Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Mkuu huyu mtu wa makamo aliyeleta mada ndio unamtusi namna hii? Nadhani kuna haja ya kulumbana kwa hoja na sio kwa mihemko.
 
Mbona hii comment ina rafudhi na man'dhari ya Mama?!
 
Haiwezi kuwa filamu nzuri kwa jinsi ilivyoandaliwa kisiasa.Umewahi kuona wapi Rais wa nchi maskini akaandaa filamu tena kwa kuongozwa na mzungu?
Tumepigwa kama kawaida yetu:Shamba la Bibi hili.
 
Kama wewe unaliona hili kwa mlengo huo, huo ni uamzi wako.
Unapolenga kutupiwa hicho kidogo na kuridhika, huku ukiwa wewe ndiye mwenye mali, na haikuumizi kabisa!

Tabia hii imeota mizizi sana hapa nchini, 'low expectation' imekuwa ndio utamaduni wetu.

Kwa nini umtegemee mtu mwingine akutafutie watalii awalete kwenye kivutio chako ambacho yeye hana? Yeye anapata mara dufu kwa kupandia kwako, na bado unaona raha tu?
 
Haiwezi kuwa filamu nzuri kwa jinsi ilivyoandaliwa kisiasa.Umewahi kuona wapi Rais wa nchi maskini akaandaa filamu tena kwa kuongozwa na mzungu?
Tumepigwa kama kawaida yetu:Shamba la Bibi hili.

..documentary sio ya kisiasa ukiacha sehemu ambayo wanam-introduce Raisi.

..tatizo langu ni vivutio walivyovitangaza.

..Kwa mtizamo wangu ni vivutio ambavyo kwa kiasi kikubwa tayari vinajulikana.

..Nilitegemea wataonyesha na baadhi ya vivutio ambavyo havijulikani vya kutosha kwa mfano mbuga za Gombe, Ruaha, Ziwa Victoria, etc.
 
UTALII UPO MIAKA 60 YA UHURU HAKUNA JIPYA
 
Sijaiona hiyo filamu, lakini ukosoaji wako sio sahihi, ungekosoa namna ya content labda ningekusikiliza lakini kwa uchaguzi wa attractions, no way, you are very wrong.
Mbona kafanya hivyo, au wewe ulitaka afanyeje?
Kasema wazi, huyo 'narrator' wa movie yenyewe anaonekana hana ujuzi wa kazi hiyo.

Na utasema vipi kwamba "...ukosoaji wake siyo sahihi" kama wewe mwenyewe hata hujaiona movie?
 
Mbona kafanya hivyo, au wewe ulitaka afanyeje?
Kasema wazi, huyo 'narrator' wa movie yenyewe anaonekana hana ujuzi wa kazi hiyo.

Na utasema vipi kwamba "...ukosoaji wake siyo sahihi" kama wewe mwenyewe hata hujaiona movie?

Kabla hujaelewa kitu mtu kaandika usikimbilie ku comment is
 
Lahaula .....!
Mleta mada unataka tuwape nafasi watuandalie nyingine Duh...
 
Hii hapa.
 
Kuna kituo kinaitwa safari. Kinaonyesha vizuri. Tungekitumia tu.
 
Fulani ina andaliwa kama watu wanakimbizwa yaani ndani ya miwili kurekodi na kuzindua hii lazima iwe mbaya tu
 
Naiangalia Royal Tour katika mtazamo tofauti kidogo. Kwamba SSH alitaka kurudisha mtazamo chanya kwa Tanzania huko duniani.

Unajua kuna kujulikana kwa njia mbili, mbaya na nzuri. Unaweza ukawa ni maarufu lakini ni ule umaarufu wa kukata chanjo, ni ule umaarufu wa kifo cha Akwilina, ni ule umaarufu wa kugombana na NGOs kila kukicha.

SSH ametaka kusafisha taswira hiyo na kuja na taswira nyingine chanya ya kimataifa. Kwamba yupo tayari kufuta makosa ya mtangulizi wake ingawa kwa watu wa karibu wa hayati JPM hawaoni na hawatakuja kuona kama yalikuwa ni kielelezo cha udhaifu wa awamu yake.

Hivyo Royal Tour inatumia tu kivuli cha utalii lakini lengo haswa ni katika kuleta taswira nyingine mpya kabisa kimataifa. Na imekuwa ni sinema yenye gharama zake kwa maana ya pesa nyingi na kwa maana ya SSH kujikuta akilazimika ingawa kwa shingo upande kukubaliana na hoja kwamba mtangulizi wake alikufa kwa Covid19.

Kwa ujumla nadhani lengo la muda mfupi ni hilo na la muda mrefu ni la kujitangaza upya kwa kutumia taasisi yenye jina na maarufu ndio maana wametutoza pesa nyingi kuweza kuikamilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…