Nimegombana na Mke wangu leo mpaka nimeshangaa


Sawa mkuu nimekuelewa
 
Labda utwambie hii tabia imejitokeza tu wakati wa ujauzito au hata kabla amekuwa na tabia hizi. Na hujatuambia hii mimba ni ya ngapi na je km tayari mna mtoto mimba hiyo pia ilileta changamoto km hizi za leo.

NB.
Kabla ya kuoa, mwanaume yakupasa kuwa makini sn hasa kuonesha muelekeo wa maisha wako, misimamo yako na matamanio yako ya maisha waziwazi ili MKE ajue nini unapenda na nini hupendi. Usiogope kumpoteza km utamuweka wazi na akaona hamuendani.

Mimi binafsi huwa nakataa katakata habari za kuhusisha mwanamke kuwa mjamzito na vitendo vitokanavyo na ujauzito huo. Ujauzito sio ugonjwa, sio mzigo, na sio msalaba kwa mume.

Eti wengine wakishika mimba wanasema waume zao wananuka hadi Wana hana vyumva au kulala chini. Serious kweli mimba inaweza kusababisha mume kunuka. "Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe".

Vijana acheni kuishi kizungu eti mwanamke akiwa mjamzito analelewa km yai na ku-misbehave kisa mimba. Na wao wamekuwa wakitumia huu mwanya kufanya vitendo na kutoa majibu ya hovyohovyo kwa waume zao eti kisa mimba inamtuma hivyo. Narudia, kataeni ujinga huo, vinginevyo mtajikuta nyie ndio mmeoolewa.

Mbana sisi tumekuwa tukiona mama zetu wakienda kulima na kufanya kazi tena ngumu huku wakiwa wajawazito, wengine walikuwa wanafanya kazi ngumu hadi siku ya kujifungua. Kwani hao hawakuwa binadamu au wao walitoka sayari gani. Na hadi sasa wanawake km hao wapo wengi na ndoa zao zipo imara.

Hii tabia ya vijana wa kiume kwenda kuoa wanawake wa kishua, wapenda kuvaa vitu artificial mwili mzima, kujikwatua hadi sura zao kubadilika, na wavivu wa kufanya kazi haya ndio matokeo yake. Kijana unaoa kwa kuangalia matako, sura, na umbo kwa kudhani sifa hizo zipo pia kichwani mwa mwanamke. Hatimae ndio unajikuta unaoa mvivu, mzururaji, jeuri, kisirani, katili, kauzu na kila sifa zote za hovyo.

Vijana wa kiume tambueni mwanamke wa kuoa ni tofauti sana mwanamke wa mahusiano ya kimapenzi mnae enda kukutana baa, disko, gesti na sehemu zote za starehe na chafu. Mwanamke wa kuoa hawezi kuwa na sifa zote uzipendazo. Note my words " huwezi kupata mke ,wala mume Bora wa maisha yako mwenye sifa zote unazohitaji, labda umuoe dada yako au uolewe na kaka yako". Kuoa/kuolewa sio jambo la mzaha km mapenzi ya kiurafiki kabla ya ndoa

Pole sana kwa yaliyokukuta mleta mada, maamuzi yako ndio yataleta furaha yako. Kazi kwako ila usikubali kuburuzwa kwa sababu za hovyohovyo km mimba. Wanawake waheshimuni waume zenu acha visingizio vya hovyohovyo km mimba.
 
Wajawazito ni shida unatakiwa ujitoe ufahamu utulie tuu yani ni zaidi ya mwanamke kuwa kwenye period
 
Kuna mdada alikuwa mwl.kafundisha Leo kesho yake akaenda kujifungua,alivyopata mimba nyingine miezi 2 tu hawezi chochote,akitembea kidogo miguu yote inavimba Hadi huruma

Duuh hatari
 
Kwahiyo inakuuma mjamzito kulala!

Acha unyanyasaji. Mimba ni kitu cha kupita tu, miezi 10 maximum. Kuwa na huruma, mapenzi ni huruma.

Halafu mnaosema ooh “flani alibeba kuni tani mbili akiwa na mimba” please stop. Mimba hazilingani, wanawake hawalingani! Just because wewe hujawahi kusumbuliwa na ujauzito usitake kila mtu iwe hivyo.

And maybe yes anadeka, there is nothing wrong with that. Ana mume, hajaiba wa mtu.
 

Unapepo yako mbinguni
 

[emoji23][emoji23] duuh mungu amsamehe
 

Well said MKUU
Umemaliza [emoji736]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…