Nimefukuzwa tena kundini

Nimefukuzwa tena kundini

NIMEFUKUZWA TENA

BAADA ya kuweka video hii ya TBC nikatolewa kundini:


View: https://youtu.be/-bwoz3jI7RA?si=rJdx_0PlMIHxm4Wm

Nilikuwa kwenye group moja nikafukuzwa naamini wengi mlisoma makala ile.

Bahati nikawa nimebakia katika group kwa no. yangu nyingine ambayo siitumii sana na kwa sababu hiyo ikawa sijui kama bado niko kundini.

Nikajiambia mwanzo hapa nimetimuliwa kwa makala niandikazo na moja ya sababu nilielezwa sielezi vizuri historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Nikaamua kuanzia sasa hapa kundini nitaweka vipindi nilivyofanya na TBC, AZAM na stesheni nyingine na vikarushwa kwa wananchi wote wa Tanzania.

Niliamini kwa kufanya hivyo nitakuwa nimewadhihirishia viongozi wa group kuwa Mohamed Said anakubalika hadi na vyombo vikubwa ikiwemo TBC.

Nikaweka video kama tatu hivi nazungumza historia ya Baba wa Taifa.
Haikunisaidia kitu.

Nadhani nimedumu kundini kwa siku kama tatu hivi leo wamenifukuza.
Inaelekea historia ya Mwalimu Nyerere itakiwayo ni ile ya zamani yuko peke yake wasitajwe wenzake

Ndugu yangu usijidanganye, hukubaliki hata na mtoto mdogo. Kwa vile wewe ni mdini
 
😆😆😆
Stow...
Tazama hiyo video hapo juu utanielewa zaidi.
Mzee Mohamed Said
Ikiwa mwandiko wangu umeonyesha hata dalili au viashiria vya kukutisha, ninaomba RADHI SANA KWAKO.

Nia yangu sio kukutisha au kukulazimisha.

Nia yangu nilitaka kujua UTHABITI WA MAHAKAMA YAKO YA NDANI katika kutoa hukumu na haki.

Mwenye mahakama huru ndani yake hajui kupendelea kwa mrengo wake au kwa maslahi yake bali huhukumu sawa na kweli ilivyo.

Nitafurahi nikipata maoni yako huru kuhusu bandari.
Naheshimu mawazo yako

Asante sana
Mungu akubariki sana
Glenn
Glenn,
Nadhani msg hii hujanikisudia mimi.
Mie na wewe hakuna mahali tumekwaruzana.

Hebu itazame upya
 
Mzee Mohamed Said
Ikiwa mwandiko wangu umeonyesha hata dalili au viashiria vya kukutisha, ninaomba RADHI SANA KWAKO.

Nia yangu sio kukutisha au kukulazimisha.

Nia yangu nilitaka kujua UTHABITI WA MAHAKAMA YAKO YA NDANI katika kutoa hukumu na haki.

Mwenye mahakama huru ndani yake hajui kupendelea kwa mrengo wake au kwa maslahi yake bali huhukumu sawa na kweli ilivyo.

Nitafurahi nikipata maoni yako huru kuhusu bandari.
Naheshimu mawazo yako

Asante sana
Mungu akubariki sana
Glenn
Glenn,
Sina la kusema kuhusu bandari.
 
Ndugu yangu usijidanganye, hukubaliki hata na mtoto mdogo. Kwa vile wewe ni mdini
Kote...
Mtoto mdogo hana uwezo wa kusoma kitabu kinachosomwa Chuo Kikuu.

Kujidanganya mwenyewe ni jambo lisilowezekana kwani nafsi inatambua kila kitu.

Ningekuwa mdini nisingepewa kazi na Harvard na Oxford University Press New York kuwa mmoja wa waandishi 500 kutoka kila pembe ya dunia kuandika Dictionary of African Biography (2011).

Katika kamusi hili lenye volume sita nimeandika historia ya Kleist Sykes (1894 - 1949).

Ningekuwa mdini nisingealikwa kuzungumza kwenye vyombo mashuhuri vya habari ulimwenguni: BBC, DW, SABC, VoA, Radio Iran kwa kuvitaja vichache.

Ningekuwa mdini Oxford University Press, Nairobi wasingenitia katika mradi wa kuandika vitabu vya historia ya Afrika na wakachapa vitabu vyangu.

Nadhani utakuwa umenifahamu.
 
1. Msikiti una uhusiano sana na DPW, kuna fununu kuwa watajenga msikiti mkubwa sana Mbeya, hii imekaaje?

2. Ni ajabu sana karibu waislam wote wameuelewa mkataba wa bandari kuliko wanasheria...hii imekaaje? (PAMOJA NA ELIMU YA MASHEIKH NI TIA MAJI TIA MAJI LKN MKATABA WAMEUELEWA KWA HARAKA SANAA)

3. Masheikhe wengi wametoa matamshi tata ya kuwakemea na kuwakejeli TEC waliochagua kulinda maslahi ya nchi...hii nayo imekaaje?

Kuna HARUFU YA UDINI ULIOJIFICHA CHINI YA DPW.

Nikwambie tu, moto huwezi kufunikwa na kipande cha khanga mzee Mohamed, tusubiri, tuombe uzima
 
Syllog...
Ukimwacha Abdul Sykes utafikaje kwa Dr. Kwegyir Aggrey aliyemtia hima baba yake Abdul Mzee Kleist kuunda African Association 1924?

Utamwingizaje Julius Nyerere katika TAA Dar-es-Salaam 1953?
Utapataje kadi tatu za mwanzo za TANU?

TANU Card No. 3 Abdul Sykes, No. 2 Ally Sykes na No. 1 Territorial President Julius Nyerere.
Utafikaje katika mitaa hii?
Mzee umekwiva.... I like watu wanaojua historia...kongole
 
Atafukuzwa na huku huyo maana ana mahaba mazito na hao kina Abdul Sykes.
Babu...
Hakika nina mapenzi makubwa na historia ya ukoo wa Sykes hili umesema kweli.

Hapa JF sijafukuzwa bali nimechaguliwa mwandishi bora Jukwaa la Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Nilipokuwa mdogo nikimsikia baba yangu akihadithia safari ya Sykes Mbuwane kutoka Afrika Kusini hadi Germany Ostafrika, maisha yake ya udogoni na Abdul, Ally na Abbas shule yao ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School nk.

Katika miaka ya mwanzoni 1960s Ally Sykes alikuwa na kipindi cha radio TBC akitangaza radio za Philips.

Baba alikuwa hakikosi kipindi hiki nami niko pembeni yake tunasikiliza pamoja.

Kuna kitu kikanivutia katika kipindi hiki nacho ni miziki ambayo Ally Sykes alikuwa anapiga.

Miziki mingi aliyokuwa akipiga ilikuwa kutoka Ulaya na Marekani mfano wa waimbaji kama Alma Cogan, wanamuziki wa jazz kama Louis Armstrong nk.

Baadhi ya santuri hizi zilikuwapo nyumbani kwetu na mimi nikizipiga katika radiogram ya baba pale nyumbani.

Baba akawa ananieleza kuwa wao katika ujana wao miaka ya mwishoni 1940s kuendea 1950s pamoja na Sykes brothers walikuwa na bendi ya muziki ''The Skylarks," na wakipiga miziki hiyo.

Stori hizi zikinivutia sana baba akinieleza stori za James Msikinya akipiga saxaphone kijana kutoka Afrika Kusini aliyekuwa katika bendi hiyo, Said Kastiko, Mzee Matesa katika drums Abdul Sykes akipiga clarinet, Ally Saxaphone, Abbas guitar nk. nk.

Ukiona picha zao na suti walizovaa utafurahi.

Mimi niliathirika sana.

Baba akielewana sana na Ally Sykes na akanihadithia msukosuko aliotiwa yeye siku Ally alipotoroka nyumbani kwenda kujiunga na KAR kwani Ally alipokuwa hajarudi nyumbani hadi usiku mkubwa Mzee Kleist akaekezwa kuwa mchana Ally alionekana na baba yangu wanazurura mitaani.

Hii ilikuwa mwaka wa 1942 na ulimwengu ulikuwa katika Vita Vya Pili Vya Dunia.

Wote wazee wangu hawa walikuwa wanasoma Kitchwele Boys Government School.

Stori hizi zikinivutia sana na zikawa sehemu ya maisha yangu.

Allah ana mengi ya kustaajabisha.

Historia ya Julius Nyerere na historia ya TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika nikaja kuisikia kutoka kinywa cha Ally Sykes sasa mimi mtu nzima na akili zangu timamu.

Historia hii ilikuwa kinyume kabisa na historia ya uhuru kama ilivyokuwa ikifahamika.

Ally Sykes akanifungulia hazina ya nyaraka zenye historia hii ambayo kila siku tunaijadili hapa.

Hebu jiweke wewe kwenye nafasi yangu.
Jiulize ungefanya nini?

Ungezikalia hizi nyaraka au ungeandika kitabu?

Mimi nikaandika kitabu.

Sihitaji kukueleza hiki kitabu kimefanya nini katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Haya mapenzi na historia ya Sykes yakawagusa Prof. Akyeampong na Pro. Gates wa Harvard wakaniomba niandike historia ya Kleist Sykes.

Unaweza ukaisoma katika Dictionary of African Biography, Oxford University Press, New York (2011).

Huu ndiyo mwaka Abdul na Ally Sykes wakatunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru na Rais Kikwete katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom