Nimefika Tabora, nawaambia wanipeleke mjini wanasema ndio hapa tulipo!

Nimefika Tabora, nawaambia wanipeleke mjini wanasema ndio hapa tulipo!

Mkuu Bush,
Nisome taratibu na kunielewa.

Hapana sehemu nimesema kuhusu kutoboa nimesema zipo fursa.

Geita kuna vijana wanapata pesa nyingi sana lakini wanaotoboa ni wachache, wengi zikiishia kwenye katikati ya mapaja na pombe.

Nimezungumzia kutoka nje ya kariakoo, nilikuwa na mentality ya kariakoo ni kila kitu na Nina ofisi mpaka sasa, lakini nilipotoka nimejifunza kuna fursa nyingi sana.

Soma unielewe nimezungumzia fursa sio kutoboa, ndio maana Unaweza ukawa na rafiki yako mmeajiriwa Polisi mwaka mmoja, mna cheo sawa kwa maana mlipata fursa Lakini akakushinda maendeleo.

Mapambano yaendelee mkuu.
FuRsa za geita utaziona kwa macho ila kiuhalisia hazipo,mpaka umtoe kafara ndugu yako
 
Sikonge ni kawilaya kahivyo kupindikia, yaani wazee wa kule wakiamka asubuhi ni kukaa vibarazani na kucheza bao na wakitoka msikitini wanamalizia siku kwenye vijiwe vya kahawa.
Wajukuu zao wengi ni wavivu grade one, wanashinda kwenye pultebo na chakushangaza watoto wao wengi wa kiume walikimbilia mijini na wakike wamebakiza kuzaa na kuwaleta wajukuu zao walelewe kwa babu na bibi
I can't live there kwa kweli
 
Nini kiliupata huu mkoa? Nimewahi kufika Nzega na Igunga nikajua Tabora mjini patakuwa bora zaidi ya kule nimeshangaa.

Yaani mjini center nyumba ni za kizamani, hakuna kabisa modern buildings. Katikati ya mji nyumba zina mabati yameoza.
Watu wa Dar mmekariri kuwa mjini lazima pawe na maghorofa marefu.

Mnaugua ugonjwa unaitwa MAGHOROFAMAREFUMANIA.
 
Mpaka tunapata uhuru mji wa Tabora ulikuwa mji wa tatu yaani Dar, Tanga na Tabora. Tabora ni mji wa njiapanda kati ya Dar, Kigoma na Mwanza na ulikuwa na shule mbili maarufu yaani Tabora Girls na Tabora Boys, shule zilizoanzishwa na mkoloni kwa ajili ya watoto wa machifu, hata hivyo viongozi wengi walisoma hapo, pia kuna chuo cha Uhazili na chuo cha Reli.
Kwenye harakati za Uhuru Tabora ilikuwa ndiyo kitovu cha harakati za uhuru mikutano ikifanyika kwenye ukumbi wa kanisa Katoliki.
Kilichotokea baada ya uhuru ni kunyofolewa nishani zote ulizokuwa nazo na ukatelekezwa, hayo mambo ya siasa na mitazamo hasi ya kikabila, kumbukeni kesi ya chifu Fundikira wakati huo alikuwa Waziri, kesi
iliyowashitua wanyamwezi na ndiyo chanzo cha wanyamwezi kujaa Kigamboni kwani wakati wa kesi walikuja toka Tabora wakawa wanalala nje ya mahakama karibu na Dar Es Salaam Yatch Club wakati huo, walipoondolewa wakahamia Kigamboni ambapo ni karibu na mahakama.
Wanaoujua mji huo kabla na wakati wa uhuru ni mji uliokuwa na ustawi mkubwa, ulikuwa makao makuu ya Kamishna wa Jimbo la Magharibi.
Asante kwa historia hii
 
Uarabu + Uislam baba..... Mahali alipopita Muarabu, akaacha uislamu, sawa na mtu alopita akaachia "USHUZI".....
Huu ni uongo.
Mbona waarabu wenyewe hapa hapa Tz mko nao wana maendeleo kuwashinda??
Huko Kariakoo kote sehem kubwa pamehodhiwa na waarabu.
Katika maendeleo usiingize udini.
RUVUMA,RUKWA,SHINYANGA HAKUJAENDELEA NA IDADI KUBWA YA HAYO MAENEO NI WAKRISTU,JE HILO UNALIZUNGUMZIAJE??
 
Huko unakosema kuna fursa kuna watu kibao wako huko na hawajatoboa na hizo fursa.

Usione watu ukadhini ni wajinga.

Ukisikia Kilo ya Mahindi Tanga au Mbarali Mbeya ni Tsh 500 tu.

Ukienda Dar kilo ya Sembe ni Tsh 2000.

Unaweza kujiuliza kwanini watu wa huko hawafanyi viashara ya Mahindi kupeleka Dar?
Umeongea sahihi maisha sio marahisi kama wengi wanavyodhani
 
Nini kiliupata huu mkoa? Nimewahi kufika Nzega na Igunga nikajua Tabora mjini patakuwa bora zaidi ya kule nimeshangaa.

Yaani mjini center nyumba ni za kizamani, hakuna kabisa modern buildings. Katikati ya mji nyumba zina mabati yameoza.


Nimecheka kwa sauti ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†

Tanzania kwa ujumla bado sana maendeleo.

Umaskinini umekithiri mno, sio huko tu .
 
Back
Top Bottom