Nimefukuzwa kazi, nimetengwa na Ndugu, jamaa na marafiki!

Kufukuzwa Kazi ndio mwanzo wa kuwa na maisha mengine, jikite kwenye mengine, ukikaa chini unasikitikia Kazi utapata magonjwa. Jiulize mbona wengi tu hawajariwa lakini Wana maisha wanaendesha, wanasomesha, nk.
Maisha ni akili sio vyeti, vyeti ni mfano wa daraja tu lakini hakumaanishi kama hakuna daraja huwezi vuka ng'ambo tumia mtumbwi, piga mbizi
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.
Id name na Avatar yako ina majibu ya Uzi wako.

Wewe ni Restless Hustler...Keep hustling..
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.
Pole sana mkuu.ndiyo maana ikawa rafiki wa kweli ni Yesu,wengine wote kuna kitu wanachokupendea.Hata hivyo kuna maisha baada ya kazi hiyo kuisha. utastrugle ila utazoea na kitapatikana kitu kingine cha kufanya.kwa sasa unahitaji utulivu wa ndani.na ondoa usumbufu kwa watu uliokuwa unawasaidia wakati unayo kazi.usianze kuwadai fadhira
 
Duh, natanguliza pole lakini mbona naona kama wewe ndio unajinyanyapaa mwenyewe?.

Ni mapema sana kuja na tathmini kama hii, jipe muda na jitahidi sana kuchukulia mambo kwa upande possitive.

Huenda ni upepo fulani unapita na mambo yatakuwa sawa...huenda yasirudi kama mwanzo kwa asilimia mia moja lakini bado itategemea utatoa mtazamo gani kwa mambo.
 
  • Wiki iliyopita imetokea changamoto kazini na ufafukuzwa, tena taasisi ya kimataifa; kuna walakini hapo - bila kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi na hatua nyinginezo za kisheria
  • Ulipofutwa tu kazi, na kanisani wakakuvua usingozi kama kwamba kazi ndio mdhamini wa uongozi.
  • Maisha ni fumbo, utaimarika tu. Mungu mkubwa
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.
Relax..
Mshukuru Mungu kwa yote, mwombe nafasi nyingine.
Kuna mlango wa baraka unakuja mbele yako mkubwa kuliko huko ulikokuwa.
Utapata kazi kubwa yenye masilahi makubwa zaidi ya ulipokuwa.
 
Nadhani umeshajua nani ni rafiki wa kweli,nani ndugu wa kweli na nani kwenye maisha yako utasafiri naye....wala usikwazike huu ndiyo muda muafaka.........ni njia tu inapitia,Mungu huwa hamuachi mja wake.....relax na baki imara kabisa
 
siku zote mrija ukishakata wote wanakimbia unaweza kupata mmoja atayekufariji kwenye kipindi hiki kigumu,nikwambie tu maisha haya yana changamoto wakati we huna kazi kuna mwenzio ana kila kitu ila afya imekuwa tatizo.
Hii ikupe nguvu ya kuinuka na kupambana upya.
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.
Nimejifunza kitu hapa asee bado sijaanza maisha nipo chuo Ila Mwenyezi Mungu akinisaidia nikatusua heeee hamna Cha ndugu,jamaa,marafiki wote piga chini Niko radhi nisaidie yatima au mtu ambae simjui kuliko kufanya hivyo paaaah asante kwa hii thread mkuu 🌴
 
Kazi Nilikuwa nafanyia kwenye moja ya taasisi kubwa za kimataifa. Wiki iliyopita kuna changamoto ilitokea ghafla Sasa kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa team leader nikafukuzwa kazini!

Taarifa zilienea kwa Kasi ya Moto wa msituni na Baada ya muda Mfupi nikatengwa na Ndugu jamaa na marafiki. Hawapokei simu na nikiwatembelea hawanionyeshi ushirikiano ule wa mwanzo.

Niliowapenda na kuwajali Sasa hawapo upande wangu. Nahisi nipo shimoni! Hata kanisani wameninyang'anya nafasi ya uongozi, wakampa Mwenye kazi. I am tired of this fucking life.
Wewe fanya hivi: tafuta kazi nyingine halafu watenge wote waliokutenga.
 
Mshukuru Mungu amekuonesha ulikuwa na watu wa aina gani waliokuzunguka. Piga moyo konde maisha uyashinde. Lakini pia kuna nyakati unapitishwa ili Mungu ajidhihirishe, na pia amini utasimama tena.
 
Back
Top Bottom