Nimegundua Watanzania wengi ni wapole kwa Sababu ya umaskini, ujinga na maradhi

Nimegundua Watanzania wengi ni wapole kwa Sababu ya umaskini, ujinga na maradhi

Kama kawaida yako,simple facts na kufanya generalization
 
"Njaa inadhalilisha heshima na uhuru wa nchi, njaa inatweza utu wa binadamu".Bashiru

Watanzania tuna njaa ya kimwili, kiakili na kiroho.
 
Nafika kwenye hiyo nchi ila nakuta kila mtu analaumu watanzania ,najiuliza je waliopo ni raia wa nchi gani 🤔

Kwenye Filamu Mawazo yako tunaweza kuiita Tanzania kama nchi ya kusadikika ambayo watu wanaoishi humo kila Mmoja anawashutumu wa Tanzania kama watu wajinga, malofa na wasiojielewa.

Kwenye Katuni, inaweza leta tafsiri mbaya zaidi
 
Na ndio hiyo tafsiri ambayo mimi naifikiria kwamba watanzania hata hatujielewi kuwa sisi ni wajinga 😁
 
Kiini kikubwa cha hali hii ya “upole wa Watanzania” ni mfumo wa elimu na matumizi ya ujinga wetu kisiasa. Watanzania wengi siyo wapole kwa asili, bali ni watu waliokata tamaa, waliodhoofishwa kiakili na kiuchumi. Elimu yetu haijengi fikra huru, bali inatufundisha kutii. Hii ni hatari sana kwa taifa. Mfumo huu wa kutengeneza raia wapole na watiifu umetumiwa na CCM kwa miaka mingi ili kuendeleza utawala wake bila upinzani wa maana. Natambua mchango wa CCM katika historia, lakini kwa sasa wamepoteza dira ya dunia ya kisasa.

Tatizo kubwa la CCM sasa ni woga. Woga wa kupoteza madaraka umezaa propaganda isiyokidhi mahitaji ya kizazi cha sasa. Badala ya kufikiri mbele, wamebaki kwenye mfumo wa zamani wa kuongoza kwa vitisho na porojo. Wanapoteza uhalali wa kisiasa, lakini kwa sababu wanajua Watanzania wengi ni maskini na wajinga, wanatumia udhaifu huo kama silaha. Wameanzisha mfumo wa kutoa ‘reward’ kwa watu wachache waliobobea kwenye kupindisha mifumo,wachuuzi wa akili za watu kama machawa, influencers wa kipropaganda, na baadhi ya viongozi wa kidini na mastaa.

Ni kwamba CCM imemaster sana balance ya kudhibiti matarajio ya wananchi kwa kutoa ahadi na propaganda zisizoisha. Lakini sasa kizazi cha leo kimebadilika, kinatazama dunia kwa mtandao. Tatizo ni kwamba, watu maskini huconsume content nyingi, na kwa kuwa hawana elimu ya kuchuja, wanageuzwa kuwa followers wa uongo. Upo mfumo wa kihaini wa kuwafanya Watanzania waendelee kuwa wanyonge kupitia makundi ya “influencers” wanaowarubuni kwa stori, siasa za kihisia, na ndoto za uongo.

Watanzania wengi wanajifanya wapole, wanaongea kwa sauti ya chini, wanajidai watiifu, lakini ukweli ni kwamba wanaumezwa ndani kwa ndani. Ukali wao umenyamazishwa kwa njaa, na upole wao siyo utulivu bali ni kukosa namna. Kuna chuki nyingi zilizojificha mtaani, kuna hasira za kimya, kuna vilio visivyosikika. Taifa likiwa na watu kama hawa, linakua na watu wa kuogopa. Si kwa sababu ni hatari, bali kwa sababu hawajui wapi waelekee wakiamua kulipuka.

Kama tunataka Tanzania yenye utu, haki, na nguvu ya kweli, lazima tufumue mfumo wa elimu na propaganda. Lazima tuache kuongozwa kwa hofu na porojo. Kila Mtanzania aelewe thamani yake,bila kujali elimu wala uwezo wa kifedha. Maana Uhuru wa kweli hauanzi na kura, unaanza na akili iliyo huru kufikiri.
 
Kuna kitu zaidi ya CCM watu wengi hawakioni.

Unajua CCM haipo Kenya, Burundi, Zambia, na nchi zingine za Afrika
 
Kuna kitu zaidi ya CCM watu wengi hawakioni.

Unajua CCM haipo Kenya, Burundi, Zambia, na nchi zingine za Afrika
Hicho kimekuzwa na CCM angalia mfumo wetu wa Elimu. Kila mtu anajua ukivo mbovu na madhara yake na pia Kila mtu mwenye nafasi flani hivi ataongea tu lakini hakuna mwenye guts wa kuubadilisha sababu utaharibu vitu vingi in long term. Hivi unajua mwanangu CCM target Yao ni kua chama Cha milele?
 
Hamjambo Wote!

Mimi Niko fresh Kabisa, nashukuru Mungu anasaidia.

Kwenye Mada.

Nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu Kabisa Sababu ya upole au tuite Ulofa kama alivyosemaga Hayyati Benjamin Mkapa.
Nikagundua kuwa Watanzania wengi upole wao( Ulofa) sio tabia wanaoipenda au kujivunia nayo na Wala sio tabia ya Asili Bali Tabia ambayo inatokana na Moja ya mambo haya au yote kwa pamoja yaani Umaskini, ujinga na maradhi

Mbaya zaidi uwe Maskini alafu uwe mjinga huna ujanja hapo lazima uwe Mpole tuu.
Wewe ni Maskini alafu hujasoma, hujui mambo mengi Ukali na ukorofi utautolea wapi.

Ukifuatilia kwenye huduma za kijamii zinazotolewa katika taasisi za serikali kama Hospitalini au hata Jeshi la Polisi utaliona tatizo Hilo kirahisi zaidi.

Watanzania sio wapole kiasili Bali wengi wao ni Maskini na wajinga. Hivyo upole unaonekana kwa sehemu kubwa ni hawana namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuwa wapole.

Mtanzania anaweza akawekwa kwenye benchi hata masaa matatu bila Sababu za maana na akatulia tuu. Sio kwamba ni Mvumilivu au Mpole hapana. Hapo atakuwa aidha ni Maskini asiye na lolote au Mjinga ambaye hajasoma akaelimika.

Fikiria mtu anafika hospitalini, yupo foleni anaona foleni haitembei, haulizi Sababu, kumbe Ofisini Daktari anapiga Stori au anachat na simu.
Au Mteja(Mgonjwa) anahudumiwa mara anatokea Daktari mwingine anakuja hapo Ofisini wanaanza kupiga Stori sio chini ya dakika tano.na Stori zenyewe hazina uhusiano na mambo ya Kazi ya Udaktari. Mgonjwa yupo hapohapo tuu anashangaa shangaa kwa ujinga wake.

Nenda Mwendokasi pale, mnaweza kukaa Lisaa hata limoja, mmejaa haswa. Watanzania wamekaa kwa upole wa bandia, hawana chakufanya.
Wahudumu wa Mwendokasi hawawajibiki kwa Sababu walishawadharau Watanzania.
Viongozi wa taifa nao wanajifanya hawaoni kwa Sababu wameshawadharau Watanzania kwani watafanya nini hao watu maskini na wajinga wasioweza kufanya lolote lile kujisaidia.

Twende kwenye Ajira.
Ndugu zangu jamani wanateseka haswa.
Hakuna cha upole hapo ni Ulofa.

Watu wanaajiriwa ni waalimu madaktari tena wadegree lakini mishahara Yao ukiambiwa utacheka kwa kuwahurumia.
Hivi MD au Mwalimu wa degree ni wakulipwa Laki 3 na serikali IPO, vyama vya wafanyakazi vipo, Dola IPO, usalama wa taifa upo, CCM IPO, chadema ipo. Viongozi wa Dini wapo 😂😂.
Kweli!
Mtu wa degree alipwe Laki Tatu na jamii IPO inaona kawaida. KWELI!
Unajua maana yake hiyo?

Kama mtu wa degree yaani mwenye elimu ya juu kabisa analipwa pesa za namna hiyo vipi Yule ambaye hajasoma Kabisa.
Unajua kimantiki ni kwamba Yule ambaye hajasoma atakuwa kwenye Hali mbaya zaidi.
Maana waajiri watatumia msemo na nahau kusema kama WA degree analipwa laki Tatu wewe nikulipe Laki Tatu ya nini na uliishia kidato cha nne au hukusoma Kabisa.

Alafu kuna Yale majitu majinga Kabisa na bila Shaka yametokea familia zile Fukara Kabisa na sio maskini utayasikia yakisema tafuta Pesa.

Huwezi mkuta mtu mwenye akili timamu na ambaye katoka familia iliyonyooka akaongea misemo ya kipunguani kama hiyo ya Tafuta pesa.

Wenye Akili wote na matajiri wanajua pesa inahitaji Mifumo Bora ya Sheria katika utafutaji ikiwemo kujiajiri na kuajiriwa hapo utahusisha na mambo ya Kodi, ulinzi wa Mitaji n.k.

Sasa mtu unamwambia atafute pesa, anakuuliza kwa namna ipi,aajiriwe alipwe Laki mbili itamtosha?
Alime tikitiki au korosho kuna soko la uhakika? Au ndio abeti?

Njoo kwenye Viwanda huko ndio utajua kuwa Watanzania sio kwamba ni wapole Bali ni umaskini na ujinga ndio adui aliyewamaliza.
Mtu anafanya Kazi masaa zaidi ya 12. Hicho kimshahara usitake kukisikia kwani itakuwa murder Case. Utakufa nakuambia.

Nilishawahi kusema na kuandika ni Bora tusiwe na kiwanda hata kimoja kuliko kuwa na maviwanda yanayogeuza Mwananchi hata Mmoja kuwa Msukule au mtumwa.

Lazima tujali watu wetu. Huo ndio Uongozi na utawala Bora.
Nilishasema kama Mtibeli hatuwezi epuka sera za UVAMIZI kama kweli tunataka kupiga Hatua.

Hayo maviwanda kama yanaulazima wa kuwepo tafuteni vibarua kutoka mataifa mengine wafanye hizo Kazi.

Wanaosema hivyo viwanda vinaleta Ajira nataka kuwaambia hakunaga Ajira za kuumiza watu na kuwafanya wawe Watumwa katika nchi Yao wenyewe. Hizo Kazi ngumu za shokoa zinahitaji ziwekewe Sheria inayoeleweka na maslahi ya wafanyakazi yawe Bora.
Kama haiwezekani vifutwe tuu.
Hao vijana wafanye shughuli zao zingine.

Serikali, usalama wa taifa, vyama vya siasa, Hatuwezi kujiona Tupo salama katika nchi yetu hii ambayo imejaa mvamvuli wa upole kumbe ni Ulofa uliosababishwa na Umaskini na Ujinga.

Nchi Ile iwe Salama sio kuwa na Jeshi IMARA lenye silaha IMARA.
Nchi Ile iwe Salama lazima wananchi wake wawe HURU.
Wasiwe Watumwa kwa wageni.
Wasifanyane Watumwa wao kwa wao.
Nchi ambayo wananchi wao wapo Huru lazima iwe na ulinzi na usalama Mkubwa.

Na Vita yoyote lazima watoboe. Iwe vita ya mapigano ya silaha za kiteknolojia, au vita ya Magonjwa, au Vita yoyote Ile.

Lakini nchi ambayo watu wake hawapo Huru. Kwa falsafa za Kitibeli tunasema nchi hiyo haiko Salama na Wala haina ulinzi wa maana.
Ni kwamba, nchi au taifa hilo lipo mikononi mwa maadui. Ingawaje kwa Nje wengi wanaweza wasilione Hilo lakini Kwa jicho la ndani au macho ya kimedani au jicho la kifalsafa tunaweza kusema taifa hilo halipo Huru na Uhuru wao upo mikononi mwa maadui. Na ikiwa maadui ndio wameshika taifa lolote lile hiyo itamaanisha taifa husika halipo salama isipokuwa kuna kiini macho.

Haishangazi kusikia utekaji, mauaji ambayo hayafanyiwi uchunguzi wowote, na watu wapo Kimya kana kwamba hakujatokea chochote. Hahitaji uwe na akili nyingi sana kugundua hatari iliyopo.

Tunahitaji Tanzania ambayo watu wanapendana Sana.
Kwa sababu kwenye upendo kuna umoja na ushirikiano na furaha.
Tunahitaji Tanzania yenye HAKI kwa Sababu Haki ndio utaifa wenyewe.
HAKI baina yetu wenyewe kwa wenyewe. Mtanzania Kwanza.

Mabadiliko haya yaanze na mtu Mmoja Mmoja.
Maana kuna watu wanataka tuu watu Fulani wabadilike labda viongozi huku wao hawataki kubadilika.
Mabadiliko unaanza nayo wewe.

Sio unahudumia wananchi labda fundi nguo unachelewesha Kazi za watu. Huna tofauti na hao wengine,
Au fundi Mwashi unaiba vifaa vya Ujenzi na kuihujumu nyumba ya Mteja wako.
Au upo hospital ni Daktari au Nurse, hudumia watu Kwa haraka na ufanisi watu waendelee na mambo mengine.

Mwalimu, sio unapigapiga kelele,unatukana Wanafunzi wako na kuwatolea Maneno yasiyo na kichwa Wala miguu kama mwendawazimu. Hufundishi vizuri na unategea. Taifa halijengwi hivyo.

Taifa lenye UKWELI na akili.

Mtibeli Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master.
Kwa sasa Dar es salaam
Taikon,kuna haja upigwe muda mrefu hadi uchakae na kuchoka.Nimecheka sana.Karibu upate hata dengelua mkuu..
 
Elimu Elimu Elimu
Wakenya pia kuna masikini, lakini wana elimu, ndio maana hawakubali kupelekeshwa, wao any time wanakiwasha wakiona viongozi wanaleta pumba
Huku kwetu, masikini hawana elimu, sababu elimu ya huku ni kukariri sio kuelimika na kujua haki yako

Siyo rahisi kuzijua haki zako mkuu endapo unaandaliwa kuwa roboti la serikali na wanafalsafa!
Unajua kwanini somo la history limekuwa ni option katika shule zetu?
Serikali inataka kuzalisha watenda kazi wengi wasio na uwezo wa kuhoji mambo!miaka ijayo wanaharakati watapungua sana katika nchi yetu!

Nchi ina maajabu hii mkuu,kama huniamin tembelea shule ya kata ya sekondari halafu chagua wanafunzi 30 wa kidato cha tatu au nne kisha wape hesabu hii 6788÷3=?
Watakaopata hesabu hiyo bila msaada wa calculator wakizidi nusu hiyo shule ni nzurii!
 
Back
Top Bottom