Nimechoshwa na Huu umungu mtu unaooneshwa na serikali! Mpaka Sasa Mshahara haujatoka? Mnatuchukuliaje?

Mshahara tukikubaliana ulipwe kila baada ya siku thelathini, let say kuanzia siku ile unayoanza kazi, basi hii hesabu yako ya tarehe 1 kila mwezi itakufa automatically.
Siku thelathini gani?

Mishahara ya serikali inalipwa kwa kuangalia calendar month.

Serikali ikikulipa mshahara wa mwezi June kabla mwezi June haujaisha, hiyo ni favor tu. Wanajiwahi wenyewe wasicheleweshe mshahara. Mshahara una accounting processes zake za payroll zinachukua siku kadhaa ku clear kibenki. Wakitaka kujiwahi wasipitilize tarehe 1, ndiyo wanaanza kulipa wiki moja kabla au hata zaidi ya hapo.

Hawana obligation ya kukulipa mshahara wa June kabla mwezi June haujaisha. Mshahara wa June unatakiwa kuanza kulipwa July 1.

Ukija hapa July 2 unalalamika hujalipwa mshahara wa June nitakuelewa.

Ukidai mshahara wa June kabla mwezi wa June haujaisha, hapo unaomba advance ya mshahara, hudai mshahara.

Kwa sababu mwezi wa June haujaisha.
 
Mshahara unaoudai ni wa mwezi gani?

Mwezi wa tano au wa sita?

Kama wa mwezi wa sita, mbona mwezi una wiki moja bado kuisha?
Jamaa unakaza sana fuvu, ili ustahiri kulipwa mshahara inatakiwa uwe umefanya kazi kwa siku zisizopungua 15 kwa mwezi sasa mwezi Mei mshahara uliingia tarehe 21 maana yake kufikia tarehe 21 Juni tunakuwa tumetumikia siku 30 kuongeza siku 3 mbele kiutumishi na kwa kufuata standing order tunakuwa tumekopwa! Haiangaliwi tarehe ya mwisho wa mwezi Bali siku na masaa unayostahiri kufanya kazi ili ulipwe.
 
Watumishi walilipwa May 22 baada ya hapo mnataka wakaibe hizo Siku ambazo hamjawalipa mtawafidia vipi Mbona ni rahisi tu serikalini inawakosea watumishi kwa kukaa kimya kwani wametimiza wajibu wao
 
Punguza hasra mkuu muelewesh mambo ya upinde ya nn tena.
 
Franky
 
Kwanza neno sahihi no stahili, si stahiri.

Pili, toa hiyo standing order unayoisema, iweke hapa tujifunze

Nina Standing Orders for the Public Service going back to PS George Yambisi ya 2009.

Weka vipengele hapa usinukuu jumlajumla.
 
Sema kwa wengine ni changamoto,binafsi nimeweka utaratibu wa kutotegemea mshahara na iwe jua ama mvua lazima niwe na akiba ya kutosha
 
Tumekumiss Swahiba! Tumia Tembocard yako kufanya malipo mtandaoni au kwenye CRDB POS machine bila gharama yoyote. Swahiba langu lako
 
Sema kwa wengine ni changamoto,binafsi nimeweka utaratibu wa kutotegemea mshahara na iwe jua ama mvua lazima niwe na akiba ya kutosha
Wanawake ni kawaida, wanaume majukumu ni mengi sana huo mshahara ndio wenzako wasiofanya kazi wanautegemea ili wautunze akiba kama wewe haturingani.
 
Hahahaha..
Kazi ipoo
 
Tumekumiss Swahiba! Tumia Tembocard yako kufanya malipo mtandaoni au kwenye CRDB POS machine bila gharama yoyote. Swahiba langu lako
Sijawahi kuwa na Tembocard na kamwe sitaitaka.
 
Favour kivipi ikiwa mfanyakazi anakuwa amefanya kazi kwa 30 days?!

Hata kama ukisema wanajiwahi wenyewe, huko kujiwahi si kunafika baada ya siku thelathini? sasa hapo favour inakuja vipi?

Kama ni suala la favour, basi huko kujiwahi kwao wafanye after 20 days mfanyakazi apate chake.
 
Wanawake ni kawaida, wanaume majukumu ni mengi sana huo mshahara ndio wenzako wasiofanya kazi wanautegemea ili wautunze akiba kama wewe haturingani.
Umesema ukweli,wanaume kukaa na pesa ni ngumu sana,Mr alikuwa anasema siwezi weka akiba maana ntaitumia tu .Mambo ni mengi japo anafanya maendeleo ila kuna mda unakuta kafulia hatari.Baada ya kujua hayo mimi ndo nikawa mweka akiba kwa hiyo hali ikiwa tete namuokoa japo mara nyingi namwambia nimekopa kwa ndugu yangu ili arudishe akiba yangu iendelee kukaa.
 
Kumbe ndo huwa unamfanyia ndugu yangu hivi , ngoja nitamshutua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…