Nimefukuzwa na mwenyeji wangu naomba msaada wa hifadhi Dodoma

Nimefukuzwa na mwenyeji wangu naomba msaada wa hifadhi Dodoma

2016..nimetoka home nimekuja kukaa na mchizi wangu
Getto kwao walikuwa na nyumba mbili
Yeye na getto lake kwao safi kidogo na sisi
Safi kidogo tumejuana ukubwani

Basi nikazoeleka hadi kwao ikawa ni kama kwetu
Kwa tabia nilizo kuwa nazo ikawa hata km sipo nimetoka wataniwekea chakula tu
Na nitaulizwa ulikuwa wapi? Mbn ujaaga
Basi nitakula nitarudi getto
Tumeishi hvyo hadi miaka 2 baadae huyo jamaa yangu alikuwa hawez kula hadi mm niwepo na mm ni km yy hata nikipata mchongo wwte lazma nimpe ela kidogo
Tukawa km ndugu nikaja kuajiriwa hadi sasa
Nina familia ya mtoto 1, sijaacha kwenda
Na wananipenda hadi leo hii,kila nikipita kawe mitaa ya maringo karibu na uwanja wa Tanganyika packers lzm nishuke kwenye gari nikasalimie nimekuta famikia imeongezeka kuna wajukuu wengi pale bs lazma nizame mfukoni niwanunulie japo
Juice juice au ice cream wale wajukuu
Kudumisha love na kulipa fadhila kidogo
Hakika mungu ni mwingi rehema.
 
Pole sana akufukuzae hakuambii toka, jaribu kufuata ushauri uliopewa wa kwenda kituo cha Polisi/Kanisani/Msikitini huko lazima utapata msaada, Mungu akusaidie.
 
Nyie mnalazimisha sana.mtu unaambia kisomi....sasa hivi ratiba zangu zipo tight sana. Unajibu ...nikija wala sitokusumbua sikai sana week 2 tu nashughulikia mambo yangu naondoka. Sasa kwa kuwa sisi hatupendi kupoteza muda tunakubali then....mnayaona.
Mpo wachoyo
 
Very true.
 
Mpo wachoyo
Si suala la uchoyo mjini si sawa na huko mikoani. Maisha yamechange sana hata imani hakuna kwa sasa. Sisi wenyewe mjini unakuta mwaka hamwonani na mpo hapa hapa Dar Mwenge na Sinza tu hapo. Mkiwasiliana kwa simu inatosha. Wewe unataka uje then nianze kukutembeza viwanja. .

Mimi huo muda sina. Kama ni demu unakuja tunapatq night moja au mqsaa kqdhaa tunabadilishana jasho. Then tunapeana muda wa kupumzika. Ndo maisha yalivyo si kugandana kama kupe.
 
Habari za wakati huu Wana JF.

Kwa majina naitwa David Mathias. Nilikuja Dodoma kutafuta maisha kutokea jijini Dar na nikafikia kwa rafiki yangu niliesoma nae chuo kimoja ambaye anaishi Nkuhungu. Rafiki yangu ameleta mwanamke ghafla na kuniambia kuwa anataka aishi nae kwahiyo mimi niondoke.

Hapa nipo barabarani tu begi langu sina pa kwenda na mimi huku mgeni. Naomba kwa mwenyeji yeyote wa Dodoma atakayeguswa kunisaidia hifadhi kwa siku kadhaa nikitafuta nauli ya kurudi nyumbani. Naomba sana na natanguliza shukurani.
Ume join JF jana tu ila upo kama unafahamu
 
Kukaa kwa Mtu ni kazi ngumu sana
 
Unaendeleaje kukaa kwa mwanaume mwenzio
Ukiwa na lengo la kutafuta maisha from scratch we fikia stend au sokon
 
Vijana tambueni maisha ya chuo uliyoishi na mwenzio siyo maisha ambayo wote mnaenda kuishi baada ya chuo hilo mjue kuna watu wanabadilika kutokana na mazingira sasa kama wewe ubadiliki matokeo yake ndio haya

Mpo chuo life style yenu ni kusoma na bata mbebana gheto mpo wanne au watatu hayo ni maisha ya kupitia tu kuna mwingine anaishi hivyo akijua haya ni maisha ya mpito do mkiachana hapo kila mtu anaenda kuishi maisha yake ngoja nitoe kisha kimoja

Kuna jamaa tulisoma naye chuo maisha yalikuwa yakisela sana tena sana mlala gheto hili kesho kule mmeamkia club nk kwakua chuo basi shule ikaisha kila mtu akarudi kwao ikabadi mawasiliano ya sm tu kumbe moja wetu yeye aliendelea na maisha yake ya kisela hakutaka badilika watu wana familia tayali nk yeye bado usela haujamwisha

Akawa anakupigia sm oya nakuja uko unasema pouwa karibu siunajua ni jamaa pengine ana issue yake unampokea anakuja kwako anakuta una familia unampa chumba nalala shemeji yake anamkarimu vizuri unashangaa mwamba anaanza kutoa na ratiba ya msosi shem pika hiki leo kwakua mgeni unaona pouwa aisee mwamba wiki yupo

Wife anaanza kuuliza uyo hana kazi au kaijia nini unasema ngoja taongea na jamaa unatafuta mda ana muuliza mzee vipi unasikia nimekuja refresh mind hapo ndio unachoka yani baba jitu zima halina muelekeo unapigia sm jamaa wanakwambia uyo ndio mikato yake hapo hata nauli utaombwa alikuwa kwangu uku amekaa mwezi mzima nikamtimua sasa ona mtu wa hivi unamfanyaje kama si mtimua

[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

ila watu wanachosha sana aisee.
 
lakini maisha magumu sana jamani.

yaani unawezakataliwa na ndugu zako wa damu,sembuse mshikaji tu wa kukutana juu kwa juu!!!

muhimu tujifunze kuwa na exit plan kabla hatujachokwa,yaani kwa mtu ukikaa sana siku 2,tena kwa dharula kweli kweli maana hata uhuru na aman unakosa.
 
mama D, mpe kijana wako hifadhi. Natambua fika unafahamiana na watu wazito wazito wengi tu wa ccm pale Dodoma!

Kijana anahitaji kukaa siku kadhaa kwa mwenyeji wake mpya, kabla ya kutafuta nauli ya kurudi alikotokea. Si unaukumbuka ule mfano wetu wa Msamaria mwema kwenye Biblia? Tumia hii fursa ili uweze kupenya kwenye tundu la sindano.
Kwanza huyo kijana ajibu amekaa kwa mwenyeji wake muda gani hadi kafukuzwa?
Huenda ukamchukua anasema atakaa siku kadhaa akahamia hadi umfukuze Tena.
 
Habari za wakati huu Wana JF.

Kwa majina naitwa David Mathias. Nilikuja Dodoma kutafuta maisha kutokea jijini Dar na nikafikia kwa rafiki yangu niliesoma nae chuo kimoja ambaye anaishi Nkuhungu. Rafiki yangu ameleta mwanamke ghafla na kuniambia kuwa anataka aishi nae kwahiyo mimi niondoke.

Hapa nipo barabarani tu begi langu sina pa kwenda na mimi huku mgeni. Naomba kwa mwenyeji yeyote wa Dodoma atakayeguswa kunisaidia hifadhi kwa siku kadhaa nikitafuta nauli ya kurudi nyumbani. Naomba sana na natanguliza shukurani.

Ilikuwaje ukatoka Dar ukaenda Jehanamu kutafuta maisha?
 
mama D, mpe kijana wako hifadhi. Natambua fika unafahamiana na watu wazito wazito wengi tu wa ccm pale Dodoma!

Kijana anahitaji kukaa siku kadhaa kwa mwenyeji wake mpya, kabla ya kutafuta nauli ya kurudi alikotokea. Si unaukumbuka ule mfano wetu wa Msamaria mwema kwenye Biblia? Tumia hii fursa ili uweze kupenya kwenye tundu la sindano.

Huyu ni mfano wa mwana mpotevu. Mwache a post hapa hela ya bundle ikiisha atauza hiyo simu apate nauli ya kurudi nyumbani kwao

Sasahivi bado ana nguvu 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom