Nimefanikisha kutimiza ndoto za binti wangu wa kazi

Vyema sana. Mimi huwa na ideas za kusomesha wasichana wa kazi lkn sharti atimize mwaka mmoja kwanza kazini ndipo nimsomeshe. Bahati mbaya wote niliokaa nao hawatimizi mwaka. Kiukweli hii ahadi huwa siwapi bali huwa moyoni mwangu tu.

Kwa maoni yangu kama unapata wasaa wa kumsomesha mtu au kumpa mtaji, Ni vyema kufanya hivyo kwakuwa unakuwa umempa chakula cha kudumu kuliko kuendelea kumfanya ni mfanyakazi wako maana hapo unamjengea utegemezi wa kudumu.

Mkuu umefanya wema na bila ya shaka utalipwa wema maradufu
Jifikirie una matatizo gani mpaka ukimbiwe na madada wa kazi?
 
Habari zenu nyote,

Ni takribani miaka 6 sasa tangu niwe na huyu msaidizi wa kazi za nyumbani, nilimchukua akiwa mdogo akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kumaliza elimu yake ya msingi.

Maisha ya nyumbani kwao yalikuwa ni duni sana, na wazazi wake walionekana kushukuru sana binti yao kupata hii kazi ambayo mshahara kwa huo mwaka tulikubaliana elfu 30.

Baada ya kukaa nae kwangu, ndugu niliokuwa nakaa nao akiwemo mke niligundua hali ambayo sio nzuri ya kumtumikisha kazi nyingi zinazomzidi umri wake na zingine zingewezwa kufanywa na wao.

Nilizungumza nao na nashukuru walinielewa na wakawa wanamchukulia Kama mdogo wao na hata utambulisho wake kwa wageni haukuwa tena mfanyakazi wa ndani bali mdogo wetu.

Nilimshurikisha mke wangu juu ya kumuendeleza huyu binti na tulipomuuliza nini anapenda kujifunza, alitujibu anahitaji kuwa mshonaji wa nguo.

Tulimtafutia chuo akasoma mwaka mmoja hapo baadae tukamhamishia VETA kwa ajili ya ujuzi zaidi wa mafunzo hayo kwa mwaka mwongine, Alipomaliza aliomba kuendelea na fani nyingine ya urembo na upambaji hapohapo VETA tukamlipia na alimaliza vema.

Baada ya kumaliza tulimnunulia vyerehani viwili kwa kutumia pesa yake ya mshahara tuliyokuwa tunamtunzia na kuongezea ilipopungua na kumlipia frem kwa miezi 6 pamoja na kumuwekea vitenge na vitambaa kidogo kwenye frem akaanza kushona huku akiwa anakaa kwangu kwa miezi miwili.

Baada ya kumchunguza na kuona akili yake imekomaa, tukampangishia chumba cha 30k kwa miezi 4 akahamia na vyombo kidogo.

Nafurahi kuona hadi sasa anaendelea vizuri hakosi 40elfu kwa siku, sasa amepata mchumba anataka kuolewa.

Hili ni Jambo la kujivunia kwangu kuona maisha yake yamebadilika.

Wema hulipwa kwa wema.
 
Hongera mkuu lakini nampa pongezi nyingi kwa mkeo ni mvumilivu na muelewa

ange kua mke wangu hakiamungu asinge weza kumruhusu kusoma kamwe angemuwekea vitimbi paka ashindwe Yule mama Ana roho mbaya sijapata kuona

kuna siku nilimnunua Dada wa kazi ndala mpya aka myanyanganya akmpa kuu, yani msichana akijitahidi sana anadumu miezi mitatu tu......yani Yule mwana mke nilisha mchoka sema tu ni mezaa nae sina jinsi

Polee Sanaa mkuu,Mana umeongea kwa uchungu kweli...huyu mtafutie mwenzake jeuri itapungua Kama sio kuishaa.

Embu funguka kidogo vigezo gani vilipelekea adi ukamchagua yeye Ili na sisi ambao bado kuoa tusije tukanasa Kwenye huo mtego.
 
Mahouse girls wengi ni wanawake wazuri sana hasa upande wa kuwaoa...wanajituma,wanatabia nzur ndani adi nje,wanajua kumuhudumia mme Kama mtoto vile japo wengi wanakuwa sio attractive (romantic) kutokana na matunzo yao but wakipata matunzo mazur wanavutia kwakweli adi mama mwenye nyumba anakuwa na wivu.

Ila hawa wadada wanapitia changamoto nyingi sana,kuna mdada nafahamiana nae kafanya hizo kazi takribani nyumba tatu na nyumba zote hzo kanusurka kubakwa na baba wenye nyumba....yani adi sasa yupo hopeless kabsa...nimempa nafasi ya kuwa mke wangu apo mbelen coz kakizi baadh vigezo vyangu,nimemwambia ajifikirie akiridhika tufate taratibu tufunge ndoa.
 
Safi sana mkuu
 
nakupongeza mkuu kwa Jambo hili. na Mimi umenifundisha Jambo nikipata nafasi nitafanya Kama wewe.

Asante Sana.

Kuna mashetani huwa yanawageuza watoto wa watu Kama watumwa, kazi kibao huku mshahara mdogo Sana mengine yanawabaka kabisa walaaniwe kwa kweli
 
Habari zenu nyote,

Ni takribani miaka 6 sasa tangu niwe na huyu msaidizi wa kazi za nyumbani, nilimchukua akiwa mdogo akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kumaliza elimu yake ya msingi.

Maisha ya nyumbani kwao yalikuwa ni duni sana, na wazazi wake walionekana kushukuru sana binti yao kupata hii kazi ambayo mshahara kwa huo mwaka tulikubaliana elfu 30.

Baada ya kukaa nae kwangu, ndugu niliokuwa nakaa nao akiwemo mke niligundua hali ambayo sio nzuri ya kumtumikisha kazi nyingi zinazomzidi umri wake na zingine zingewezwa kufanywa na wao.

Nilizungumza nao na nashukuru walinielewa na wakawa wanamchukulia Kama mdogo wao na hata utambulisho wake kwa wageni haukuwa tena mfanyakazi wa ndani bali mdogo wetu.

Nilimshurikisha mke wangu juu ya kumuendeleza huyu binti na tulipomuuliza nini anapenda kujifunza, alitujibu anahitaji kuwa mshonaji wa nguo.

Tulimtafutia chuo akasoma mwaka mmoja hapo baadae tukamhamishia VETA kwa ajili ya ujuzi zaidi wa mafunzo hayo kwa mwaka mwongine, Alipomaliza aliomba kuendelea na fani nyingine ya urembo na upambaji hapohapo VETA tukamlipia na alimaliza vema.

Baada ya kumaliza tulimnunulia vyerehani viwili kwa kutumia pesa yake ya mshahara tuliyokuwa tunamtunzia na kuongezea ilipopungua na kumlipia frem kwa miezi 6 pamoja na kumuwekea vitenge na vitambaa kidogo kwenye frem akaanza kushona huku akiwa anakaa kwangu kwa miezi miwili.

Baada ya kumchunguza na kuona akili yake imekomaa, tukampangishia chumba cha 30k kwa miezi 4 akahamia na vyombo kidogo.

Nafurahi kuona hadi sasa anaendelea vizuri hakosi 40elfu kwa siku, sasa amepata mchumba anataka kuolewa.

Hili ni Jambo la kujivunia kwangu kuona maisha yake yamebadilika.
Hongera sanaaa mkuu kwa moyo huo
 
Hongera mkuu lakini nampa pongezi nyingi kwa mkeo ni mvumilivu na muelewa

ange kua mke wangu hakiamungu asinge weza kumruhusu kusoma kamwe angemuwekea vitimbi paka ashindwe Yule mama Ana roho mbaya sijapata kuona

kuna siku nilimnunua Dada wa kazi ndala mpya aka myanyanganya akmpa kuu, yani msichana akijitahidi sana anadumu miezi mitatu tu......yani Yule mwana mke nilisha mchoka sema tu ni mezaa nae sina jinsi
Pole sana mkuu, wanawake sampuli hii ni wengi sana kwenye jamii yetu
 
Mimi mwenyewe beki3 mkuu! Kama itakupendeza naomba 300,000/ - nimnunulie mama kiwanja!
Ukishindwa naomba 30000/-
Hongera kwako pia.
Kama haya mawazo ni ya beki3 ina maana hata wewe bosi wako anakutunza vizuri na anastahili pongezi lol!!

..Wasaidizi wa ndani wanatumikishwa kitumwa kiasi kwamba hata wao wenyewe wanajidharau na kutokukua kiakili.
Wengi wao ni ndani tu muda wote, hawapewi nafasi ya kujua dunia inaendaje.
Hata kuangalia tv ni mpaka bosi wake aondoke na hapo wanaishia kuangalia bongo muvi na tamthilia nyinginezo.
Kwa asilimia kubwa Ubeki3 ni utumwa ndani ya jamii huru.
 
Back
Top Bottom