Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaka, ndo Mimba yenu ya kwanza?.
Relax bana, Wakati mimba mjamzito anapitia mabadiliko mengi .
Tena Bora wako anashinda nyumban, **** wengine wanawachukia waume zao kwelikweli, hataki hata Umsogelee .
Relax , wee jifanye mjinga... Alafu mbona hamjagombana, majibu yake alokuambia ni sehemu ya madeko ya Hawa Wanawake ,ndivo walivyo , wameumbwa kua na midomoooo
nilikua napenda ugali mbichi na ngisi wa kuchemsha nawajaza maembe tele, maskini baba wa watu anakula akifika kati ananawa ananambia siwezi kula maede, mimi nasogeza sahani naula wote nabeua natafta maji nalala, sjawah kumuamsha usiku wa manane nalilia kitu
Mh nimesoma comment nimecheka tu kka nakumbuka nilikuwa na soma na kaa kwa kaka yangu shemeji alikuwa mjamzito yey mimba yake ilikuwa siku akijisikia kusafiri anaondoka amwambi mtu
Akiludi ana anafika usiku ana anza njoo na ngazi unampelekea anapanda anaenda safisha fen niny mkiwepo hapo sebleni akishuka anaaza kufoka ukimwambia nikusaidie ataki kaka akiludi anamwambia mwambie mdogo wako awe ananisaidia kazi nachoka
Siku akitibuka anatukasilikia wote sasa wewe hapo ilo tu unataka kumludisha kwao haya angekuwa anakuletea vitmbwi kama hivi ungekaa nae ata nusu saa? Hivi vichache kati ya vingi
Hii kauli huwa ina wapumbaza sana.Mwanamke akiwa na mimba anakuwa kama kichaa flani.
Labda utwambie hii tabia imejitokeza tu wakati wa ujauzito au hata kabla amekuwa na tabia hizi. Na hujatuambia hii mimba ni ya ngapi na je km tayari mna mtoto mimba hiyo pia ilileta changamoto km hizi za leo.
NB.
Kabla ya kuoa, mwanaume yakupasa kuwa makini sn hasa kuonesha muelekeo wa maisha wako, misimamo yako na matamanio yako ya maisha waziwazi ili MKE ajue nini unapenda na nini hupendi. Usiogope kumpoteza km utamuweka wazi na akaona hamuendani.
Mimi binafsi huwa nakataa katakata habari za kuhusisha mwanamke kuwa mjamzito na vitendo vitokanavyo na ujauzito huo. Ujauzito sio ugonjwa, sio mzigo, na sio msalaba kwa mume.
Eti wengine wakishika mimba wanasema waume zao wananuka hadi Wana hana vyumva au kulala chini. Serious kweli mimba inaweza kusababisha mume kunuka. "Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe".
Vijana acheni kuishi kizungu eti mwanamke akiwa mjamzito analelewa km yai na ku-misbehave kisa mimba. Na wao wamekuwa wakitumia huu mwanya kufanya vitendo na kutoa majibu ya hovyohovyo kwa waume zao eti kisa mimba inamtuma hivyo. Narudia, kataeni ujinga huo, vinginevyo mtajikuta nyie ndio mmeoolewa.
Mbana sisi tumekuwa tukiona mama zetu wakienda kulima na kufanya kazi tena ngumu huku wakiwa wajawazito, wengine walikuwa wanafanya kazi ngumu hadi siku ya kujifungua. Kwani hao hawakuwa binadamu au wao walitoka sayari gani. Na hadi sasa wanawake km hao wapo wengi na ndoa zao zipo imara.
Hii tabia ya vijana wa kiume kwenda kuoa wanawake wa kishua, wapenda kuvaa vitu artificial mwili mzima, kujikwatua hadi sura zao kubadilika, na wavivu wa kufanya kazi haya ndio matokeo yake. Kijana unaoa kwa kuangalia matako, sura, na umbo kwa kudhani sifa hizo zipo pia kichwani mwa mwanamke. Hatimae ndio unajikuta unaoa mvivu, mzururaji, jeuri, kisirani, katili, kauzu na kila sifa zote za hovyo.
Vijana wa kiume tambueni mwanamke wa kuoa ni tofauti sana mwanamke wa mahusiano ya kimapenzi mnae enda kukutana baa, disko, gesti na sehemu zote za starehe na chafu. Mwanamke wa kuoa hawezi kuwa na sifa zote uzipendazo. Note my words " huwezi kupata mke ,wala mume Bora wa maisha yako mwenye sifa zote unazohitaji, labda umuoe dada yako au uolewe na kaka yako". Kuoa/kuolewa sio jambo la mzaha km mapenzi ya kiurafiki kabla ya ndoa
Pole sana kwa yaliyokukuta mleta mada, maamuzi yako ndio yataleta furaha yako. Kazi kwako ila usikubali kuburuzwa kwa sababu za hovyohovyo km mimba. Wanawake waheshimuni waume zenu acha visingizio vya hovyohovyo km mimba.