Nimegundua Watanzania wengi ni wapole kwa Sababu ya umaskini, ujinga na maradhi


Sahihi Kabisa.
Hata mambo ya kujitolea serikali inatakiwa ipige Marufuku.
 
NONSENSE.
 
STOCKHOLM SYNDROME - a psychological phenomenon where hostages or victims develop positive feelings and emotional bonds with their captors or abusers, sometimes even defending them, as a survival mechanism in a traumatic situation.

Ukipitia huu uzi vizuri unakiona hiki kitu kwa weupe sana.
Big up muandishi.
Wenzetu wakishakua na mentality na utayari wa kufanya mageuzi ya nchi yetu tutakuja kuungana nao, Lakini kwa sasa hawawezi kutuelewa kabisa.
From Walvis bay, Namibia.
 
Mfano mwingine ni pale ilipo ibuka LBL hapo ndo utajua watu tuu wajinga kiasi gani,watu waliingia kama nyumbu,siku moja jiulize kwa nini watu wanazamia nje,watu wanafuata soft loaf of bread wenye mayai,lakini hivi waulize hata ccm kweli wanataka nini,nadhani jibu hutapata,nchi hii job Ndungai ndo aliongea ukweli,wizi uko kila Kona mpe mtu kazi lazima aibe sababu hajui kampuni inataka nini sababu Kampuni inakaba mno,juzi nimepita kiwanda cha 21 century walahi siha za watu wale zilinifanya nione Mimi ni kichaa,tumexhoka mno kifikra.
 

Hatari Sana Mkuu
 
Kiukweli sijasoma yote. Ila nikuulize, upuuzi anaofanya Trump na Wamarekani wamekaa kimya, nao ni maskini?
Nani kakuambia Wamerekani wamekaa kimya? Hujui kuna kesi ngapi mahakamani dhidi ya maamuzi ya Trump? Hujui Trump kapigwa stop na mahakama asiendelee na hatua nyingine yoyote ya kuisambaratisha USAID? Hujui Trump kapigwa stop na mahakama asiendelee kurudisha wahamiaji haramu haramu makwao?

Hii nchi vijana wengi ni wajinga tu. Wanaijua simba na yanga tu
 
☝🏿🤯Unaunga umasikini, ujinga na maradhi na ukosefu wa ujanja? Kivipi?

hizo ni assumptions

je umasikini, ujinga na maradhi yanapunguza akili au uwezo wa kuwa mjanja?

Ulaya, iliyokumbwa na Umasikini Ujinga na Maradhi kabla ya Industrial revolution, na kwa mantiki uliyotumia, utaweza kusema watu wa Ulaya hawakuwa wajanja kuingia kwenye Industrial revolution?
Ukifuatilia kwenye huduma za kijamii zinazotolewa katika taasisi za serikali kama Hospitalini au hata Jeshi la Polisi utaliona tatizo Hilo kirahisi zaidi.

Watanzania sio wapole kiasili Bali wengi wao ni Maskini na wajinga. Hivyo upole unaonekana kwa sehemu kubwa ni hawana namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuwa wapole.
sumu
Mtanzania anaweza akawekwa kwenye benchi hata masaa matatu bila Sababu za maana na akatulia tuu. Sio kwamba ni Mvumilivu au Mpole hapana. Hapo atakuwa aidha ni Maskini asiye na lolote au Mjinga ambaye hajasoma akaelimika.

Umefanya huo ulinganishi na nchi zipi na taasisi gani hizo ambazo huwezi ukawekwa benchi hata masaa matatu?

Jana ama juzi ndio uliyoyaona hayo mloganzila? Na kama ndio uliyaona wewe ulifanya nini?

Ulibakia unashangaa Ama kwa sababu wewe sio Mtanzania hukushangaa? Utuambie ulifanya nini baada ya kuona hivyo
*
*
*
Huwezi mkuta mtu mwenye akili timamu na ambaye katoka familia iliyonyooka akaongea misemo ya kipunguani kama hiyo ya Tafuta pesa.
*
Wenye Akili wote na matajiri wanajua pesa inahitaji Mifumo Bora ya Sheria katika utafutaji ikiwemo kujiajiri na kuajiriwa hapo utahusisha na mambo ya Kodi, ulinzi wa Mitaji n.k.
*
Sasa mtu unamwambia atafute pesa, anakuuliza kwa namna ipi,aajiriwe alipwe Laki mbili itamtosha?
Alime tikitiki au korosho kuna soko la uhakika? Au ndio abeti?
*
🙌🏾
Lazima tujali watu wetu. Huo ndio Uongozi na utawala Bora.
Nilishasema kama Mtibeli hatuwezi epuka sera za UVAMIZI kama kweli tunataka kupiga Hatua.
Utanganyika wako ni lazima utiliwe mashaka. Lugha iliyotumika hapo juu inadhihirisha kwamba una Uraia wa nchi nyingine. Watibeli ndio nini?

Sera za Uvamizi au Ukoloji mamboleo. Yaani huko kote unasema Watanzania ni wapole, wajanjaruke halafu kwenye kauli hizo hizo unawataka wawe even more Submissive and subjugated eiti kwasababu ni njia ya kupiga hatua ya maendeleo?

Hatahivyo ni wapi(nchi)umefanya hizi comparisons?
Hayo maviwanda kama yanaulazima wa kuwepo tafuteni vibarua kutoka mataifa mengine wafanye hizo Kazi.
☝🏿🤔Nyie watibeli kwanini msifanye hivyo basi kama unavyojinadi ni mchapa/wachapa kazi?
☝🏿 Hapo kidogo ume make sense.
Serikali, usalama wa taifa, vyama vya siasa, Hatuwezi kujiona Tupo salama katika nchi yetu hii ambayo imejaa mvamvuli wa upole kumbe ni Ulofa uliosababishwa na Umaskini na Ujinga.

Umasikini na Ujinga? Umasikini unafananaaje
Nchi Ile iwe Salama sio kuwa na Jeshi IMARA lenye silaha IMARA.
Nchi Ile iwe Salama lazima wananchi wake wawe HURU.
Wasiwe Watumwa kwa wageni.

Wasifanyane Watumwa wao kwa wao.

Nchi ambayo wananchi wao wapo Huru lazima iwe na ulinzi na usalama Mkubwa.
Hapo unajikanganya. Huko juu umedai ili nchi iwe salam haitaji jeshi imara na silaha imara, sasa utueleze, hilo jeshi litakuwa la kufanya nini? Unawezaje kuhakikishia usalama wa raia iwapo huna jeshi imara na silaha imara?😌🤔
*
Haishangazi kusikia utekaji, mauaji ambayo hayafanyiwi uchunguzi wowote, na watu wapo Kimya kana kwamba hakujatokea chochote. Hahitaji uwe na akili nyingi sana kugundua hatari iliyopo.
Kwa ukweli, ulitaka watu wafanye nini. Mpaka hapa namaliza kuandika kuna watu zaidi ya elfu moja wametekwa wamepotea au wameuwawa duniani, na kuna nchi nyingine kama Marekani watu bado hawajapatikana miaka mingi sana, je ni kwasababu wamekosa Ujanja? ama Raia wao wako kimya?- oversimplifying, overgeneralizing
Tunahitaji Tanzania ambayo watu wanapendana Sana.
Kwa sababu kwenye upendo kuna umoja na ushirikiano na furaha.

Sasa ukiondoa upole kupendana si itakuwa ni kama ngumu?
Tunahitaji Tanzania yenye HAKI kwa Sababu Haki ndio utaifa wenyewe.

HAKI baina yetu wenyewe kwa wenyewe. Mtanzania Kwanza.
Nina mashaka sana na Utanzania wako bwashee.
Mabadiliko haya yaanze na mtu Mmoja Mmoja.
Maana kuna watu wanataka tuu watu Fulani wabadilike labda viongozi huku wao hawataki kubadilika.
Mabadiliko unaanza nayo wewe.
Upo sahihi na mtazamo huo, ila nafikiri mabadiliko uyaanze mwenyewe kwanza mkuu. Si ajabu umendika haya watu wabadilike, anza mwenyewe kama unavyodai, na ukubali huwezi wapangia Watanzania wafuate tabia za watu wengine kufanya shughuli zao.
Sio unahudumia wananchi labda fundi nguo unachelewesha Kazi za watu. Huna tofauti na hao wengine,
Au fundi Mwashi unaiba vifaa vya Ujenzi na kuihujumu nyumba ya Mteja wako.
I disagree. Hakuna Nchi yeyote ile ambayo haina watu au jamii enye hayo matatizo, nabhiyo haina maana nasema tuachie tu, lakini kudai ni hulka za Watanzania pekee, nakataa katu katu.

Au upo hospital ni Daktari au Nurse, hudumia watu Kwa haraka na ufanisi watu waendelee na mambo mengine.
*
Mwalimu, sio unapigapiga kelele,unatukana Wanafunzi wako na kuwatolea Maneno yasiyo na kichwa Wala miguu kama mwendawazimu. Hufundishi vizuri na unategea. Taifa halijengwi hivyo.
*
Taifa lenye UKWELI na akili.

Mtibeli Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master.
Kwa sasa Dar es salaam
*{nitarudi}
 
Una hoja
 
Hebu wajuvi wa mambo mtujuze angalao nchi 3 au 5 duniani za mfano zenye raia walio elimika, werevu au smart ili walao tuone tujifunze walifanyaje nasi tujipange wapi tuanze au turekebishe.
Kuwa na nchi raia wake ni maskini, hohehahe, wasiojitambua bali kupelekwapelekwa tu haipendezi.
 
Ukweli mtupu...Malofa ni wengi sana na huwa yanavaa sare za mbogamboga fc huku yako hohehae yanacheka tuu bila kujua adui yao ndo huyo waliyo vaa
 
Tanesco wanaweza kukata umeme wiki bila taarifa yeyote na unakuta mtaa mzima watu wapo kimya.Hapo hujasema idara ya MAJI ambayo imekuwa kilio kwa wengi.Yaan hata kumuuliza tu M/kiti wa kitongoji hakuna.

Unajiuliza hapa nimezungukwa na watu au misukule?
 
Kwani Ukiwa na pesa huwi mpole? Umeanza Kuandika pumba maana wenye pesa hapa Tanzania ndio huwezi wakuta kwenye harakati wanaogopa TRA na kupoteza hela zao.

Ila ni ukweli mtupu Kwa sehemu kubwa,ila Mimi siko hivyo Huwa nakiwasha.
 
Kwani Ukiwa na pesa huwi mpole? Umeanza Kuandika pumba maana wenye pesa hapa Tanzania ndio huwezi wakuta kwenye harakati wanaogopa TRA na kupoteza hela zao.

Ila ni ukweli mtupu Kwa sehemu kubwa,ila Mimi siko hivyo Huwa nakiwasha.

Ukiwa na pesa huwezi kuwa mpole wa kijingajinga
 
mkuu umenena vyema kabisa, juzi nimepanda bajaji, dere kamwona mdada wanafahamiana kasimamisha daladala wanaanza salimiana na stori kama dk 3 hadi tulipo muuliza unajua tunaenda kufanya nini huku ndio kustuka kuacha salamu
 
Utawakoromea uliowazidi hela ila huwezi.leta jeuri Kwa Serikali unless uungane nao.

Watumishi wa Umma sio Serikali
Na serikali lazima iangalie Haki za watu na kuheshimu watu. Hiyo ndio serikali. Tofauti na hapo haiwi tena serikali Bali Genge la Wahuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…