Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa

Habar wana JF,

Nashukuru mungu wote ni wazima
Mtanisamehe mimi sio muandishi mzuri sana wakuu.

Nimetoka kugombana na wife mpaka nimebaki nashangaa na kuwaza kwa maneno alioyasema wife, nikwamba wife ni mjamzito wa miezi 4 sasa anatimiza ikifika tarehe 13 sasa leo nimetoka kazini nikawa nimekaa kwenye gari nawaza sana kutokana na maisha na life style anayoishi wife sio kabsa kiupande mwingine.

Kutokana na maisha yalivyo toka wife amebeba mimba anaishi life style ambayo kwa upande mwingine bado haijanivutia lakin ni kawaida sana yeye ni 24hrs/7days yupo ndani amelala akichoka anafungua insta atashinda mitandaoni akichoka sebleni kuangalia TV tamthilia zake mwenyewe.

Ni vizuri kupata muda wa kupumzika kwa hali yake lakini mimba sio mzigo au mimba sio ugonjwa ukufanye ushinde ndani 24hrs. Nikampigia sim kumjulia hali kashindaje leo then nikamuuliza unafanya nini akajibu yupo kitandani amelala.

Nikamwambia kiupole sana na kiutaarabu kuwa mkewangu em bas uwe unatoka na kuchakarika kuna duka la biashara now yupo kijana uwe hata unakwenda basi kuangalia mambo yanaendaje sio hadi mimi nitoke kazini nimechoka nipitie tena huko wakati wewe upo tu nyumbani umetulia vituvingine ni kuichangamsha akili na kupambana kuliko kushinda tu ndani mamaangu wewe sio mgonjwa.

Kusema kwamba huwez kutembea mbona kuna wanawake wana mimba lakini wanachakalika wengine unakutana nao anatumbo kubwa kabeba beseni lake la mboga anatembeza mitaani wengine wanakimbiza maofisi na matumbo yao tena makubwa lakin wanachakalika asubuh na mapema kashafika ofisi nikamwambia hayo siyo maisha uyaotaka kuishi.

Sijajua nihilo tu au kuna mengine ila Alivimba na kuanza kuongea kwa hasira na kuongea maneno mengi sana ambayo sikutegemea na kusema kuwa namnyanyasa mara kisa kubeba mimba naanza kumuona mjinga so nisimfananishe na hao wajinga ye anaakili zake na anajua anachofanya, mara nimeanza kumuona mzigo kwangu kwakuwa kabeba mimba duuh wakuu nilibaki nimeishiwa nguvu maana sikutegemea kama ndo yangekuwa hayo mara sasa ataondoka ataenda kukaa kwao duuh.

Kiukweli sikumjibu chochote nikaamua kutumia hekima tu maana yeye teali alishapanda kaamua kushuka nakumuacha nikakata simu yangu nikawaza sana huyu skuiz amekuaje kwamba ndo mimba inampeleka hivyo au nikaacha kama yalivyo lakin narud nyumbani njiani ninawaza sana yale maneno Nikafika home nikaingia ndani nikamkuta kakaa sebleni, sikumsemesha chochote nikapitiliza jikoni nikamkuta beki 3 anapika nikamuuliza kuwa dadaako kala akasema ndio alikula na saivi ndio napika chakula cha usiku nikasema powa nikapitiliza chumbani nikaingia bafuni nikaoga nikamaliza nikapanda kitandani nikapumzika.

Dakika 3 akaja chumbani kimya sikumsemesha kakaa nikamwambia jiandae kesho nakupa nauli yakuendea huko kwenu iliuepuke hayo manyanyaso unayosema.

Nikainuka nikavaa nikafungua mlango kabla sijatoka nikamwambia natoka napiga simu kwenu kesho wakupokee nikaondoka zangu now nipo somewhere nimetulia kwanza ila kweli nimewaza huyu kesho namsafirisha kweli sioutani acha aende kwanza kwao akatulie akikaribia kujifungua nitamfata wakuu kwasababu najitahdi sana anapopanda namimi nisipande maana minajijua nina hasira sana
Kaka, ndo Mimba yenu ya kwanza?.

Relax bana, Wakati mimba mjamzito anapitia mabadiliko mengi .

Tena Bora wako anashinda nyumban, **** wengine wanawachukia waume zao kwelikweli, hataki hata Umsogelee .

Relax , wee jifanye mjinga... Alafu mbona hamjagombana, majibu yake alokuambia ni sehemu ya madeko ya Hawa Wanawake ,ndivo walivyo , wameumbwa kua na midomoooo
 
Ushauri huu natoa bure sitaki hata mia yako. Rudi home, tulia, muombe msamaha kabisa!

Kesho wahi kutoka job, Rudi home mchukue nendeni Dukani, mpitishe kwenye ice cream ama pahala penye miti mingi, ama maji, aone ukuu wa Mungu na ajue mimba siyo ugonjwa.

Mkeo ana upweke sana ni vile hujajua tu, suala la ww kwenda job kurudi siyo issue kwa kipindi hiki

Kesho kutwa yake mpeleke akafanyiwe massage nzuri kabisa, atengeneze kucha, nywele ukiwepo, nasisitiza ukiwepo!

taratibu kabisa utashangaa na roho yako, utarudi kushukuru.

Umpeleke kwao ndo wamemtia mimba? em tuliza akili mwanaume

Sawa MKUU nimekuelewa
 
Kweli mwache aende kwao usije haribu ulichokivuna best Wala usimkaripie nimaisha tu unayapitia ya baba kijachoo

Sure MKUU sipendi kumkwaza hata yeye anajua lakin now naoma kama ana disrespect frani hivi
 
Kosa lako lilianzia hapa.

Hujawahi kufuatilia mambo ambayo mwanaume hapaswi kumuuliza mwanamke.

Hilo swali hukupaswa kumuuliza kwa njia ya simu umeharibu dogo, kosa lingine ni wewe kuzozana na mjamzito.
Nadhani umri wako bado mdogo ktk ndoa.

Nikushauri tu "ahirisha kumpeleka kwao badala yake mtake radhi, jishushe kabisa" utakuja kunishukuru

Kumbuka hasira huzaa hasara.

Sawa Mkuu nimekuelewa
 
Aisee nimeona hili jambo niliweke hapa.
Kila aliyewahi kufanyiwa kioja na Mama Kijacho Ateme nyongo yake hapa.

Moja ya kisa ambacho sitakuja kukisahau ni siku niliyoamshwa usiku wa manane na mke wangu na kuniambia anataka "Bunduki" Khaaa! nilichanganyikiwa sana Bunduki! mimi Mlinzi au Polisi? Au atazaa mtoto Komandoo au mwanajeshi! Alinifanyia fujo tangu saa nane hadi kumi na moja alfajiri.

Mbili Kuna siku Wakati tunashuka kwenye gari nyumbani niliona vipande viwili vya keki za Tsh mia mia ndani ya gari. Mwenzangu alishuka kwemye gari na kwemda moja kwa moja chumbani kulala. Mimi Nikavichukua Vipande vile na kuviweka Jikoni., Kule Akaja dogo mmoja, akavichukua na kula. Baadae alipoamka tukiwa chumbani nikamsikia anasema "ooh nimechoka Hebu ngoja niende nikachukue keki zangu nile"[emoji1787][emoji1787] Nikamwambia "Ooh zile keki nimempa Dogo amekula" Moto ambao tuliwashiwa sijawahi kuuona, Kutafuta suluhu ilibidi niongee na mama mkwe ambembeleze ila wapi![emoji52] Nikafunga safari kwenda kutafuta keki nikakosa zile za mia mia nikanunua za 7500, nilipomletea akazidi kucharuka! Nikakosa simile na kugeuka simba huyoo akanywea na kuanza kula zile huku akizisifia kuwa ni nzuri.

Wadau leteni mambo
 
Habar wana JF,

Nashukuru mungu wote ni wazima
Mtanisamehe mimi sio muandishi mzuri sana wakuu.

Nimetoka kugombana na wife mpaka nimebaki nashangaa na kuwaza kwa maneno alioyasema wife, nikwamba wife ni mjamzito wa miezi 4 sasa anatimiza ikifika tarehe 13 sasa leo nimetoka kazini nikawa nimekaa kwenye gari nawaza sana kutokana na maisha na life style anayoishi wife sio kabsa kiupande mwingine.

Kutokana na maisha yalivyo toka wife amebeba mimba anaishi life style ambayo kwa upande mwingine bado haijanivutia lakin ni kawaida sana yeye ni 24hrs/7days yupo ndani amelala akichoka anafungua insta atashinda mitandaoni akichoka sebleni kuangalia TV tamthilia zake mwenyewe.

Ni vizuri kupata muda wa kupumzika kwa hali yake lakini mimba sio mzigo au mimba sio ugonjwa ukufanye ushinde ndani 24hrs. Nikampigia sim kumjulia hali kashindaje leo then nikamuuliza unafanya nini akajibu yupo kitandani amelala.

Nikamwambia kiupole sana na kiutaarabu kuwa mkewangu em bas uwe unatoka na kuchakarika kuna duka la biashara now yupo kijana uwe hata unakwenda basi kuangalia mambo yanaendaje sio hadi mimi nitoke kazini nimechoka nipitie tena huko wakati wewe upo tu nyumbani umetulia vituvingine ni kuichangamsha akili na kupambana kuliko kushinda tu ndani mamaangu wewe sio mgonjwa.

Kusema kwamba huwez kutembea mbona kuna wanawake wana mimba lakini wanachakalika wengine unakutana nao anatumbo kubwa kabeba beseni lake la mboga anatembeza mitaani wengine wanakimbiza maofisi na matumbo yao tena makubwa lakin wanachakalika asubuh na mapema kashafika ofisi nikamwambia hayo siyo maisha uyaotaka kuishi.

Sijajua nihilo tu au kuna mengine ila Alivimba na kuanza kuongea kwa hasira na kuongea maneno mengi sana ambayo sikutegemea na kusema kuwa namnyanyasa mara kisa kubeba mimba naanza kumuona mjinga so nisimfananishe na hao wajinga ye anaakili zake na anajua anachofanya, mara nimeanza kumuona mzigo kwangu kwakuwa kabeba mimba duuh wakuu nilibaki nimeishiwa nguvu maana sikutegemea kama ndo yangekuwa hayo mara sasa ataondoka ataenda kukaa kwao duuh.

Kiukweli sikumjibu chochote nikaamua kutumia hekima tu maana yeye teali alishapanda kaamua kushuka nakumuacha nikakata simu yangu nikawaza sana huyu skuiz amekuaje kwamba ndo mimba inampeleka hivyo au nikaacha kama yalivyo lakin narud nyumbani njiani ninawaza sana yale maneno Nikafika home nikaingia ndani nikamkuta kakaa sebleni, sikumsemesha chochote nikapitiliza jikoni nikamkuta beki 3 anapika nikamuuliza kuwa dadaako kala akasema ndio alikula na saivi ndio napika chakula cha usiku nikasema powa nikapitiliza chumbani nikaingia bafuni nikaoga nikamaliza nikapanda kitandani nikapumzika.

Dakika 3 akaja chumbani kimya sikumsemesha kakaa nikamwambia jiandae kesho nakupa nauli yakuendea huko kwenu iliuepuke hayo manyanyaso unayosema.

Nikainuka nikavaa nikafungua mlango kabla sijatoka nikamwambia natoka napiga simu kwenu kesho wakupokee nikaondoka zangu now nipo somewhere nimetulia kwanza ila kweli nimewaza huyu kesho namsafirisha kweli sioutani acha aende kwanza kwao akatulie akikaribia kujifungua nitamfata wakuu kwasababu najitahdi sana anapopanda namimi nisipande maana minajijua nina hasira sana

Mpuuze, itakusaidia sana, tumepita huko dogo unakopita na angalau tungepata ushauri kama huu.
 
Weacha tu mkuu sababu kuna dada nafanya nae kazi ofisi moja yule dada alikuwa mjamzito yule dada alikuwa anakuja kazini mbaka anajifungua ndo wakampa likizo ya uzazi lakin alikuwa na uwezo wa kuomba likizo before hata ya kujifungua akajifungulie hata kwao lakini wapi mbakatulikuwa tunamuonea huruma kazi nyingine za kiofisi tunamsaidia katoka kujifungua January mtoto wa kiume
Kuna mdada alikuwa mwl.kafundisha Leo kesho yake akaenda kujifungua,alivyopata mimba nyingine miezi 2 tu hawezi chochote,akitembea kidogo miguu yote inavimba Hadi huruma
 
nilikua napenda ugali mbichi na ngisi wa kuchemsha nawajaza maembe tele, maskini baba wa watu anakula akifika kati ananawa ananambia siwezi kula maede, mimi nasogeza sahani naula wote nabeua natafta maji nalala, sjawah kumuamsha usiku wa manane nalilia kitu
 
Mkuu umefanya maamuzi ya kiume zaidi,,,wana akili sana hawa viumbe,,,akupandishie sauti ety then we ujishushe mwanaume nani sasa ndani,,mimba siyo sababu ya yeye kukupandishia, ana yake huyo.

Wanajisahau sana tukishaanza kuwa treat kulingana na hali zao sema tutafika tu MKUU
 
mkuu umemlinganisha na wanawake wengine wanaopiga kazi wakiwa na mimba zao na matumbo yao makubwa, Wala usibishe!

achana na hizo habari, tulia kuwa nae karibu kutengeneza akili yake na mtt ajae, labda kama unaplan ya kupata mtt asiye na akili timamu

Sawa MKUU nimekuelewa
 
Mh nimesoma comment nimecheka tu kka nakumbuka nilikuwa na soma na kaa kwa kaka yangu shemeji alikuwa mjamzito yey mimba yake ilikuwa siku akijisikia kusafiri anaondoka amwambi mtu

Akiludi ana anafika usiku ana anza njoo na ngazi unampelekea anapanda anaenda safisha fen niny mkiwepo hapo sebleni akishuka anaaza kufoka ukimwambia nikusaidie ataki kaka akiludi anamwambia mwambie mdogo wako awe ananisaidia kazi nachoka

Siku akitibuka anatukasilikia wote sasa wewe hapo ilo tu unataka kumludisha kwao haya angekuwa anakuletea vitmbwi kama hivi ungekaa nae ata nusu saa? Hivi vichache kati ya vingi
 
Back
Top Bottom