Nimeamua sasa kuachana na ualimu na kwenda kusoma

Nimeamua sasa kuachana na ualimu na kwenda kusoma

Niko manispaa mkuu, mjini hapa, at least ninakuelewa, ningepata nafasi ya kuhama kwenye manispaa au majiji nisingefikiria kwenda kusoma maana ningeanzisha biashara immediately, lakini akili haijatulia kwa sababu sioni fursa za biashara kabisa, mji mgumu huu, Bora kasulu kuliko mjini hapa.
Kama Kasulu kuna fursa kwa nini usiombe uhamisho uende huko?
 
Nimetenga mpaka 1.5 m nihame huu mkoa, nifike hata kibaha tu lakini Ngoma imekua ngumu, nadhani kwa sababu sijampata mtu sahii wa kunifanyia mchongo.
"As long as" huko ndani ya ajira tena ajira ya ualimu hutoboi na utakuwa masikini milele! Chukua maamuzi magumu huku ukimtanguliza Mungu! Umesema hujaoa na hela ya mtaji unayo! Maeneo ya mbezi mwisho ni maeneo mapya yenye msongamano mkubwa wa watu na wengi zaidi 75% ni wageni (hakuna uswahili)! Tafuta chumba cha karibu upange anzisha biashara ya vyakula. Ukipata watu sahihi utakaowaajiri utatoboa!
 
Shukrani sana mkuu nimekuelewa.
 
Optimists
Mkuu nafikiri ukiweza fanya michakato ya kusoma nje haswa Western countries, yaani endelea na masters.. NI vema Sana Kama unampango was kufanya kazi hukohuko.

1.. Tafuta nchi ambazo Zina sera nzuri za kufanya kazi na maswala mazima ya uhamiaji Kwa wageni.
2.. Nchi zinazotoa government scholarship, zinazokubali kiurahisi mifumo ya elimu ya Tanzania

DOKEZO: Sweden...
✓Wana government full funded scholarship.
✓Tanzania ni eligible
✓No English test
✓ minimum ni 2 years of work experience
✓Centralized University application system
✓Hulazimishwi kurudi in your home country baada ya kumalizia masomo

Zipo nyingi mfano Canada,USA,German
 
Zipo nyingi mfano Canada

NB : ziwe Western countries
 
Shukrani sana Mkuu, ngoja niwaze kwa upande huu, sijawai kufikiria kabisa.
 
sema una busara ungelijibu vibaya ningejua IQ yako cha kufanya tafuta connection ya kuhamia maeneo yenye biashara na vyuo kwa ajili ya kusoma.

Na maanisha usipohama hilo eneo ukahamia sehemu zenye mzunguko wa hela kama Dar... utaenda kusoma ukimaliza utarudishwa huko huko pia hadi upewe IT au cheo chochote ni connection.

Tafuta connection ya uhamisho ama nenda kusoma ila weka akilini neno kuhama na connection.

ukiendelea kuwaza kufanyiwa re-cate utatumia nguvu kubwa halafu mwisho utakuja kukata tamaa maana mshahara ni mshahara tu hautoshi.

Nikupongeze kitu kimoja umeshagundua kuwa ajira ni utumwa. Neno mtumishi kwa mimi mwanalugha (a linguist PhD) limejificha kwenye maana ya msingi "mtu anayetumwa" yaani anayetumika kwa niaba ya mtu fulani ambaye anapata faida kukutumia anavyotaka.

Poor Brain Intelligent businessman
Mimi ninakuelewa ila post yako ya kwanza kwenye mada imebeba mawazo na fikira zoote za huyu dogo.

Mimi nitakuwa wa mwisho kumshauri ijapo ninaamini anayo maamzi tayari.
 
Narudia Tena mkuu, siwezi invest million 15 alafu nikauza 60,000/= kwa siku na Mimi nikajitapa kwamba Nina biashara huo ni ujinga, ningekua kwenye miji mikubwa ungenishangaa sana, lakini kwa kigoma ndio nimeshindwa ning'amue nifanye nini, nimefanya biashara dar kwa mtaji wa million 1.5 nilikua nauza viatu hapo karume kwa mwezi nilikua sikosi laki 5 hapo nimeshafanya kila kitu, hapa nazingumzia kigoma, hizo idea za kufungua kijiwe cha kahawa sio mambo yangu ndoto zangu ni kubwa zaidi ya hizo.
 
Shukrani sana mkuu, kwa sababu ndoto zangu ilikua ni IT na nikaona open university hawatoi hiyo kozi upande wa degree, ndio nikaja na hiyo idea ya uhasibu.
Screenshot_20240412-211858.jpg

Siku nyingene fanya research vizuri open wanatoa degree ya IT We jiandae TU muda ukifika uombe usome
 
Kwanza mkuu nikwambie kitu kimoja. Huwezi kufanya biznez ukiwa upo kazini. Hilo ni gumu kama huna msaidizi mwenye uelewa wa biashara. Biashara inahitaji ujitoe kweli kweli ikiwezekana uache kabisa ajira. Na ukifikia hatua ya kuacha ajira na kuingia kwenye biashara, basi nakuhakikishia una miaka miwili tu ya kuhusle, baada ya hapo itakuwa history.

Kuhusu kusoma naona ni mule mule tu. Ajira ni ajira hata kama upo TRA. Nakushauri ujitoe muhanga japo ni ngumu kwa sababu unadaiwa umeshachukuwa mkopo. Kusoma unapoteza muda.
 
Nimeangalia Nimeikosa mkuu, wanatoa kwa ngazi ya certificate sio degree.
Ipo nadhani umeshindwa kuona tu,inaitwa bachelor of Science in information communication and technology (ICT)

Ingia kwenye tovuti ya OUT then fungua kwenye menu then ingia academics then faculties then bofya faculty of science,technology and environmental studies (FTES) mwisho ingia kwenye undergraduate programmes utaona orodha ya bachelor degrees zinatolewa ikiwemo hiyo na data science na zinginezo
All the best
 
Attachments

  • Screenshot_2024-04-12-23-01-12.png
    Screenshot_2024-04-12-23-01-12.png
    210.7 KB · Views: 6
Nakushauri nenda kasome Course inaitwa HSM(Health Service Management) Ukatibu wa Afya inapatikana Mzumbe University na St John University sijajua kama UDOM wameanza kutoa.
Faida yake ni kwamba ukifanyiwa Recategorizing Salary haitoshuka wanatumia viwango vyao vya Salary ambavyo nitofauti vya Food n Nutrition ambavyo salary Yao iko chini.
Pia IT ni nzuri sana na wakikufanyia recategorizing hutoathirika Salary wananzia TGS E ambayo ni Million na kidogo.
Mm nimesoma Degree ya Educationa nimeona NILIKOSEA nimeamua kurudi tena kusoma Health Service Management namaliza mwakani, ila ni msoto mkali sana aisee no Boom lakini najua nilimaliza tu nitakuwa pahala sahihi sana.
Health service? Management ?
Mkuu hiii kozi mzumbe haipo
Pale inaitwa Health system management, yaani unasoma afu ata jina la kozi yako hulijui?
 
Watu wanatoboa na milioni moja mkuu...ni mipango mizuri na target tu✊🏽
Nyie watu mnaongea tu hamuijui kigoma vzuri... mm namuelewa jamaa kwasbb nimeishi kigoma huku hata uwe na million 100 kama sio mwenyeji wa kigoma inaweza kuisha bila ww kujua...!!! Ww mkoa wachanga wameushindwa unafikiri kuna biashara hapo
 
Back
Top Bottom