Nimegundua Watanzania wengi ni wapole kwa Sababu ya umaskini, ujinga na maradhi

Trump kufukuza wakuu wa majeshi au kuwanyima wakina Biden national security briefings kunawagusa na kuwaathiri vipi raia wa kawaida?
Ahahahahaha! Kwahiyo ni ruksa kuvunja Katiba ili mradi tu hujawaathiri wananchi sio? Ahahahahaha! Wewe jiniasi!
 
Hamjambo Wote!

Mimi Niko fresh Kabisa, nashukuru Mungu anasaidia.

Kwenye Mada.

Nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu Kabisa Sababu ya upole au tuite Ulofa kama alivyosemaga Hayyati Benjamin Mkapa.
Nikagundua kuwa Watanzania wengi upole wao( Ulofa) sio tabia wanaoipenda au kujivunia nayo na Wala sio tabia ya Asili Bali Tabia ambayo inatokana na Moja ya mambo haya au yote kwa pamoja yaani Umaskini, ujinga na maradhi

Mbaya zaidi uwe Maskini alafu uwe mjinga huna ujanja hapo lazima uwe Mpole tuu.
Wewe ni Maskini alafu hujasoma, hujui mambo mengi Ukali na ukorofi utautolea wapi.

Ukifuatilia kwenye huduma za kijamii zinazotolewa katika taasisi za serikali kama Hospitalini au hata Jeshi la Polisi utaliona tatizo Hilo kirahisi zaidi.

Watanzania sio wapole kiasili Bali wengi wao ni Maskini na wajinga. Hivyo upole unaonekana kwa sehemu kubwa ni hawana namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuwa wapole.

Mtanzania anaweza akawekwa kwenye benchi hata masaa matatu bila Sababu za maana na akatulia tuu. Sio kwamba ni Mvumilivu au Mpole hapana. Hapo atakuwa aidha ni Maskini asiye na lolote au Mjinga ambaye hajasoma akaelimika.

Fikiria mtu anafika hospitalini, yupo foleni anaona foleni haitembei, haulizi Sababu, kumbe Ofisini Daktari anapiga Stori au anachat na simu.
Au Mteja(Mgonjwa) anahudumiwa mara anatokea Daktari mwingine anakuja hapo Ofisini wanaanza kupiga Stori sio chini ya dakika tano.na Stori zenyewe hazina uhusiano na mambo ya Kazi ya Udaktari. Mgonjwa yupo hapohapo tuu anashangaa shangaa kwa ujinga wake.

Nenda Mwendokasi pale, mnaweza kukaa Lisaa hata limoja, mmejaa haswa. Watanzania wamekaa kwa upole wa bandia, hawana chakufanya.
Wahudumu wa Mwendokasi hawawajibiki kwa Sababu walishawadharau Watanzania.
Viongozi wa taifa nao wanajifanya hawaoni kwa Sababu wameshawadharau Watanzania kwani watafanya nini hao watu maskini na wajinga wasioweza kufanya lolote lile kujisaidia.

Twende kwenye Ajira.
Ndugu zangu jamani wanateseka haswa.
Hakuna cha upole hapo ni Ulofa.

Watu wanaajiriwa ni waalimu madaktari tena wadegree lakini mishahara Yao ukiambiwa utacheka kwa kuwahurumia.
Hivi MD au Mwalimu wa degree ni wakulipwa Laki 3 na serikali IPO, vyama vya wafanyakazi vipo, Dola IPO, usalama wa taifa upo, CCM IPO, chadema ipo. Viongozi wa Dini wapo 😂😂.
Kweli!
Mtu wa degree alipwe Laki Tatu na jamii IPO inaona kawaida. KWELI!
Unajua maana yake hiyo?

Kama mtu wa degree yaani mwenye elimu ya juu kabisa analipwa pesa za namna hiyo vipi Yule ambaye hajasoma Kabisa.
Unajua kimantiki ni kwamba Yule ambaye hajasoma atakuwa kwenye Hali mbaya zaidi.
Maana waajiri watatumia msemo na nahau kusema kama WA degree analipwa laki Tatu wewe nikulipe Laki Tatu ya nini na uliishia kidato cha nne au hukusoma Kabisa.

Alafu kuna Yale majitu majinga Kabisa na bila Shaka yametokea familia zile Fukara Kabisa na sio maskini utayasikia yakisema tafuta Pesa.

Huwezi mkuta mtu mwenye akili timamu na ambaye katoka familia iliyonyooka akaongea misemo ya kipunguani kama hiyo ya Tafuta pesa.

Wenye Akili wote na matajiri wanajua pesa inahitaji Mifumo Bora ya Sheria katika utafutaji ikiwemo kujiajiri na kuajiriwa hapo utahusisha na mambo ya Kodi, ulinzi wa Mitaji n.k.

Sasa mtu unamwambia atafute pesa, anakuuliza kwa namna ipi,aajiriwe alipwe Laki mbili itamtosha?
Alime tikitiki au korosho kuna soko la uhakika? Au ndio abeti?

Njoo kwenye Viwanda huko ndio utajua kuwa Watanzania sio kwamba ni wapole Bali ni umaskini na ujinga ndio adui aliyewamaliza.
Mtu anafanya Kazi masaa zaidi ya 12. Hicho kimshahara usitake kukisikia kwani itakuwa murder Case. Utakufa nakuambia.

Nilishawahi kusema na kuandika ni Bora tusiwe na kiwanda hata kimoja kuliko kuwa na maviwanda yanayogeuza Mwananchi hata Mmoja kuwa Msukule au mtumwa.

Lazima tujali watu wetu. Huo ndio Uongozi na utawala Bora.
Nilishasema kama Mtibeli hatuwezi epuka sera za UVAMIZI kama kweli tunataka kupiga Hatua.

Hayo maviwanda kama yanaulazima wa kuwepo tafuteni vibarua kutoka mataifa mengine wafanye hizo Kazi.

Wanaosema hivyo viwanda vinaleta Ajira nataka kuwaambia hakunaga Ajira za kuumiza watu na kuwafanya wawe Watumwa katika nchi Yao wenyewe. Hizo Kazi ngumu za shokoa zinahitaji ziwekewe Sheria inayoeleweka na maslahi ya wafanyakazi yawe Bora.
Kama haiwezekani vifutwe tuu.
Hao vijana wafanye shughuli zao zingine.

Serikali, usalama wa taifa, vyama vya siasa, Hatuwezi kujiona Tupo salama katika nchi yetu hii ambayo imejaa mvamvuli wa upole kumbe ni Ulofa uliosababishwa na Umaskini na Ujinga.

Nchi Ile iwe Salama sio kuwa na Jeshi IMARA lenye silaha IMARA.
Nchi Ile iwe Salama lazima wananchi wake wawe HURU.
Wasiwe Watumwa kwa wageni.
Wasifanyane Watumwa wao kwa wao.
Nchi ambayo wananchi wao wapo Huru lazima iwe na ulinzi na usalama Mkubwa.

Na Vita yoyote lazima watoboe. Iwe vita ya mapigano ya silaha za kiteknolojia, au vita ya Magonjwa, au Vita yoyote Ile.

Lakini nchi ambayo watu wake hawapo Huru. Kwa falsafa za Kitibeli tunasema nchi hiyo haiko Salama na Wala haina ulinzi wa maana.
Ni kwamba, nchi au taifa hilo lipo mikononi mwa maadui. Ingawaje kwa Nje wengi wanaweza wasilione Hilo lakini Kwa jicho la ndani au macho ya kimedani au jicho la kifalsafa tunaweza kusema taifa hilo halipo Huru na Uhuru wao upo mikononi mwa maadui. Na ikiwa maadui ndio wameshika taifa lolote lile hiyo itamaanisha taifa husika halipo salama isipokuwa kuna kiini macho.

Haishangazi kusikia utekaji, mauaji ambayo hayafanyiwi uchunguzi wowote, na watu wapo Kimya kana kwamba hakujatokea chochote. Hahitaji uwe na akili nyingi sana kugundua hatari iliyopo.

Tunahitaji Tanzania ambayo watu wanapendana Sana.
Kwa sababu kwenye upendo kuna umoja na ushirikiano na furaha.
Tunahitaji Tanzania yenye HAKI kwa Sababu Haki ndio utaifa wenyewe.
HAKI baina yetu wenyewe kwa wenyewe. Mtanzania Kwanza.

Mabadiliko haya yaanze na mtu Mmoja Mmoja.
Maana kuna watu wanataka tuu watu Fulani wabadilike labda viongozi huku wao hawataki kubadilika.
Mabadiliko unaanza nayo wewe.

Sio unahudumia wananchi labda fundi nguo unachelewesha Kazi za watu. Huna tofauti na hao wengine,
Au fundi Mwashi unaiba vifaa vya Ujenzi na kuihujumu nyumba ya Mteja wako.
Au upo hospital ni Daktari au Nurse, hudumia watu Kwa haraka na ufanisi watu waendelee na mambo mengine.

Mwalimu, sio unapigapiga kelele,unatukana Wanafunzi wako na kuwatolea Maneno yasiyo na kichwa Wala miguu kama mwendawazimu. Hufundishi vizuri na unategea. Taifa halijengwi hivyo.

Taifa lenye UKWELI na akili.

Mtibeli Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master.
Kwa sasa Dar es salaam
Siyo lazima kuandika uzi,unahara hara tu!
 
Ulivyoandika tu daktari mwenye MD na mwalimu mwenye degree analipwa laki 3 nimeacha kusoma hizo takataka zako zingine, nimekudharau na kukupuuza. We ndio mjinga na pengine maskini zaidi kuliko hao unaowananga. Jitu zima unapoteza muda wako kuandika uwongo, upotoshaji, dharau mikogo ya kipumbavu nia yako ni nini? Upuuzwe na hizo nia zako ovu zishindwe.
 
Mp
Kweli baada ya kimya umerudi katika mada zako unaelimisha ,unatukuna kimtindo na kuchochea mabadiliko.

Watanzania asilimia kubwa ni Wapumbavu na wajinga na Ccm ndo hapo wanakula BINGO.

Hapo juu umezungumzia Mwalimu wa degree kulipwa 300K

Yaani ukisikia Mwalimu analipwa 300K ujue anafanya Kazi kuanzia Ahsubui hadi jioni na huo mshahara anapewa tarehe 45

Baadhi ya taasisi chache nazipongeza zinafanya vizuri Kama Kaizirege , .

So Mimi mwaka huu naungana na Tundu Lissu kudai mabadiliko chanya
Mpumbavu mamako we ngedere
 
Wewe akili zako ndogo sana. Unatumiaje pesa zako za mfukoni kufanya kazi za serikali? Afu bado hujioni wewe ni mpumbavu?
Wewe ni zuzu. Unapaswa kujua serikali ni mfumo.

Wewe zuzu umeshindwa kupambana nayo, unaona Mtendaji wa kijiji au nurse ndio adui yako.

Narudia tena wewe ni zwazwa.
 
Hayo maeneo ni ya kuishi ngedere wewe unaendaje kuishi huko halafu unalaumu serikali .Maeneo mazuri huyaoni?
Nimecheka sana ,Kivule iko Ukonga jimbo la Jery Slaa
Huku kiukweli wanatakiwa waishi ngedere ila tuna Akina waitara,Assa Mwambene n.k ila kinatia huzuni mnoo
Mimi binafsi nashangaa wanaoshabikia serikali huku Kivule
 
Ukitaka kujua Tanzania ni masikini nenda vijijini,Dodoma ...achaa...Kuna siku nilienda Kijiji kinaitwa mpk leo wananchimba maji chini wanatumia sio kusimulia nimeona mwenyewe kwa macho yangu ,Nilienda Kijiji cha makanda nikabanwa na haja kwenda chooni Yale maji haja ilikata ikabidi niulize ,haya ndo maji mnayatumia?yule kaka alicheka sana...
Hii nchi kuna watu wachache wanannufaika na vizazi vyao mnooo wengine sisi tia maji tia maji,ila mi nshasema sikai porini na sifanyi kazo porini ,ukiangalia wengine wengi walioko vijijini ni wale ambao wametoka familia duni mfano walimu,watendaji ,manesi na madaktari yaani hyo ajira huko vijijini ndo unafuu ila kwa mtu mwenye watu haendi huko abadani asilani
Mmezunguka Dodoma vijiji vyote karibia nikiangalia maisha ya watumishi wa kule vijijini kiukweli wanatia huzuni sana...hakuna miundo mbinu kabisa,benki mpk mjini network shida ,mawakala wa pesa mfano NMB au crdb wakala hawapo kabisa ,vijiji vichache wapo kama Kijiji cha soya kipo wilaya ya chba ila hizo barabara ni heka heka mnooo....
In short viongozi wa kiafrik ina roho mbaya na wabinafsi wapo pale kimaslahi yao tu
 
Unataka kufanya social engineering.
??

Ukisoma kwa umakini unagundua kuna ulinganishi ambao umefanywa na nchi pamoja na watu wake?

Ni nchi gani hiyo?
 
Umaskini na ujinga umeleta tabia moja ya uchawa.
Tutajie Watanzania nchi moja tu Duniani isiyokuwa ma wajinga na tabia za uchawa.

Ukitaja nchi moja tu, utakuwa umefuta Upumbavu na upuuzi ulioandika.
 
Na hii ndiyo furaha ya Watawala wetu! Amani wanayohubiri kwa nchi yetu imejengwa juu ya hivyo vitatu-Ujinga,maradhi na umaskini.
Na kuna Uoga sasa!
Kilichobaki ni Uchawa.
 
Nyerere alisema maadui wa taifa ni watatu.
UMASIKINI, JINGA NA MARADHI.
 
Kiukweli sijasoma yote. Ila nikuulize, upuuzi anaofanya Trump na Wamarekani wamekaa kimya, nao ni maskini?
Anachokifanya trump akili ya nchi za Dunia ya tatu toka kusini mwa jangwa la Sahara haziwezi elewa, bali ni wale tu wanaoishi Dunia ya 1 na hasa toka taifa lenye nguvu duniani, yaani waamerika wenyewe.
 
Ulivyoandika tu daktari mwenye MD na mwalimu mwenye degree analipwa laki 3 nimeacha kusoma hizo takataka zako zingine, nimekudharau na kukupuuza. We ndio mjinga na pengine maskini zaidi kuliko hao unaowananga. Jitu zima unapoteza muda wako kuandika uwongo, upotoshaji, dharau mikogo ya kipumbavu nia yako ni nini? Upuuzwe na hizo nia zako ovu zishindwe.

Kwamba huna ndugu au jamaa au marafiki waalimu au madaktari wanaolipwa hiyo mishahara huko sekta binafsi?

Kama hauna Tulia. Acha kubwabwaja
 
Back
Top Bottom