Nimefanikisha kutimiza ndoto za binti wangu wa kazi

Hongera zenu kwa Utu mlionao!
 
Hivi anawezaje kumsomesha mdada wa kazi huku mdogo wake yupo nyumbani? Vitu vingine vinajijibu automatically
 
Hivi anawezaje kumsomesha mdada wa kazi huku mdogo wake yupo nyumbani? Vitu vingine vinajijibu automatically
Mzee unajua maisha ya familia yangu na huyo mdogo wangu unaemzungumzia?

Ndugu yaani kumtaja mdogo wangu kwenye uzi wewe ushaconclude kwamba hana mishe zozote, Aiseee
 
Mkuu kwani huku kuna shida gani?
hahaha kwamba nimekosa baraka haha, wewe jamaa umenichekesha sana
 
Umeandika nilichotaka kuielezea...mie wangu alikua akiona ratiba unasoma maharage ananuna hatari....bas DStv ikate mnuno..unamkosesa matamthilia ! yake...khaa!
[emoji23][emoji23] kawa mama mwenye nyumba sasa, yaani haya maisha jamani unaweza kuta boss hana shida binti sasa [emoji24][emoji24][emoji24], unakuta binti safi boss sasa maisha hayako sawa kabisa!
 
Hakika ni kitu cha kujivunia sana. Mungu atakurudishia!
 
[emoji23][emoji23] kawa mama mwenye nyumba sasa, yaani haya maisha jamani unaweza kuta boss hana shida binti sasa [emoji24][emoji24][emoji24], unakuta binti safi boss sasa maisha hayako sawa kabisa!

Hahaha bas akabebeshwa mimba...nikamwambia maisha sio unavyofikiri wewe. Bas alidhan akizaa mtoto atamspoil as I do!..hhah kachakaa balaa yuko huko Musoma. Namuona huruma kaolewa na wababe. Full vipigo. Akampa jina mwanaye jina langu. So nnatakiwa kumsaidia mtoto yule walau aende shule!
 
Duu pole yake, halafu mabinti wasiku hizi wameranduka kweli hata ukimshauri anaona unamzibia, kuna mmoja alikuwa kwa ndugu yangu nikamshauri vizuri sana, na walikuwa mjini kabisa boss anamwamini kwakila kitu, safari na katoto ka boss ni ndege tu, baadaye kaona ni upuuzi nakuja sikia kaolewa na mbabe kipondo kwa sana maisha duni mtoto kaumwa hata pesa ya hosp shida mpaka mtoto kafia mgogoni mme yupo kwa kahaba
 
Yaani wanaharibu Sana maisha yao kwa tamaa za kijinga!
 
Yaani wanaharibu Sana maisha yao kwa tamaa za kijinga!
Sana nilimwambia kuna akili yakujiongeza kuna wengine Mungu aliwajalia akili ya kuzaliwa hakuna ushauri wa mtu unajiongeza mwenyewe na Mungu anakusaidia, sasa wewe unapata washauri wazuri watumie, lakini ndiyo hivyo
 
Na Mimi nashukuru Mungu msichana wangu wa kazi wa Kwanza nilihakikisha anatunza mshahara mpaka kununua cherehani yake halafu Mimi nikamlipia Ada ya mafunzo.....ingawa aliondoka Kwa jeuri lakini baadae alirudi kuomba msamaha. Sasa yupo kijijini amekuwa single mama na kazi ya ushonaji inamsaidia
Msichana wangu wa sasa naye ameshanunua cherehani yake na nimeshamtafutia shule ataanza next month.
Nashukuru Mungu
 
Hizi ndizo mada tunaziitaj humu..

Sio ujinga wa ngono kimasihara kla siku..

Mods hizi ndizo nyuzi za kuzipa kipaumbele..

Sio ujinga ujinga tu..
 
Ndugu umefanya jambo kubwa sana maishani mwako na huyo dada kadri atakavyowasaidia wengine basi ujue una fungu lako hapo lipo kwa Mungu...ulichokifanya hakina utofauti au naweza kusema ni zaka kwa upande wetu waislamu(wanoujua watanisahihisha).

M/Mungu akubariki wewe na familia yako na ukoo wenu
 
Hongera sana mkuu, huyo ndio uzalendo, na kuonyesha imani yako kwa Muumba wako. Tofauti na wale wapiga porojo wa mitume , wa kutoa sadaka, wa kuimba sabato,na ujinga mwingine wa kiitikadi za kidini ambazo haiongezi thamani kwa binadam mwenzake. Wale wenye itikadi Kali za dini na wao walete matendo yao anayozidi hili la kwako tuone. Mungu akubariki sana kiongozi
 

Wew ni #MshuaMaster

Hongera sana kwa Moyo huo..

Barikiwa sana
 
Hongera sana Kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…