Mzee nenda kasome. Nitakupa mfano kwenye nyanja mbili nilizoziona napofanyia kazi.
1. Pesa, pesa inaongezeka, sijui huko kwenu. Hapa kwetu ukienda kusoma Master ukaleta cheti unakula Proff. Allowance ya 700k+. Na utaongezwa daraja kila baada ya miaka 2 au 3 ya kutumikia nafasi uliyonayo. Kila daraja la juu na malupulupu yanaongezeka ( hii ni sera ya ofisi)
2. Fursa nje ya ofisi. Kwetu hapa, mwezi uliopita zimekuja fursa kadhaa.
i) Zilikuja nafasi ya UN, mwenye Master ya Sheria apeleke vyeti. Kazini kwetu hakuna tumebaki tunashangaana tu.
ii) Wenye degree ya sheria na experience ya miaka kadhaa (alitaja) wapeleke vyeti wapitishwe kama mawakili wa kujitegemea (wenye certificate na diploma wakakosa).
iii) Alikuja Kiongozi, akataka wenye Masters ya Uongozi awape nafasi kusoma Chuo cha Ulinzi (wale watu wale), baadaye wapewe nafasi serikalini huko. Hakuna mtu, hii nafasi iliwauma watu wengi sana.