Kaka naomba nikupe my expirience kuhusu hili suala la kutoa mimba yaliyonikuta Mimi especially niliyekuwa kwa ndoa..You all can learn pia kupitia mimi
My wife kabla ya kuanza uhusiano nae was a good friend of mine alikuwa na jamaa wake wanadate akapata mimba na akaona si kesi bora aichomoe tena kwa ushauri wa Marafiki na Dada zake yote hiyo ni sababu kuu cha kwanza ni kuogopa wazazi watasemaje..Lakini pili na kubwa jamaa wake alikuwa ana wanawake kama watatno anaotoka nao kwa pamoja na yeye akiwemo..
Mimi huwaga nina mentality ya kupotezea na wengine husema ya kizungu,nikasema yes she made a mistake so siwezi kumhukumu kutokana na alichokifanya as so long as amejifunza..So we started dating kiroho safi bila kuwaza na wala kumkumbushia kuwa ulitoa mimba hata siku moja bali nilikuwa nammind jamaa in a way ila nikapotezea na kusema ajali kazini
Fast foward we started dating na kwa kuwa tulikuwa wote kwenye hustles na tunashirikiana katika utafutaji wote tukaona si busara yeye kupata mimba..so i was very keen kwenye sex kwenye suala zima la kuwithdraw nikiwa nina cum so hakuwahi kuwa na wasiwasi wa mimba during kudate kwetu..
Baada ya miaka miwili na nusu nikaona why not get married kwa mtu ambaye she has been almost perfect kwa vitu vingi sana na ana mapungufu machache..so tukaingia kwa ndoa..Then after six months tukaamua tuanze tafuta mtoto kwa kila namna..Na hapa sasa ndo ikawa Interesting..Jaribu sana kwa kila namna for like a year,ila waapii..I was ready kusubiri na nilikuwa patient sana na niko nae bega kwa bega...Mama yangu Mzazi pia alikuwa na sisi bega kwa bega..baaada ya mwaka kupita akaanza kupata shauku ya kupata mtoto na anatamani kweli kweli Na mimi kwangu ikawa ni hivyo pia..
Tukaanza sasa officially kuhangaika nae kwa kuonyesha kila namna ya support kwake kwenye kutafuta suluhisho la tatizo lake,sihesabii gharama tulizotumia na usumbufu like ni almost around mil 5 kwa kuhangaika kwa madaktari bingwa hapa Dar yote na hata mitishamba ya kila namna..sasa ikawa imepita miaka 3 hadi hivii sasa hatujabahatika kupata mtoto..
Kubwa sasa ni juzi hapa tukaenda kwa Mtumishi mmmoja na kiukweli ingawa mimi haya mambo ya dini siamini lakini kwa kuonyesha support kwa mke tukaenda kwa huyo mtumishi na hapo ndipo ukweli ukadhihirika ambao umebadilisha kila kitu na uelekeo wa ndoa kwa ujumla..
Ilikuwa hivii,Mtumishi akamuuliza anhaa naona umeamua kuja na mume wako na ni jambo zuri sana...akasema ndiyo...Basi mtumishi akamuuliza na ndiyo kwanza anatuona kwa mara ya kwanza..Akauliza swali unahangaika na mnahangaika sana kupata mimba lakini mume wako anajua ukweli..???.Mi nilikuwa chilled na kusema aaaah kama ni kutoa mimba hilo nalijua alitoa mimba yes na niliridhia bila shida...akamuuliza swali jingine ni mimba ngapi ushawahi kutoa...Mi kwa kujiamini nikawa najua ni mmoja ila nikashtushwa na ukimya kwanza wake...Mapigo ya moyo yakaongezeka kwanza kwa sekunde zile 5 alizokaa kimya
Nikajisemea haraka mbona anasita tena..Then nikasikia akimjibu ni tatu(3) daaaaaah aisee nilipigwa na ubaridi pale na hasira zikanijaa lakini nikaact calm kwanza...Nikashusha pumzi lakini nikawa siamini lile jibu kutoka kwake...Na ndiyo ilikuwa muda tunaondoka so tukaingia kwenye gari tukawa tunaondoka eneo tulilokuwepo huku mtumishi akitupa lift..Nilibadilika ghafla nikawa nasikia baridi na kutetemeka kwa hasira sana sana...sijawahi kuwa na hasira toka nimezaliwa kama ile siku..
Tukashuka mtumishi akatuacha mitaa mitaaa.Akawa ananiangalia asielewe anaongea nini...Tulivyokuwa kituoni swali la kwanza nikamuuliza like why uliamua kujifanyia hivii kwa mwili wako and la pili nikamuuliza why did you choose to hurt me katika namna hii...I was so very hurt kiasi cha kwamba nimeapa sitofikia ile hatua kuumia namna ile..Tukapanda Daladala kuelekea mitaa yetu ya nyumbani lakini kwenye daladala natetemeka nina hasira sana na ninachokitamani ni kuvunja vioo vya gari kwa ngumi ili nitulize tuu hasira...huwaga niko hivyo,nikivunja kitu ni bora zaidi kwa kuwa siwezagi kupiga...Maana ninaweza mchakaza mtu na nikaishia pabaya...
Fast foward tukashuka kwa Daladala tukatembea kama dakika moja hivii,Nilimtikisa vya kutosha bila kumpiga hata maana ningeweza kumuharibu kwa namna ninavyojua mimi...Nilimshika sana na kumtikisa huku ninalia kama mtoto mdogo na kumuuliza kwa nini aliamua kufanya hayo na kunisababishia pia kupitia a lot of problems kwenye marriege huku labda tungeju Intensity ya tatizo mapema ningekuwa tayari kupambana nae kama ningeweza maana kama niliweza kukubaliana kuwa nae kwenye mahusiano huku nikijua alifanya abortion tayari angeweza kunijali enough kunieleza ukweli na si kunificha kama kweli she really cared about me as much as nilimpenda yeye bila conditions
Asee nililia sana bila kujua namfanyaje pale,she was also crying kusema kuwa aliogopa kutokana na hiyo Idadi na nisingemuelewa lakini nikamwambia hukusaidia na ona tunaingia kwa matatizo ilihali intensity ya tatizo analijua yeye..Kiukweli nilikuwa down sana and so devastated..Tulikaaa njiani kwa almost 1hour wote soaking in tears na niko na hasira sana...Tukaelekea nyumbani,kilichoendelea ni kuvunja vikombe kwa hasira na kioo cha chumbani cha kujiangalia.....
Niseme tuu ni expirience katili sana niliyowahi kupitia maishani mwangu so far ila imenifunza sana,Bottom line nimemsamehe whole heartedly ila mambo hayako the same tena..Vingi vimebadilika lakini unajifunza kumove on na kuendelea...Good thing hata hospital walisema she can still conceive sema uvumilivu tuu,Nimempa chances lakini kiukweli kuna conditions nyingi sana...
Yote ya yote jifunze kupitia kisa changu,na wengine mnaotetea mtaelewa kutokana na yaliyonikuta mimi...nitakuwepo kujibu maswali yote ambayo pia mnaweza kuwa nayo...