Na hawa woote wanao sema eti wamefurahi Mondi kuikosa Tuzo wasiyoisotea wala kuijua!! waongo hao Msiwaamini!! Dunia imejaa Mawakala wa Kuzimu ni usipime siyo binadamu halisi/wa kawaida ni maajenti wa shetani,
one day nitawaonyesha njia rahisi sana jinsi ya kuwatambua mawakala wa kuzimu kirahisi! na hii ni popote hata barabarani, Ndani ya daladala hata wakitembea wakiongea hata humu ndani wana JF msidhani mko watu halisi tupu, la hasha!!
kuna mawakala kibao wa shetani mnajibishana nao lkn hamwajui nawambia hivo sababu niliwahi fanya haya!! kabla sijajirudi.
wanaiwakilisha kuzimu mchana kweupee sasa wanachokifanya ni wanatujaribu km kweli sisi wa karibu yake tuna ufahamu wa kutosha kwa kile kilicho tokea pale siku ile kwenye utoaji tuzo?? kusema kweli....
Lengo la ile tuzo ni Diamond aipate kiu kweli kabisaa, yaani aitwae kabisaaa! ili kwa kufanye vile akae nayo immalize kimuziki kwa njia za kichawi!! kuumbe hawakujua padoogo sana,
Diamond yeye anatabia ya kumtanguliza Mungu wa kweli, kabla ya kila onyesho, ndiyo maana ile Tuzo ile ikapita hivi kushoto!! bila maneno wala ugomvi wala ulalamishi na yeye kapiga kimya!!
Wabaya wake wangejua mapema kuwa yule bwana ni mtu wa Maombi ya mfungo sana!! wange mroga usingizi wa pono!! ili alale asikumbuke kusali!! lkn hapa walisahau!!! ndo maana wanajifanya eti wamefurahi;
kuuumbe nyuma ya pazia tuliwapiga ngumi za uso!! na ndo kawaida ya wachawi ukimpiga kwa kumpatia atasema ''hilooo limenikosa hiloo , limepiga mti hiloo'' anakuzomea flani hivi, ili umjibu uchawi ukugeukie kimazingara
Sasa km wewe una Maarifa ya kuzimu kiduchu uta mjibu mchawi faster uone muziki wake!! ''Mauchawi yanakugeukia yooote km yote!! kwa kulijua hili Mondi kapiga kimya!! ebu fikiria tu kidogo huyu ni chalii tu wa Mtaani tu hata hatujui sisi, lkn eti amefurahi?!!
Mond kapiga kimyaa! ila sasa sisi tunawapa Makavu Mjue kuwa tunajua kinachoendelea!! Mond angeitwaa tu ile tuzo la mtego wa kichawi mjue ndo ungekuwa mwisho wa wasafi yoote mbaya!!
sometimes ukiwa na Mali, umaarufu, cheo kubwa unatakiwa uwe na Maarifa ya ziada juu ya Ulimwengu wa Giza wana jamii forum mie nawahusia sana mara kwa mara bila kinyongo,
Kwa mfano mtu utafurahia vipi maanguko ya Mtu usiye mjua? ndo maana wazaramo wanasema ''mchawi ndugu'' hao wana maana huyu mleta mada angekuwa na undugu na Mond tungesema '' Naam sasa yametimia!!
Mashabiki wetu muwe makini na hawa watu wa kuzimu.............Dawa yao hao akikuchanganya tu usijue pa kutokea wewe mtaje tu Yesu wa Nazareth!! wanakatikaga mbaya, sasa hapa nimetamka hivi hutawaona!