Nimeanza Biashara ya Kukopesha, naomba ushauri

kuwa makini.... watanzania wengi hawakopesheki
 
Wakuu mimi kuna mtu amenikopesha 1m namlipa 70k kila mwisho wa mwezi, Hiyo riba ni kubwa au ndogo? Isije ikawa napigwa[emoji85][emoji3]
Kwa miaka mingapi?
 
Wakuu mimi kuna mtu amenikopesha 1m namlipa 70k kila mwisho wa mwezi, Hiyo riba ni kubwa au ndogo? Isije ikawa napigwa[emoji85][emoji3]
Fair sana, ila hujasema ni kwa muda gani hilo rejesho la mkopo.
 
nakusanya Marejesho daily kama 8,000

kwa wiki nalaza elfu 50 mpaka 60

Huu mwaka lazima tununue kiwanja.

hizi bukubuku ni za mama muuza genge😅😅

bado wa vitumbua

 
kuwa makini.... watanzania wengi hawakopesheki
Kuna wamama wa vikundi huwa wananifuata sana.

mfano mchana huu huu, kaja mmoja anataka laki aende aka top up achukue mkopo mara 2 huko kwenye kikundi chao.

Aisee nimempa 50,000

utaratibu wake ni kwamba akichukua anarejesha kesho yake Tsh 60,000😃😃😃

hapo ndo mtaniua sasa kwa maneno. Wengine wanakuja kesho kama wawili hivi na mimi nimeishiwa Cash ndani.
 
nadhani neno biashara kichaa lilitokea huku. Watz wengi hatuna culture ya kukopa na kulipa

hapo riba zao kila mmoja 20%

Jamani kila mtu atafute fursa tusibezane wala kupeana maneno ya kurudishana nyuma

edited...

riba imerudi chap kwa mama wa 100k na mkopo umeendelea..

wa 60k karudisha 72,000
 
HakyaMungu mi ntatumia ukurya wangu kumkarabati mtu/watu wa hivyo

umafia utatumika kudili na watu kama hao sitakubali kufilisika kizembe[emoji28][emoji28]
Umafia ndiyo utakaribisha kufirisika.

Mara zote "umakame nguvu" humfanya mtu ajute baada ya kutenda.

Ukishamfanyia umafia mtu, tayari milango mingine ya kihalifu(Polisi na mahakama) inafunguka na kubakia wazi.

Je haujatapanya pesa zako za mtaji kujiokoa ili kuifunga milango ya gereza kwa pesa isikumeze mzima mzima?
 
nakusanya Marejesho daily kama 8,000

kwa wiki nalaza elfu 50 mpaka 60

Huu mwaka lazima tununue kiwanja.

hizi bukubuku ni za mama muuza genge[emoji28][emoji28]

bado wa vitumbua

View attachment 2159389
Kungelikuwa na utaratibu wa kukata % kwa noti chafu chafu, waTz tungejifunza kuhifadhi pesa.

Sasa tatizo noti chafu na noti safi thamani yake ni sawa!
 
Toka nimeomba unipe abc umegoma mkuu😆
 
Toka nimeomba unipe abc umegoma mkuu😆
Sijagoma mkuu nabaishwa na maneno ya wachangiaji.

kama unataka kuanza, anza na wamam unaowajua vizuri, wawe ba makazi ya kudumu!

Anza pole pole tu utafika mbali..
 
Umafia sio wa kiwango hicho mkuu

Mi huwa nakubaliana na niliemkopesha anaweka kitu bondi chenye thamani mara 2 ya mkopo wake.

akifeli achague moja, kuleta riba aunge mkopo ama tuuze bondi..

kokudo get this noted
 


hapo kuna faida ya 32,000 kwa wiki moja kutoka kwa wateja wawili tu.

bado wengine watano this week
 
Kwanini unakopesha kwa riba ?

Lengo lako kuwasaidia au kupata pesa kupitia wao ?
 
View attachment 2159740

hapo kuna faida ya 32,000 kwa wiki moja kutoka kwa wateja wawili tu.

bado wengine watano this week
Amini unachokifanya hii biashara naikubali sana japo niliingia cha kike kukopesha wahuni wakanizima laki mbili yangu hadi leo hii ukiwatafuta hawapatiakani ukipiga simu hawapokeii aisee ila sijakata tamaa bado naendelea nayo

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kwanini unakopesha kwa riba ?

Lengo lako kuwasaidia au kupata pesa kupitia wao ?
Nafanya biashara ya pesa mkuu. Kama zilivyo benki zote za biashara

riba zangu ni kwa siku 7 unaleta elfu 2 kwa kila elfu 10 unayochukua.

kuna wengine wanachukua kwa siku 3, 4 mpaka 5 lakini interest iko palepale.


nakusanya hio hela kutoka kwa wakopaji wadogo wale wa teni teni every day.

Nashukuru Mungu mtaji umekua kwa kasi sana kutoka 100,000 mpaka sasa inagonga laki 6.

nakopesha wale ninaowajua kiundani.

nisiowajua wanaweka vitu bondi.

CHANGAMOTO
mpaka sasa changamoto yangu ni mtaji umepungua wakopaji wamekuwa wengi, tena wale LEGIT wanaoletwa na wateja WAKONGWE.

imagine kama jana kuna mmama kaletwa anataka laki 1, arudishe 120k leo.

nilishangaa sana lakn nilipouliza kiundani waliniambia wanaenda ku top up mkopo wao kwenye kikundi na huwa wanafanya hivyo ili WAPATE MIKOPO MARA 2.

Hii biashara inalipa ila inahitaji uwe mtu makini sana.

SIO KILA MTU NI WA KUKOPESHA
CHUNGUZA KABLA HUJAKOPESHA.
ULIZA ULIZA KWA WANAOMJUA

kokudo note something
 
😋Asante mkuu naendelea kujifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…