Wakuu habari ninaomba mawazo na mchango nini nifanye nimegundua mke wangu ananiroga na hii akishirikiana na wazazi wake.
Nimegunduaje nilidukua simu yake na kuona taarifa zote pale alipotoka nyumbani nami kua na wasi wasi kama hio safari si ya usalama kwangu maana ilikua inalazimishwa na wazazi wake kukataa kwingi kukafanya kukasirikiana baina yangu na baba mkwe nikaomba ushauri kwa mzazi wangu wa kiume akanambie we mruhusu ila nilimueka wazi kuhusu kua na wasi wasi na hio safari.
Nilichokiamua ndio nikadukua simu yake na kuweza kuona kila kinachoendelea ukweli ni mtihani ni anataka anikamate kila kitu atachosema mimi niwe naitikia tu na hata nikipata pesa niwe kama bunyenye nafanya kumpa yeye. yawezekana mungu ndie anae nisaidia mimi niliacha tu afanye kila atakalo na alivorudi alirudi na madawa niliyaona na zengine zimeabdikwa kiarabu kwakua najua kukisoma niliona lengo ya hio karatasi.
Ukweli ninasikitika sana katika hili nikitu kimenifanya hata nakua sina hamu nae kabisa. Je, mnashauri nitumie njia gani kumuelimisha aachane na habari za kuniroga maana kama anafata maneno ya wazee wake ajue kua yeye yupo na familia yake?
Napokea ushauri