Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Itabidi tuachane na JF kama hii siyo chai. Mama yako bado binti umri haujaenda
 
Fanya utafute taasisi zinazohusika na kuwatunza, kuwashauri waathirika wa madawa ya kulevya. Hapo ndio unaweza kwenda polisi ili wawasaidie kumpeleka kwenye hizo nyumba za malezi. Kabla ya hapo, jaribuni kuyaondosha mapanga, jembe au chochote mnachohisi anaweza kukitumia na kuwadhuru. Poleni sana kwa changamoto hiyo!
 
Hizo taasisi ni bure? Maana nimeonaa inahitajika laki 3
 
Ni Sawa ila kwa namna yake ni mtu Mzima tayari
Sawa ni mtu mzima siyo umri umeenda! Umri mkubwa ni kuanzia 90 huko. Mama yako bado kabisa maana angekuwa amestaafu miaka 2 iliyopita. Na kama angalikuwa ni mwalimu wa chuo kinachoitwa University na amefika level ya juu kitaaluma angekuwa amebakiza miaka 3 kustaafu. Je, ni halali mtu wa aina hiyo kusema umri umeenda?
 
Tupo Dar ila huo uwezo wa kulipia kila mwezi laki 3 hatuna
Nenda ofisi za ustawi wa jamii hapo manispaa uliyopo muombe msaada wa vituo vinavyo toa hiyo huduma bure kwa msaada.
Au nenda ofisi ya ustawi jamii kwenye hospital kubwa kama Muhimbili, Mlonganzila, Amana Hospital Ilala, Temeke hospital, Mwananyamala hospital, Mnazimmoja, n.k.
Nenda kaombe msaada wa maelezo unawezaje kupata huduma hiyo kwa msaada wa wasiojiweza.
 
Huyu huwezi kukaa nae ukaongea… kuna mkubwa wetu alijaribu yaani ni anapandisha anakuwa juu na kukutukana juu
mimi naamini akifuatwa kwa namna sahihi akakalishwa chini bila kulahumiwa kwa anayoyafanya apo nyumbani atawasikiliza tu.

Tatizo anahisi mnataka mumfukuze apo nyumbani ndiomaana anapandisha na kuwa mkali, ata ungekuwa wewe kwenye viatu vyake lazima ungekuwa mkali tu.

Huyo kwenye maongezi yenu msimwambie habari za kuhama nyumbani mtazidi kumchanganya. Maongezi yenu yajikite zaidi kumtia moyo na kumuaminisha kuwa bado anayo nafasi nyingine ya kuanza upya maisha yake.
 
MAOMBI
MAOMBI
FUNGA NA KUSALI
IBILISI UTAMSHINDA
 
kamrepoti polisi awekwe kwa ndani kwa usalama wake pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…