hivi unawajua wenye tabia za uparasite? scenario zipo nyingi sana, mimi haitotokea kuishi na mtu ghetto moja, hata kushare sitting room na mwanaume siwezi, watu ni wabaya, nshamkaribisha mtu baada ya a level tunapiga tempo za kufundisha, napata mshahara napendeza san, mwana tuko nae job, sasa nikawa mzuri wa kulenga nguo pale dox, makunguru, i was good, sasa msela badala ya kuuliza tu kumbe wivu umemjaa kinoma, mimi nisijue, kumbe moyoni anaushindani. kama best nikamkaribisha nyumbani, ile tumelala usiku jamaa nikastukia kaamka anatoa viatu, raba zangu uvunguni anakagua na kushangaa, Mungu alinipa subra, ila baadae kumekucha nikamwambia nimeona kila kitu ulichofanya, dhamira yako nini, mimi nina roho nzuri unachotaka nikuuzie sema tu mi ntatafuta kingine usiwe na shaka. damn kuna watu akiwa mchawi hawasaidiki kamwe. si kila mtu ni mbaya ila wabaya husogelea wenye nacho ili wafanye yao.