Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

Pesa ya urithi haifanyiwi biashara Tafuta eneo ununue litakusaidia baadae
 
timu moja daily weka double chance weka million hukosi 250k mpaka 300k per day, ..ndo kitu nafanya siku hizi najifungia ni mwendo wa kumtafuna muhindi mpaka mtaani washaanza kuni-doubt nasukuma sembe aka ERIC MANDALA ,.... nasisitiza usivuke zaidi ya timu moja utakuja nilaum.
Weka screenshot tuone
 
Fungua Duka la Vifaa vya pkpk, usiwe na Tamaa ya kutaka Faida kubwa, pia Oil Tafuta Faida ndogo utapata wateja Wengi. Na wanaokuja kumwaga oil Buku iwe ya Fundi usichukie Wala kigawana hilo Buku na fundi utapata wateja Wengi sana
Kwa hiii biashara mwaka Jana bro wangu hime mfilisi kwa nilicho experience kwenye hiii biashara Kam hanataka kufanya basi 1/ntafuta fundi mnzuli
2/Eneo la biashara liwe Lina onekana hasa road
 
Aisee kama wewe ni dume uwe makini na hizo hela kuna mimalaya itakuwa imeshazinusa
 
Kaka, hongera kwa kubahatika kushika hiyo Mil 15.

Mi naona now hauko tayari kufanya biashara that why umekuja huku kuuliza, kama ungekuwa tayari basi bila ushauri wowote ungejitupia ndani ya biashara.

Mawazo yangu, naomba chukua hiyo Hela iweke UTT, au Fixed acc Kwa kipindi Cha miezi 6 mpaka kumi na mbili then Ile faida ndogo itumie Kwa kufanya survey na kujiridhisha kuwa nikifanya biashara hii itanitoa. Mfano, ukaweka fixed ya let say asilimia 1 Kwa mwezi Kwa ulichoweka, hapo utapata 150,000/= tzs kila mwezi, chukua hiyo Laki na nusu, halafu itumie kufanya utafiti. Kwani kupoteza Laki na nusu Kwa tafiti ya uhakika ni Bora kuliko kupoteza 15M kwenye biashara.

Pili, option ya mwisho, chukua 15M yote inunulie mpunga kipindi Cha mavuno halafu Bei ikipanda uza, truste, lazima utoboe.

Ukihitaji sana nikushauri karibu kwenye comment hapo chini. - Deus Michael Ndololo.
 
kama kweli ndio bunduki yako ya mwisho fanya biashara ambayo wewe mwenyewe ndio utakuwa msimamizi wa karibu kwanza
 
Una leseni, nunua gari yako fanya taxi mtandao, bolt, uber, taxify, farasi na wengineo
 
Mkuu hii ungefunguka zaidi, akishapata mkopo marejesho ataanza lini, coz kwa biashara mpya kuanza direct na mkopo, atakua kwenye pressure kubwa sana
Marejesho ni ile income yako ya UTT , wewe kazi yako itakuwa kupambana na biashara tu
 
Chukua 10m tupia hisa za CRDB 5m Hisa za Nicol utakuja kunishukuru baadae. Mda wa maamuzi ni sasa
 
Chai... Hiyo Kemebos ndiyo imefanyaa nigundue hiyo Chai..
 
Back
Top Bottom