Today...Hata akiwa mimi ndiye adm na ukaleta upotoshaji nakupiga block.
Kuna wakati mnapandikiza uongo ili uwe kweli sababu mnaweza kuunda kutokana na kusikia kutoka kwa waliokuwepo na ambao hata wao kuna mengine wana_adjust au updates to new version of history.
Mada zako hizo ni kwa Mwl. Nyerere tu au hata issues nyingine za mapinduzi ya zanzibar unawaandikia huko groupuni?.
Mzee Mohamed,Joa...
Nini maana ya kwiva?
Historia hii ni historia ya babu na baba zangu.
Sikusomeshwa kwenye shule au chuo chochote kile.
Ninayoeleza hapa ndivyo nilivyopokea kutoka kwao.
Joa...Mzee Mohamed,
Kwiva ni kivumishi Cha neno kuiva/iva/wiva/kwiva
Je wewe ni mjukuu/mtoto kutoka ukoo upi haswa kati ya mbili unazozielezea,Je ni wa Nyerere au ni wa Sykes?
Hakika historia imekaa mahali pake kabisa ndio maana imenyooka.... Hongera Kwa babu kuwa mmoja wa waasisi wa kupigania uhuru wa nchi yetuJoa...
Mimi ni mjukuu wa Salum Abdallah.
Babu yangu ni mmoja wa waasisi TANU Western Province 1954 na muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) 1955 Kasanga Tumbo akiwa katibu.
Chini ya uongozi wao waliunganisha TRAU na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hapa ndipo ulipokuwa uhusiano wa Babu yangu na Julius Nyerere.
Alikuwa mtumishi wa Tanganyika Railways akifanyakazi ya kufua chuma Loco Shed Dar es Salaam katika miaka ya 1920 Kleist Sykes akiwa Accounts Clerk.
Kleist na babu yangu walikuwa majirani nyumba zao zikitazamana Mtaa wa Kipata na New Street na watoto wao walisoma Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School ambayo walijenga babu zetu kama juhudi za kukwepa watoto wao kusoma shule za wamishionari.
Babu yangu alihamishwa kwenda Tabora mwaka wa 1947 Loco Shed ilipoondolewa Dar es Salaam na kupelekwa Tabora.
Salum Abdallah aliongoza mgomo wa Railway wa mwaka 1947, 1949 na wa 1960 uliodumu siku 82.
Mwaka wa 1964 babu yangu alikamatwa pamoja na viongozi wengine wa wafanyakazi na kuwekwa kizuizini Jela ya Uyui Tabora.
Huu ukawa ndiyo mwisho wa maisha yake ya siasa.
Alifariki mwaka wa 1974 na alipata mazishi makubwa na TANU ilisoma rambirambi wakimsifia kwa mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwa hali na mali
Unalijuwa group lipi?Sawa samahani kwa Hilo
Ila kuleta huku unalikosea group
DPW na msikiti vinahusika nini na hii mada?Mzee wangu tusaidie basi waboreshe mkataba wa DPW au utafukuzwa na msikitini kabisa.
Maana mashekhe wameuelewa mkataba haraka kuliko wanasheria
Wanakutimua sio kwa kumsema vibaya nyerere bali kwa kuendekeza udini. Wasilisha jumbe zako bila udini mzee watakusikilizaNikajiambia mwanzo hapa nimetimuliwa kwa makala niandikazo na moja ya sababu nilielezwa sielezi vizuri historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Umeiona video clip au umekurupuka tu?Wanakutimua sio kwa kumsema vibaya nyerere bali kwa kuendekeza udini. Wasilisha jumbe zako bila udini mzee watakusikiliza
Huwezi kufananisha dini na mjivuni mmoja. Ni ujinga huo.Kuna watu historia ya Nyerere wanavyoielewa kuwaambia mambo mengine ni sawa na wewe kuambiwa hiyo Dini Yako ni feki kamwe huwezi kukubali.
Taratibu wataelewa Mzee wangu. Kama Kuna haja tuanzishe group letu huko unashusha mizigo unavyoweza.
Niqu...Wanakutimua sio kwa kumsema vibaya nyerere bali kwa kuendekeza udini. Wasilisha jumbe zako bila udini mzee watakusikiliza
Wapo sahihi kukuondoa. When in Rome, do as the Romans do.NIMEFUKUZWA TENA
Inaelekea historia ya Mwalimu Nyerere itakiwayo ni ile ya zamani yuko peke yake wasitajwe wenzake
Kwa neno "mdini" unamaanisha Muislam? Au sivyo?Ndugu yangu usijidanganye, hukubaliki hata na mtoto mdogo. Kwa vile wewe ni mdini
Tazama unavyobweka, kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.Kumbe maaskofu wote ni zero kichwani?
Walikurupuka bila kuusoma mkataba?
Masheikh ndio waliuelewa zaidi?
Nyie watu dini imeharibu.
Tunajua fika mnachokitetea nyuma ya mlango wa DPW.
Katika hili tutaambiana bila woga.
Tutawanyooshea kidole bila woga.
Tutawakemea tena na tena.
Nasemaje?
Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.
Zaburi 116:6
Hakuna sheikh ameelewa nkataba, akili zenyewe za kuelewa ziko wapi?Tazama unavyobweka, kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.
Umeulizwa swali jepesi sana, tulizana ulijibu:
"Unadhani Maaskofu wameelewa?"
Mandonga alipoulizwa kwanini anaitwa "Mandonga"? Alijibu "ndonga hata upepo wake ukikupitia unalewa".
Missile,Unatolewa kwenye makundi pengine kwa sababu stori yako ni moja tu ya Sykes
Huchangii mada nyingine, wewe ukiamka ni Sykes, ukishinda ni Sykes, Ukilala ni Sykes. Kiufupi pengine unateka makundi kwa mjadala mmoja.
Hebu jirekebishe uanze kuchangia mada nyingine za kijamii n.k
Unawachosha watu na mjadala "mono"