Nimegundua mpenzi wangu akiwa na marafiki zake, huwa ananiita mimi kimburu

Kimburu ni aina ya paka wa porini, paka aliyeasi na kuamua kuishi porini huitwa kimburu. Kimburu ni maarufu sana kwa kukamata kuku wa kienyeji.
 
Mburu kwa kichaga cha Vunjo ni mbuzi sasa kimburu ni "Kambuzi 😁😁
 
Mtoto akitoka kucheza na wenzie,akirudi home kachafuka vumbi mwili mzima...huwa tunasema unaonekana Kama kimburu...
 
Huku uzaramuni ni Ile mt mbadi inayopasulia mayai kwenye koo inatema maganda wakati imeshakula mtaga mayai kiatambo!
 
Kimburu ni mvizia kuku mnyama anaiba kuku na kuwatafuna inaonekana na wewe ni kicheche . Kisukuma kimburu ni kicheche
 
Kimburu ni paka aliyeasi yaani yule paka aliyetoka kwa bwana wake kulingana na tabia zake chafu may be kuiba mboga au hata kula vifaranga vya kuku na baadaye akafukuzwa na bwana ake kwenda kuishi porini,,, kwahyo maisha yake ni kujitafutia chakula na kula vifaranga vya kuku huyo ndiye KIMBURU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…