Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

Usifananishe ulaya na bongo mkuu.
Ulaya mtu anapoanza kufanya kazi mshahara anaopata unakuwa ni mkubwa na umepigiwa hesabu kwa matumizi ya mahitaji yote.
Huwezi kulinganisha na bongo ambapo mishahara ni ya kunyonyana tu hata basic needs tu haijazingatia.
Kwa hayo mawazo uliyoyatoa hapo kwa huku bongo hata mkurugenzi akiyafuatisha anahangukia pua.
 
wekeza kwenye biashara.. kama unaona huna akili ya biashara kanunue viwanja vya kutosha kwa maisha bora ya baadae
 
Ulipaswa kuomba ushauri kabla hujachukua mkopo, sasa umeshachukua ndio unaomba ushauri, wa nini wakati ulishajipanga kitu cha kufahya?
 
Ina maana umechukua mkopo ila hujui vizuri ufanye nini na huo mkopo?
 
Kina msemo; Kama hudaiwi huna akili.
Jamaa anaogopa kuitwa kilaza.
Alipoona kabanwa kwa idea yake akajiongeza na kusema ooh nina vitega uchumi na huku anasema mshahara huwa siugusi kabisa
Sasa najiuliza kwanini ukope wakati mshahara haugusi na vitega uchumi vina generate cash
Well kila mtu ana maamuzi yake lakini anaeleta mawazo yake humu lazima apate comments za kila aina
 
Kitega uchumi cha kunipa mil 30 cash sina. Mimi similiki viwanda .hio hela ya mkupuo utaipata kirahis? Ungeuliza kitega uchum gan
 
Ulipaswa kuomba ushauri kabla hujachukua mkopo, sasa umeshachukua ndio unaomba ushauri, wa nini wakati ulishajipanga kitu cha kufahya?
Ningeomba ushaur humu wengne wangesem nichukue wengine wangesema no.. sasa nimeamua kuchukua na hayo ndio mahitaji yangu nimeomba ushaur utakaonipendeza nitaufata
 
Yard gani hiyo mkuu?
 
Mkuu hela ya mkopo iheshimu sana usije ukaweka rehani familia yako, Ohoo!
 
Wabongo vichwa vizito sana kuelewa,haya ndio madhara ya kula ugali hovyo hovyo
 
Kitu chako chochote kile ambacho kinakugharimu basi kitu hicho ni liability (dhima) na ambacho kinakuletea mkwanja basi hicho ni asset (mali).

Kama nyumba na gari lako zina kugharimu pesa, financially speaking tutaziita ni liabilities. Lakini kama una nyumba nyingine zina wapangaji na unakusanya kodi tutaziita nyumba hizi assets, hali kadhalika kama una magari mengine yanayokuletea kipato, magari hayo pia ni assets.

Chacharika ili uwe na assets (mali) nyingi kuliko liabilities (dhima). Hapo utakuwa umetoka kwa kiwango cha lami.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…