#COVID19 Nimechanja chanjo ya COVID-19 jana na niko salama

#COVID19 Nimechanja chanjo ya COVID-19 jana na niko salama

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Jana baada ya waheshimiwa kupata chanjo yao, nami nikaingia chemba kuipata rasmi. Nimechanjwa hii chanjo ya Jonson and Jonson kama hatua moja ya kinga ya ugonjwa wa corona.

Nia ya bandiko hili ni kuwajulisha ninavyoendelea kadri siku zinavyokwenda.

Mpaka sasa na leo niko salama na nita update mara moja au mbili kwa wiki kadri siku zinavyokwenda.

Mwenye swali tafadhali.

DAY 3: MYTH QUASHED
Nimeweka shilingi nilipochoma sindano, Shillingi haigandi, inaanguka.

DAY 14: Wakuu bado nipo nipo tu, sija dedi!
Johnson and Johnson inafanya kazi yake
 
Sisi pia kwenye kampuni moja ya kitalii nimechanja ni mwezi wa pili sasa huu na niko fresh kabisa.
Tena nimechanja Astra zeneca (uk)ambayo wengi wanasema inawalakini
Watanzania tuchanje asee
umesha jaribu na kutafuta mtoto baada ya kuchanjwa mkuu? maana ndio wasiwasi mkubwa Africa
 
Kwanza hakuna uthibitisho wowote kwamba umedungwa hilo lichanjo. Huenda unaigiza tu ili watu wasio na hatia waingie mkenge na kushawishika kudungwa hayo masumu.

Halafu pili, madhara ya chanjo huwezi kuyapima kwa siku moja. Ndio maana hata majaribio ya chanjo yanafanywa kwa miaka nane mpaka kumi ili kubaini athari zake za muda mfupi na mrefu.

Kiufupi umedungwa sumu za majaribio, na hatujui nini kitakupata ndani ya miezi ama miaka kadhaa.

Jiandae kwa matokeo hasi ya aina yoyote na usimlaumu yeyote.
 
Jana baada ya waheshimiwa kupata chanjo yao, nami nikaingia chemba kuipata rasmi.
Nimechanjwa hii chanjo ya Jonson and Jonson kama hatua moja ya kinga ya ugonjwa wa corona.

Nia ya bandiko hili ni kuwajulisha ninavyoendelea kadri siku zinavyokwenda.

Mpaka sasa na leo niko salama na nita update mara moja au mbili kwa wiki kadri siku zinavyokwenda.
Mwenye swali tafadhali.
Mkuu hongera ila mimi Kama ni hiari sizani kama ntakubali hio kitu wazungu sio wenzetu bro
 
Miaka 15?
Chukua tahadhari mkuu, watu wameupata ugonjwa wa covid Delta variant, siku mbili tu hawapo.Dont take chances!
Wewe dalali wa chanjo, acha vitisho uchwara.

Hakuna cha delta variant wala bibi yake na delta variant. Mtaani watu wako salama na wanaendelea na maisha yao ya kila siku.

Haya ni maigizo tu kama futuhi zingine.
 
Kuamini au kutoamini kuwa nimechanja , litabaki kuwa tatizo lako na sina haja ya kufanyia propaganda ukweli ninaoeleza.
Anafanya maigizo huyu! Yeye amedungwa juice ya embe, hapa anataka kuwaingiza watu mkenge wakapewe ile yenyewe.
Wewe dalali wa chanjo, acha vitisho uchwara.

Hakuna cha delta variant wala bibi yake na delta variant. Mtaani watu wako salama na wanaendelea na maisha yao ya kila siku.

Haya ni maigizo tu kama futuhi zingine.
 
Ni mapema sana kutoa ushuhuda kuhusu chanjo hiyo. Hebu rudi tena hapa utupe mrejesho baada ya miezi mitatu hivi.
 
Back
Top Bottom