanza harakati hapo saa 8 usiku(nilikua namwaga viatu nje), mpaka saa 3/4 mgambo wanatufukuza, then jioni saa 10 kumwaga tena hapo nje mpaka saa 4/5, Kila siku, bado kwenda minadani n.k nilivyopata ajira niliona ndio Chaka la kupatia mtaji, natamani sana nifanye biashara hasa nafaka, phone accessories na electronics, sema mkoa niliopo naona ndio unanizuia kufanya hayo, ndio maana nikapata mawazo ya kwenda kusoma, nikiweka million 5 kufanya biashara niliyokua naifanya karume huku kigoma nitakua napoteza muda tu, nitaweka site then nikae siku nzima sijauza, nitajisifuje kwamba Nina biashara?
 
Bora achana na ualimu kabisa kwa kuwa hufai! Yaani mwalimu uliyesomea ualimu unaandika ........ "hipi itakua" ...... badala ya ....."ipi itakuwa...
Hakika hakuna walimu siku hizi bora ondoka tu usiharibu watoto wetu.
Pack and go!
Wewe mwenyewe Ni bogus ?!
Unajua kiswahili wewe?? Mbona una mu attack jamaa..

Hujui kutofautisha ""BORA ONDOKA TU" au ""BORA UONDOKE TU""

😊😊😊😊
 
sema una busara ungelijibu vibaya ningejua IQ yako cha kufanya tafuta connection ya kuhamia maeneo yenye biashara na vyuo kwa ajili ya kusoma.

Na maanisha usipohama hilo eneo ukahamia sehemu zenye mzunguko wa hela kama Dar... utaenda kusoma ukimaliza utarudishwa huko huko pia hadi upewe IT au cheo chochote ni connection.

Tafuta connection ya uhamisho ama nenda kusoma ila weka akilini neno kuhama na connection.

ukiendelea kuwaza kufanyiwa re-cate utatumia nguvu kubwa halafu mwisho utakuja kukata tamaa maana mshahara ni mshahara tu hautoshi.

Nikupongeze kitu kimoja umeshagundua kuwa ajira ni utumwa. Neno mtumishi kwa mimi mwanalugha (a linguist PhD) limejificha kwenye maana ya msingi "mtu anayetumwa" yaani anayetumika kwa niaba ya mtu fulani ambaye anapata faida kukutumia anavyotaka.

Poor Brain Intelligent businessman
Ushauri mzuri.
 
Una milioni 15 lakini hujui cha kufanya unaipeleka benki wakazungushe kwenye mikopo. Kigoma sijawahi kufika lakini ukiniambia biashara ngumu huko kigoma hakuna wafanyabiashara? Wao hawaoni huo ugumu unao uona? Hakuna kitu ambacho hakina changamoto mdogo wangu ni kupambana kwa kila fursa iliyopo mbele yako.
Kigoma nimeishi miaka 6 pale mjini na Wilaya karibu zote na vijiji vyake nimefika.Kwa hoja ya biashara sikupingi hata kidogo mleta mada.Kama unataka kukimbia chaki kasome community development au sociology (ukirudi unatafuta NGO) unafanya KAZI na mashirika.Kuna majamaa Wana NGO yao walikuwa walimu saivi wanapata miradi mikubwa sana na washakuwa sana
 
Bora achana na ualimu kabisa kwa kuwa hufai! Yaani mwalimu uliyesomea ualimu unaandika ........ "hipi itakua" ...... badala ya ....."ipi itakuwa...
Hakika hakuna walimu siku hizi bora ondoka tu usiharibu watoto wetu.
Pack and go!
Sifundishi kiswahili mkuu nafundisha physics na mathematics. Sijazoea kucheza na lugha ya maandishi.
 
Wakuu baada ya kuchakata mawazo mengi sana, kuanzisha biashara au kwenda kusoma, Kwa Sasa Sina familia yoyote age miaka 26. Nimeweza na kung'amua mambo yafuatayo.

Kigoma ni sehemu ngumu kidogo kwa kufanya biashara nimeona hii hela yangu million 15 niiweke bank kwanza isije kupotea, nimewaza nikasome kitu gani ili nichomoke huku nimewaza vitu vitatu kwa uzoefu wenu naombeni muweze kunisaidia kuchakata, najua watanifanyia re-categorization lakini ni njia ya Mimi kufika ninapotaka kwenda nikimbie kidogo kwenye kushika chaki.

Nina passion kubwa ya kusoma information technology mkoa niliopo kuna uhaba mkubwa wa IT, halmashauri na mkoani pia, lakini ugumu unakuja kwenye ruhusa nimeanza kazi na degree, Nina miaka miwili kazini, then ruhusa wanatoa baada ya kukaa miaka 3 kazini, pia kwa sababu nimeanza na degree watanipa miaka 2 ya kwenda kusoma masters.

Plan A ya kwenda kusoma IT ikifeli, nimeona course ambazo open university wanatoa uwezo wa kusoma nikiwa kituo cha kazi ninao, nimewaza vitu viwili business administration (accounting) au bachelor of science in food nutrition and dietetics, nimejaribu kuchunguza OUT hawatoi bachelor ya I.T.
form six nilipata division 2 point 11. Vipi wakuu kwenu hipi itakua ni Bora zaidi?
Uhamuzi wa either kwenda kusoma au hapana na ukasome course gani inategemea na malengo yako ya baadae,unajiona wapi miaka 5 au 10 ijayo.
Hata hivyo wakati unafanya maamuzi ni vizuri kuzingatia yafuatayo ili usije kuwa dissapointed huko mbele au ukasema ningejua hiki na hiki,
(i) Ukienda kusoma course tofauti na taaluma yako ya sasa na ukaomba kufanyiwa re-categorization, ukikubaliwa unaanza na mshahara wa entry level kwenye hizo taaluma yako mpya. Hivyo ni vizuri ukajua kabisa mishahara wanayolipwa entey level kwenye hizo course unazotaka kusoma

(ii) Kufanyiwa re-categorization siyo automatic inategemea na upatikanaji wa nafasi. Unaweza kwenda kusoma course nyingine na bado ukarudi ukaendelea kufundisha
(iii) Kupewa likizo ya kwenda kusoma siyo automatic, unaweza pia kukataliwa. Uwe makini unnapoomba ruhusa kwenda kusoma course tofauti na taaluma yako, inaweza kuwa sababu ya kukataliwa hasa kama Mwajiri hana upungufu wa wataalamu kwenye hiyo taaluma

(iv) Unaweza kufikiria kusoma Post graduate au Masters ya Education ukatoka kwenye kufundisha sijui primary au secondary na kuangalia fursa nyingine. Kuna vyuo vingi tu vinahitaji Lecturer hasa kama GPA yako ya first degree ni nzuri
 
Mzee nenda kasome. Nitakupa mfano kwenye nyanja mbili nilizoziona napofanyia kazi.
1. Pesa, pesa inaongezeka, sijui huko kwenu. Hapa kwetu ukienda kusoma Master ukaleta cheti unakula Proff. Allowance ya 700k+. Na utaongezwa daraja kila baada ya miaka 2 au 3 ya kutumikia nafasi uliyonayo. Kila daraja la juu na malupulupu yanaongezeka ( hii ni sera ya ofisi)

2. Fursa nje ya ofisi. Kwetu hapa, mwezi uliopita zimekuja fursa kadhaa.
i) Zilikuja nafasi ya UN, mwenye Master ya Sheria apeleke vyeti. Kazini kwetu hakuna tumebaki tunashangaana tu.
ii) Wenye degree ya sheria na experience ya miaka kadhaa (alitaja) wapeleke vyeti wapitishwe kama mawakili wa kujitegemea (wenye certificate na diploma wakakosa).
iii) Alikuja Kiongozi, akataka wenye Masters ya Uongozi awape nafasi kusoma Chuo cha Ulinzi (wale watu wale), baadaye wapewe nafasi serikalini huko. Hakuna mtu, hii nafasi iliwauma watu wengi sana.
 
Uhamuzi wa either kwenda kusoma au hapana na ukasome course gani inategemea na malengo yako ya baadae,unajiona wapi miaka 5 au 10 ijayo.
Hata hivyo wakati unafanya maamuzi ni vizuri kuzingatia yafuatayo ili usije kuwa dissapointed huko mbele au ukasema ningejua hiki na hiki,
(i) Ukienda kusoma course tofauti na taaluma yako ya sasa na ukaomba kufanyiwa re-categorization, ukikubaliwa unaanza na mshahara wa entry level kwenye hizo taaluma yako mpya. Hivyo ni vizuri ukajua kabisa mishahara wanayolipwa entey level kwenye hizo course unazotaka kusoma

(ii) Kufanyiwa re-categorization siyo automatic inategemea na upatikanaji wa nafasi. Unaweza kwenda kusoma course nyingine na bado ukarudi ukaendelea kufundisha
(iii) Kupewa likizo ya kwenda kusoma siyo automatic, unaweza pia kukataliwa. Uwe makini unnapoomba ruhusa kwenda kusoma course tofauti na taaluma yako, inaweza kuwa sababu ya kukataliwa hasa kama Mwajiri hana upungufu wa wataalamu kwenye hiyo taaluma

(iv) Unaweza kufikiria kusoma Post graduate au Masters ya Education ukatoka kwenye kufundisha sijui primary au secondary na kuangalia fursa nyingine. Kuna vyuo vingi tu vinahitaji Lecturer hasa kama GPA yako ya first degree ni nzuri
Mkuu Asante sana kwa muda wako, nitakujibu kama ifuatavyo, IT hapa wa manispaa wako wawili tu, then wanaobaki kama wanne wanajitolea, pia hata uhasibu bado kuna upungufu juzi walitoa tangazo kama Kuna walimu wenye hiyo fani na vyeti wapeleke wanafanyiwe recategorization lakini hakuna hata mmoja aliepeleka, kwahiyo nafasi ya kwenda kusoma na kufanyiwa recategorization kwa miaka hii mitatu kuanzia sasa naiona, maana hata hao It na accountant wengi inakua ni njia tu na wao wanawaza kwenda taasisi zingine, Kuna rafiki yangu ni mmoja ni accountant hapo anataka kuhama lakini mkuu wa idara kamkatalia kwasababu Kuna upungufu bado.

Kwa halmashauri IT pamoja na wanasheria wakifanyiwa recategorization wanaendelea palepale, mshahara hawarudishi nyuma lakini kwa idara nyingine zote wanarudisha nyuma, mfano sasahivi Niko TGTS D4 823,000/= baada ya miaka miwili naingia E then napata 1,000,000=/ nikisoma uhasibu basi watanirudisha D ya uhasibu, lakini nadhani huko at least kuliko kwenye ualimu.
 
Back
Top Bottom