Nimefukuzwa na mwenyeji wangu naomba msaada wa hifadhi Dodoma

Nimefukuzwa na mwenyeji wangu naomba msaada wa hifadhi Dodoma

Mal
Mkuu

Endapo hautopata msaada wowote hadi muda huu basi fika kituo chochote cha polisi utapta msaada bana.

Ukiwaeleza issue yako wanaweza hata kushauriana na mwenyeji wako au namna ya kukupatia hifadhi kwa muda unaosubiri nauli.

Na kama unataka kurudi Dar kwa namna yeyote, polisi wanaweza kukuombea lift kwenye malori ya mizigo ukafika Dar hata kesho.
Malori yana vijumba vidogo vidogo vingi njiani balaa.
 
Pole kpnd Cha kumalza chuo kinakuaga kigumu sana me mwenyewe nlwai fukuzwa kijanja na shosti angu ...Iyo siku niliishia lala hospitali chumba Cha sindano🙂..Maisha ni safari jamani ...
Mi niliondoka kwa mdogo wangu wa damu kabisa,nilipotezaga kazi nikiwa mkoani nikapitia kipindi kigumu sana. Ndugu wakasema wanavyojiskia mi sikujali. Sasa ikawa nakuja Dar kufuatilia mafao yangu enzi hizo ndo wamepiga pini fao la kujitoa. Dogo alikua ndo kamaliza chuo kapata kazi. Basi Ikawa dogo hana stori namimi kabisa na hata asubuhi akisepa ni kimyakimya. Sikugundua hadi kama mara ya 3 hivi nimefikia kwake ndo hali ikawa waziwazi nikashindwa kuvumilia.

Jioni nilimtext tu kuwa nimeondoka nimeenda kwa jamaa yangu. Kuna mshkaji wangu alikua kajenga goba nyumba imeisha kabisa anakaa mlinzi na kulikua na chumba ambacho mshkaji alikuaga akija Dar anafikia,so nikapewa key nikaanza kaa hapo.

Kimsingi I loved the place na mazingira ya kule coz nilikua sijawahi fika pande zile kabla. Mwishowe nikapata nssf yangu namimi nikavuta kiwanja pande hizohizo kipindi kabla havijapanda, na nikaamua kuhamia mazima Dar, na nikapata mchongo mwingine hadi leo nakimbizana soon nahamia kwenye mjengo. Saizi wanashangaa nilipataje vile viwanja maana vilikua double afu bei za saizi ni nyoko
 
Unaondokaje nyumbani bila plan umesema ulikuwa na savings ulizifanyia nini ? Kinachonishangaza ni kuwa ulishindwa kupanga hata nyumba za elfu kumi na tano kwa mwezi ufanye michakato mingine au ulienda dodoma kutafuta white collar jobs .

Sasa unarudi dsm ili iweje ili hali nyumbani kwenu hali unaijua! Mpaka sasa hivi unabegi la nini sasa ? Uza hilo begi kisha tafuta kibegi cha mgogongoni weka nguo kadhaa na vyeti vyako ingia mtaani anza kujichanganya ukipata shavu hata kwenye ujenzi kuwa punda mdogo mdogo siku kampuni inaona unakitu cha ziada unaweza kupewa hata stoo ushike.

Wewe ni mwanaume usisahau hili .
 
Nimeshakaa na jamaa yangu miaka hiyo tulisoma chuo pamoja bahati ni kuwa nilikuwa na sehemu dsm .
Yule ndugu akaja kuanzia maisha kwangu alikaa anaenda kwenye mishe zake anarudi kulala wakati mwengine tunakula wote au kila mtu anakula anapopajua kwakuwa nilikuwa na mambo yangu na yeye yake sikuwahi kuhesabu siku ila uzuri jamaa alikuwa na mpango kazi .

Ninapoandika wakati huu jamaa ameshaweka makazi yake mjini hapa na anafamilia ndani .
Mwanaume hautakiwi kuwa legelege dunia haina haki huruma wala usawa pambana tena kama mzee wako hakupigania uhuru inabidi upambane zaidi.
 
Enhe Mungu naomba unipe nguvu za kuendelea kupambana, nina wadogo zangu bado hawajajitegemea.

Mkuu kila la heri, Sisi wengine tuko Dodoma ila hatuwezi kukuhifadhi, bora hata ungekua ke, unaeza mtungia baba chanja hata stori ya uongo na ukweli, ila me unasema nini?? Ni ngumu.
 
Kama ni mzima wa afya na siyo mlemavu, nakushauri acha kulialia kwanza Dodoma joto hata nje unaweza ukalala.
Unasema kuna joto!? Hupajui dom wewe, huku kuna jua kali, ikifika jioni baridi, usiku baridi kali na asubui mapema sana kijua hicho yaani hapajawai kutulia kbs!
 
Pole sana mkuu ndio maisha yalivyo hakuna anayejali watu tumekuwa wabinafsi sana japo na wema wapo ila wachache sana.

Ngoja nikupe tips mdogo wangu kama wewe ni mtafutaji ugenini basi jitahidi sana kwenye begi lako usikose koti kubwa na shuka la kimasai ni heri uwe hata na suruali mbili na t-shirt mbili siyo kukosa hivyo vitu na jitahidi begi lisiwe kubwa maana litakuwa linakupa kadhia kwenye movements zako.

Haina haja ya kuwa na simu kubwa utakuja kuwafaidisha vibaka kuwa simple mpaka kibaka ajiulize atakuibia nini?

Kwa vile hauna options za kupata pesa jitahidi kujichanganya maeneo yenye mkusanyiko na kubwa zaidi jiandae kisaikolojia kukabiliana na njaa, kejeli, matusi na dharau.
 
Mtumish kabisa serikalin alisema anakaa mwezi ili salary ile September ataondoka akapange matokeo sijui alihonga.. navumilia salary hii asipoondoka namtimua 😂😂😂
Kwa hiyo ndio umeamua kunitangaza huku? Siku zote tunapiga story unashindwa nini kuniambia kama umechoshwa na uwepo wangu hapo kwako?
 
Mkuu

Endapo hautopata msaada wowote hadi muda huu basi fika kituo chochote cha polisi utapta msaada bana.

Ukiwaeleza issue yako wanaweza hata kushauriana na mwenyeji wako au namna ya kukupatia hifadhi kwa muda unaosubiri nauli.

Na kama unataka kurudi Dar kwa namna yeyote, polisi wanaweza kukuombea lift kwenye malori ya mizigo ukafika Dar hata kesho.

Apa umemaliza nilikua nataka kushauri iviivi.
 
Sikia mzee kama bado haujarudi dar basi usirudi kabisa nyumbani hesabu maisha yanaanzia apo changamsha akili Mungu atakusaidia tafuta sehemu salama kahifadhi begi lako anza mchaka mchaka utatoboa tu niamini nnachokuambia tena utamzidi uyo mshkaji mbali sana,
 
Pole Sana kijana. Kifuatacho ni kutafuta nauli ya kurudi Dar. Kuhusu hifadhi ni ngumu sana kupata sehemu haswa kwa kipindi hiki kigumu tunachopitia na pia uaminifu umepungua sana katika jamii yetu. Alisema Marijani (Mungu amrehemu), Dunia ya sasa Imani imekwisha, penye watu kumi binadamu ni mmoja tu.
 
Pole jamaa, nakumbuka kuna kipindi natoka mkoani naenda Dar nimeshaa chonga na ndugu yangu vzr kabisa kwamba nitatua kwake.

Nakaribia kufika napiga simu haipokelewi, nikajua normal tu, hee nashuka naona simu haipokelewi.
Asnte Yesu nikikua vzr mfukoni ikabidi niingie lodge tu, nikapata akili kumbe binadamu sie dah.!

Hakunitafutaga mpaka leo japo kwenye masuala muhimu huwa tunakutana mfano misiba, harus lkn hakuwahi wala sikuwah muuliza ilikua
Nilimwachia mtu simu muda huo na hakuniambia kama nilipigiwa simu,na nilivyoona uko kimya nikajua ulihairisha safari.
 
Naona jamaa wako kakufukuza kijanja usikute hata mwanamke hatokaa nae katafuta njia ya kukutoa hapo geto
Kwenye maisha ogopa sana watu wasio na misimamo na ambao siyo wawazi. Huyu jamaa angeweza tuu kumwambia jamaa yake kwamba aisee nakupa mwezi mmoja utafute sehemu yako ya makazi kwa sababu sitoweza kuendelea kuishi na wewe kwa sababu hii au ile, au hata kumwambia kwa sababu zangu binafsi. Na kama anakauwezo angeweza hata kumtafutia nauli au pesa ya guest hata za hali ya chini kwa siku mbili tatu. Pia uzoefu wangu kwa watu wa aina hii ikitokea mko wote kazini ni wa hatari kwa sababu wanaweza wakapiga dili la hela kazini halafu wakakusingizia wewe ili pengine ufukuzwe kazi au ufungwe, kiufupi ni watu hatari sana.
 
Pole jamaa, nakumbuka kuna kipindi natoka mkoani naenda Dar nimeshaa chonga na ndugu yangu vzr kabisa kwamba nitatua kwake.

Nakaribia kufika napiga simu haipokelewi, nikajua normal tu, hee nashuka naona simu haipokelewi.
Asnte Yesu nikikua vzr mfukoni ikabidi niingie lodge tu, nikapata akili kumbe binadamu sie dah.!

Hakunitafutaga mpaka leo japo kwenye masuala muhimu huwa tunakutana mfano misiba, harus lkn hakuwahi wala sikuwah muuliza ilikuaje.
Babu yangu aliniasa kwamba hata siku moja usiende ugenini bila kuwa na akiba yako ya kukulinda pale utakapopatwa na changamoto ugenini.
 
Niliwahi karibisha jamaa yangu akae siku tatu tukiwa chuo akakaa miezi mitatu na point. Sikuwa na mambo mengi na tuliendana vitu vingi basi alikaa mpaka alipoamua kuondoka. Inaleta changamoto ukikaa na mtu mko tofauti sana na bado unapenda uhuru wako
Hii situation ilinikuta. Rafiki yake na rafiki yangu alikuja town kuanza maisha.
Rafiki yangu akasema yeye huwa dem wake anakuja kulala hapo so ni bora afikie kwangu. Basi nikajua atakaa wiki.
Ebwana eeh. Alihamia jumla jumla kama miezi minne hivi akapata kazi mkoani...
Kwa kweli alisababisha usumbufu kwa kuwa 'ndege zilikuwa zinashindwa kutua'.
 
Hii situation ilinikuta. Rafiki yake na rafiki yangu alikuja town kuanza maisha.
Rafiki yangu akasema yeye huwa dem wake anakuja kulala hapo so ni bora afikie kwangu. Basi nikajua atakaa wiki.
Ebwana eeh. Alihamia jumla jumla kama miezi minne hivi akapata kazi mkoani...
Kwa kweli alisababisha usumbufu kwa kuwa 'ndege zilikuwa zinashindwa kutua'.
Mimi huyu alikuwa mwanachuo na tumesoma shule moja hivyo namjua fika. Alikuwa flexible anaweza toka siku moja ukimwambia so hatukuishi kwa shida
 
Naona jamaa wako kakufukuza kijanja usikute hata mwanamke hatokaa nae katafuta njia ya kukutoa hapo geto
naye katumia njia ndefu dawa ya watafta makaz kama hawa unamchana utakaa mwezi ukiisha unasepa bas maana vijana wanajisahau ukiruhusu siku moja ndo bas tena
 
Back
Top Bottom