Kaka, hongera kwa kubahatika kushika hiyo Mil 15.
Mi naona now hauko tayari kufanya biashara that why umekuja huku kuuliza, kama ungekuwa tayari basi bila ushauri wowote ungejitupia ndani ya biashara.
Mawazo yangu, naomba chukua hiyo Hela iweke UTT, au Fixed acc Kwa kipindi Cha miezi 6 mpaka kumi na mbili then Ile faida ndogo itumie Kwa kufanya survey na kujiridhisha kuwa nikifanya biashara hii itanitoa. Mfano, ukaweka fixed ya let say asilimia 1 Kwa mwezi Kwa ulichoweka, hapo utapata 150,000/= tzs kila mwezi, chukua hiyo Laki na nusu, halafu itumie kufanya utafiti. Kwani kupoteza Laki na nusu Kwa tafiti ya uhakika ni Bora kuliko kupoteza 15M kwenye biashara.
Pili, option ya mwisho, chukua 15M yote inunulie mpunga kipindi Cha mavuno halafu Bei ikipanda uza, truste, lazima utoboe.
Ukihitaji sana nikushauri karibu kwenye comment hapo chini. - Deus Michael Ndololo.