Nimechukia sana kukosekana kwenye ajira za jana. Nina jazba sana nimekata tamaa

Kuna makosa mengine yanahitaji mda mrf kuyarekebisha na sio kwa siku kadhaa, mfano suala la ajira kuna graduate zaid ya laki tatu waliolimbikizwa mtaani na mwendazake, kuwapunguza hawa mpk waishe is not overnight process.
Simple tu, atleast warudishe ule utaratibu wa zamani kuwachukua wote wanaotoka vyuoni, at the same time, waache private schools ziwe na uwezo wa kuajiri walimu wanaomaliza toka vyuoni, huku wakiendelea kuongeza idadi ya walimu mpaka shule zenye uhaba huko vijijini.
 
Walimu waanzishe chama chao cha siasa kipiganie haki zao. La sivyo wataendelea kuburuzwa kila siku.
 
Alishapendwa na mama Janet ikamtosha...yaani wewe utasugua benchi hadi akili uzi reset
 
Ni kweli lakini pia lazima kuwe na udhibiti ukiruhusu masharti "rahisi" kwenye sekta kama ya afya utatengeneza tatizo kubwa zaidi.Kwahiyo udhibiti lazima uwepo.
 
Mzee mbona unanishambulia mimi[emoji23][emoji23]
Mimi nimeuliza tu, kwanza sijasoma ualimu pili nimejiajiri toka 2014..
Nilitaka nijue tu ukubwa wa tatizo.
Sorry bana, ila nawachana tuu haoo hkl wanaonyata kitaa na suti & tai hawawez endesha hata boda et it is too risk afu wana na engineering zao wana hustle kitaaa hata kama kaz n ya kuchafuka na oil😂😂😂
 
Jamani mkiona vijana wengi wanalia ajira maana yake sekta binafsi imekufa, ni nadra sana popote duniani serikali kuajiri watu wengi......
 
Pole sana ndugu. Kwanza ningekusihi kuacha kulaumu. Ajira hata wangesema kwa 2016 pekee sidhani kama wote wangepata.

Lakini pia kumchukia mtu, ambaye hata hayupo ni kujiumiza tu upate vidonda vya tumbo bure. Nikushauri vitu vichache
1. Acha kulaumu na ukubaliane na matokeo
2. Ujue kila mlango unaofungwa kuna mwingine unakuwa umefunguliwa. Mwamini Mungu kuwa amefungua mlango. Kazi yako ni kukaa na kutumia ubongo ambao Mungu amekupa kujaribu kutafuta ufunguo wa mlango uliofunguliwa
3. Tafuta kukaa na watu ambao wanawaza kutatua shida hii na sio wanaolalamika
4. Anza na ulicho nacho, usikidharau. Inaweza kuwa ni watu, kuuza vitu vidogo vidogo au kitu kingine. Kuna kipawa Mungu alikupa anza nacho hicho.
5. Ikiwezekana achana na mambo za kuomba ajira. 2016 ni muda mrefu sana, inawezekana huko sio ulikoitiwa. Jaribu kitu kingine.

Mungu akutie moyo na kukuongoza!
 
Capital is Man Made

Refer to Capital formulation and accumulation concepts as well!!

Mtaji lazima uutengeneze, uulee na uutunze kwa gharama zako
Niko foleni hapa Kijibuzi stationery kwa ajili kuifanyia lamination hii comment yako mkuu.
 
Ghafla ghafla hvyo mkuu itakuwa ngumu kumbuka mwendazake pamoja na cousin wake walikomba kile kibubu kwa miradi ya ovyo ovyo isiyo na tija
 
Mfano ebu cheki ni mabilion mangapi yaliyotumika kufanikisha ile issue ambayo watu wanataka watumie kuanikia mazao
 
 
Muongo sana wewe Taga. Ni mwaka upi wa kikwete alioajili walimu wachache,si wote?
 
Angalau kikwete alikuwa anaajiri kila mwaka wahitimu wapya,ila mwendazake miaka sita hajawahi kuajiri MTU kwa hiyo wamejazana mitaani hakuna ajira labda ukajitoleekale kababa kalikuwa na roho ngumu mpaka ikaongezewa uzito Wa pacemaker.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…