Nimefukuzwa kazi, nimetengwa na Ndugu, jamaa na marafiki!

Nimefukuzwa kazi, nimetengwa na Ndugu, jamaa na marafiki!

Unafanya kazi ndani ya shirika kubwa la kimataifa, unafukuzwa kazi kisha ndani ya siku chache unakiwa miserable kiuchumi na kijamii kiasi cha kutengwa na kukimbiwa na ndugu na jamaa??

Umuhimu wa kufanya kazi mashirika makubwa uko wapi???
 
January inazidi kuwa ngumuu, hapa naona umuhimu wa walioajiriwa kufungua biashara (kuwa na shughuli za ziada nje ya kazi) - hii ni kwa maandalizi ya matukio kama kufukuzwa kazi ama kujiandaa kustaafu
 
Hii story mbona kama vile Haina mashiko? Week moja TU yameshatokea yote hayo? Ndugu na marafiki wameshakutenga, kanisani wamekuondosha kwenye uongozi. Kama tukio limetokea week iliyopita, lini umeitwa kwenye disciplinary committee? Au tuseme ni kosa kubwa kiasi kwamba ilibidi uwe fired instantly, kwahio nani alitangaza? Anyway, najaribu kuunganisha muda vs matukio nakosa logical flow. Pole All will be well
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.

Kwa sababu ulishapata kazi na kufikia kwenye nafasi ya uongozi wewe una wasifu mzuri unaouzika. Chakarika kutafuta kazi nyingine, ikiwezekana kwenye sekta hiyohiyo uliyokuwemo.

Kabla ya kuwalaumu hao waliokutenga, jiulize je tabia yako ikoje? Bado una tabia za kibosi kana kwamba uko kwenye wadhifa wako wa ubosi, au umeshatambua kuwa sasa hivi huna hela na ubadilike uache ubosi?

Hakuna changamoto ngumu kama changamoto ya kupoteza pesa. Maana unakuwa ulishazoea maisha ya aina fulani, na maisha ya kunyenyekewa. Sasa hivi inatakiwa wewe ndo unyenyekee watu wenye pesa. Ukifanikiwa kurudi tena kwenye chati ndo utaendelea na tabia ya kupenda kunyenyekewa.

Kingine ni pata ushauri wa kisheria kuhusu mkataba wako wa ajira na jinsi ulivyofukuzwa kama ni sahihi. Kabla ya kufukuzwa kazi inatakiwa upewe nafasi ya kusikilizwa ili ujitetee. Je ulipata nafasi ya kujitetea? Kama hukupata, basi hapo kesi unashinda.
 
Yaani kazi ufukuzwe ndani ya wiki tu ndugu na jamaa wameshakutenga?? Sitaki kuamini hii.

Mimi pia nimeikataa hii chai, how comes mtu aliyefanya kazi kwenye shirika kubwa la kimataifa (tena akiwa team leader), eti afukuzwe kazi kisha ndani ya week moja tu atengwe na watu wake wote wa karibu. Kwamba amekuwa na maisha magumu ndani ya kipindi kifupi hivyo??

Najua ni kawaida kutengwa unaposhuka ila sio kwa haraka hivyo.😂
 
Hii story mbona kama vile Haina mashiko? Week moja TU yameshatokea yote hayo? Ndugu na marafiki wameshakutenga, kanisani wamekuondosha kwenye uongozi. Kama tukio limetokea week iliyopita, lini umeitwa kwenye disciplinary committee? Au tuseme ni kosa kubwa kiasi kwamba ilibidi uwe fired instantly, kwahio nani alitangaza? Anyway, najaribu kuunganisha muda vs matukio nakosa logical flow. Pole All will be well

Hii ni chai mkuu, ngoja nifate vitafunwa.
 
Mkuu , haukua hata na kiji-account kana million 100 hivi mkuu, et?
 
Mimi pia nimeikataa hii chai, how comes mtu aliyefanya kazi kwenye shirika kubwa la kimataifa (tena akiwa team leader), eti afukuzwe kazi kisha ndani ya week moja tu atengwe na watu wake wote wa karibu. Kwamba amekuwa na maisha magumu ndani ya kipindi kifupi hivyo??

Najua ni kawaida kutengwa unaposhuka ila sio kwa haraka hivyo.😂
Jamaa katuuzia chai leo. Anataka kuaminisha watu kwamba marafiki na ndugu ni watu wabaya. Amechemka leo
 
Man ndio ukubwa huo, umeshawahi ona kivuli gizani. Jibu hapana kivuli uonekana juani. Tafsiri yake ukiwa na pesa tegemea ndugu, marafiki na majamaa kuwa wengi hao ndio kivuli au nzi. Ukikosa pesa wote wanapotea hii ni nature ya mwanadamu. Hata wwe ukipata pesa utawasahau marafiki mliosota nao utatafuta marafiki wapya.
Maisha hayana formula we ishi jinsi yajavyo. Unaweza ukajibana Sana ukajinyima Sana ukaishia kuwa masikini na unaweza ukala Sana bata na ukaishia kuwa tajiri.
 
Yaani kazi ufukuzwe ndani ya wiki tu ndugu na jamaa wameshakutenga?? Sitaki kuamini hii.
chai hiii,, kwanza unapata wapi hata pozi lakuja JF kutangaza suala kama hili?
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.
Ndio changamoto za duniani hizo
 
Ukipata matatizo njia pekee Ili yasikuchanganye " cheka sana KISHA yapuuze usiyape uzito matatizo, iachie nature iamue, wewe ni wewe na matatizo ni matatizo Katu usiyaunganishe na wewe. Then ni rahisi kuyashinda.
 
Back
Top Bottom