Pole sana. Ufupi wapo mpaka waliohitimu masomo ya sayansi na hesabu mwaka 2019, na bado wameajiriwa. Wa 2015 wapo wengi zaidi kuliko makundi mengine. Serikali pia imeajiri wahitimu wengi wenye cheti na stashahada kuliko wale wenye shahada kwa upande wa shule za msingi! Bila shaka lengo lilikuwa ni kukwepa gharama ya kulipa mishahara.
Walimu wenye shahada wa masomo ya Sanaa (Arts) wameajiriwa wachache mpaka inakera! Anyway, hakuna namna. Kumchukia marehemu haiwezi kusaidia chochote kwa sasa. Ushauri wangu ni huu, hizo hasira zihamishie Mtaani! Naamini unaweza ukafanikiwa zaidi kimaisha kuliko hao wanao enda kuwa watumwa wa ajira miaka yao yote.
Angalia tu fursa kwa sasa na mlango wa kutokea. Ukiupata huo, hakika utakuja kujishangaa hapo baadae kwa kudhani ajira ilikuwa ni bora sana kuliko kuajiriwa. Maisha ni vita, hakikisha unapambana mwanzo, mwisho! Never give up!!! [emoji123]