Yaani unauliza kabisa ufanyeje ili aache tabia ya kukuroga?. Sio kuachana nae mazima?. Labda kama unataka kuwa ndondocha?. MUNGU amekuonyesha.
Labda nikuambie usichokijua, wanawake wengi wanapowaroga waume zao wanakuwa hawajui matokeo yake,hata wewe hujui matokeo. Ni mganga tu anajua. Mwisho wa siku na yeye anaweza kukikosa mazima anachokurogea. Unaweza kufikia kuwa kama zezeta. Mganga anachokifanya ni kufanya ushinde nyumbani tu kama mke anavyotaka uwe wake peke yake. Matokeo yake utakuwa hufanyi chochote unakuwa unakuwa unashinda nyumbani tu kama zezeta