Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Pole sana mkuu, kama una documents za kusapoti nenda police but kwa mimi ningemuacha tuu Mungu ni lazima atamnyoosha huko aliko

Kumuachia Mungu jambo lililo ndani ya uwezo wako ni ujinga. Mungu aache kuangalia watu wanakufa na njaa Sudan huko aje kukutafutia wewe tapeli wako? Hapa ni kumsaka na kumuadabisha mwenyewe.
 
Alikuwa ni kijana wa gheto tu maana alifukuzwa kazi akashuka sana kiuchumi na hii project ndio ilimpa walau nafasi ya pili, anapokaa nilifika na vitu alivyoviacha thamani yake haizidi au haifiki milioni moja.
Kama haonekani inawezekana pia akawa amepatwa na matatizo. Hivyo toa taarifa polisi ukieleza yote.. yaweza pia ikawa amedhulumiwa na patner wenu wengine au kafanyiwa kitu kibaya hata kuuliwa. MUHIMU UTOE TAARIFA POLISI. Watafanya uchunguzi toka alipopewa hayo malipo kitu ambacho wewe huwezi kufanya. PESA INAUA HUJASIKIA WATU WANAUA KWA SABABU YA MIA TANO AU ELFU CHACHE TU?
 
Safari ya mafanikio Ni ngumu Sana.unachokipitia wewe Kuna watu wengi wamekipitia..kutapeliwa na kudhulumiwa pesa nyingi hata Mara kumi ya hiyo...inaumiza inavunja Sana moyo...kwanza kwa nature ya kazi yenu ilikuwa kuaminiana zaidi kuliko documentation( bank,contract, payments etc) hapo itakupa ugumu kupata Chako hata ukimpata anaweza asikupe labda tu mtishiane maisha..Hii ni fundisho kwa wote ,Mambo ya kuaminiana dunia ya leo yamepitwa na wakati..unapowekeza fedha calculate Ni kwa namna gani u will be safe if anything happen ..usimwonee mtu aibu atanionaje...if Ni banks hao waasia wapewe muongozo akanti za kulipa na kutoa pesa bank utaratibu ujulikane..Sasa wewe unamwachia mtu afanye kila kitu halafu akuletee pesa mezanj hapo tegemea maumivu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naongeza tena ni mjinga wa Karne ya 21 ya Sayansi na Technologia! Utasemaje ni rafiki yako mlieshibana ili hali huna taarifa muhimu juu yake! hujui anapoishi, amepanga au amejenga, ameoa, ana watoto, anaishi na wazazi, ndugu zake, mke wake au wazazi wake na mwisho ni mwenyeji wa wapi hapa Tanzania..
 
We acha ujinga, hao wabongo watakuwa wamemuua kisha wakamtupa huko porini, halafu wewe wanakuambia amekimbia, tumia akili wewe...
 
Pole sana, ila msamehe na usonge mbele ila usisahau Don't trust anybody linapokuja suala la pesa.Ubaya ubaya tu.
 
Yote kwa yote hakikisha jasho lako halipotei kaka kwa njia yoyote ile ….
 
Chata,

Ni miezi zaidi ya 7 sasa tangu jamaa akupige.

Tunaomba mrejesho!!!
 
Mrejesho Mfupi wadau;


Baada ya kumtafta sana jamaa bila mafanikio, mwaka jana mwezi wa 12 alinitafuta yeye mwenyewe whatsap kwa namba mpya akaniambia aliitumia ile pesa kwenda South Africa kutafuta maisha, akanitumia na picha zake akiwa huko South na akaniomba sana msamaha(kitu cha kijinga tu ofcoz) na aka ahidi akirudi bongo atanirudishia hela yangu nimuwie radhi sana.

Nilimwambia "mzee bado sijakusamehe na sitokusamehe, nataka hela yangu kabla ya mambo mengine yote".

So najua now ata yeye huko alikokwenda ni kama aliitupa tu hio hela instead angeitumia hapa hapa bongo labda kuna uwezekano ingezaa, maana ukipiga hesabu hapo siku za kwanza kwanza tu kwenda South ni wazi nusu ya hela iliishia kwenye nauli na accomodations na ushamba wa mji tu.

Tukio hili limenifanya nijiulize maswali mengi sana, moja ni; inakuaje kijana wa umri wa miaka 30 ana waza kwenda kwenye nchi ya kiafrica kutafuta maisha sehemu ambayo ni very dangerous na kuna vitisho vikubwa vya mauaji kwa raia weusi wa kigeni? au shetani kazi yake kukupa ramani, matamanio alaf ana kuseti ufe? So sad.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…