Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Siku thelathini gani?Mshahara tukikubaliana ulipwe kila baada ya siku thelathini, let say kuanzia siku ile unayoanza kazi, basi hii hesabu yako ya tarehe 1 kila mwezi itakufa automatically.
Mishahara ya serikali inalipwa kwa kuangalia calendar month.
Serikali ikikulipa mshahara wa mwezi June kabla mwezi June haujaisha, hiyo ni favor tu. Wanajiwahi wenyewe wasicheleweshe mshahara. Mshahara una accounting processes zake za payroll zinachukua siku kadhaa ku clear kibenki. Wakitaka kujiwahi wasipitilize tarehe 1, ndiyo wanaanza kulipa wiki moja kabla au hata zaidi ya hapo.
Hawana obligation ya kukulipa mshahara wa June kabla mwezi June haujaisha. Mshahara wa June unatakiwa kuanza kulipwa July 1.
Ukija hapa July 2 unalalamika hujalipwa mshahara wa June nitakuelewa.
Ukidai mshahara wa June kabla mwezi wa June haujaisha, hapo unaomba advance ya mshahara, hudai mshahara.
Kwa sababu mwezi wa June haujaisha.