Tatizo ni masharti ya walimu kujiajiri. Serikali imeweka masharti magumu mno ya MTU binafsi kumiriki shule. Masharti yote yanafeva matajiri. Kuna watu wanamajengo mitaani, wanakubalika na watu lakini hawakubaliki na serikali na hivyo kutokuwa walipa kodi. Sheria hizi zinazalisha watu wanaoichukia serikali bila sababu, na lazima serikali itambue kwamba haiwezi ajiri kila mtu.
Nchi hii unakuta kijana ni daktari, lakini ni bodaboda, kwa sababu masharti ya kufungua zahanati ni magumu mno, cha ajabu mganga wa kienyeji anaruhusiwa kuendesha huduma hata kwenye banda LA nyasi lakini kijana aliyesomeshwa na serikali tunamuwekea masharti yanayomtia umaskini.
Tanzania kijana amemaliza digrii ya sheria lakini si mwanasheria mpaka aende shule ya sheria kwa nini hicho kinachotolewa kwenye shule ya sheria wasifundishwe watoto zetu ili baada ya digrii wapate mihuri ya mahakama na kujiajiri?
Nchi hii ina sheria nyingi zinazozalisha wazururaji. Tengenezeni sheria zinazowasaidia watu waanzie pale walipo ili kusonga mbele maadamu watu hao wataaminiwa na jamii inayowazunguka. Tusaidieni watanzania, asilimia kubwa ya hawa vijanaa wataalam wametoka kwenye familia maskini. Serikali ikiwasaidia hawa pia itakuwa imezalisha walipa kodi.