Nimeguswa na wale wananchi waliookoa watu ajali ya ndege

Wewe ni mchawi.
 
kwahiyo unaona mtu anakufa unasubiri mtaalam wa uokozi?
usitumie matako kufikiri.
 
In an ideal world where everthing is 100% efficient ulichokiandika pale kiko sahihi 100% ... Lakini kiuhalisia hasa kwa nchi yetu uko chaka kabisa, na umekasirisha watu kwa kujifanya huujui uhalisia wa mambo.

Mvuvi anacheza na maji kila siku, pengine alishaokoa watu au alishajiokoa yeye mwenyewe zaidi ya mara 100. Mtaalam gani wa uokozi majini bongo hii anamzidi mvuvi ujuzi? Hasa wa vitendo?
 
siku utakapopata ajali wewe o familia yako utawaambia watu watakaa hata dk 60 wakisubiri wataalam waone wanawaokoa vip!
 
We mume wako/mke wako, kaka,dada, mama,baba,mtoto au hata wewe mwenyewe ikitokea kupatwa na ajali uko tayari watu wasubiri hizo dakika?
 
Ulaya gani wewe..tumia akili bwana, hivi kusubiri polisi wafike kwenye tukio ni mambo ya ulaya..
we chizi nini?unaona watu wanakufa unasubiri polisi waje kufanya nin sasa?
huo ubongo umejaza makamasi?

polisi si ndo hao wamekuja na virungu vyao kwapani wako pembeni huku wavuvi wakiendelea kuokoa roho za watu.
 
Hongereni sana Wavuvi...mmeonyesha mfano mkubwa na Funzo kwa jamii na Taifa
 
Ulaya gani wewe..tumia akili bwana, hivi kusubiri polisi wafike kwenye tukio ni mambo ya ulaya..
Naomba Mungu siku upate ajali hata ya Gari umebanwa na kitu chochote watu wafike wakuangalie tu wasema tunasubiri professionals waje kukusaidia! Tokea siku hiyo ndo utambua kuwa kuna rangi zaidi ya 7
 
Kiutaratibu yawezekana ukawa na hoja lakini kiubinadamu haiwezekani.
Hawa wavuvi wamefika kwenye eneo ilipo ndege, labda wanasikia watu wanalia ndani, hawaoni mtu yeyote wa kuwaelekeza wafanye nini, halafu eti wasubiri tu! Wasubiri mtu hewa. Ndugu yangu ubinadamu hautaki hivyo.
Kama wangeona vyombo vya uokoaji vinasogea haraka na kupewa ishara kuwa subirini, wangesubiri.
Manusura mmoja anasema hata baada ya mlango kufunguliwa na wao kutoka nje hawakuona chombo chochote cha kupanda, baadae ndipo mitumbwi ya wavuvi wa kawaida ilifika, hata wakawa wanahofia kupanda.
Fikiria muda wote huo, hao waliotakiwa kutoa maelekezo sahihi walikuwa wapi? (na unaambiwa ndege ilizunguka hewani kwa nusu saa - wakati wote huo wanajiandaa - mpaka rubani anaambiwa tua majini tutakuja kuwaokoa - anatua hawapo!)
Ndugu yangu, nyumba inaungua, watu wamo ndani wanapiga kelele wewe badala uvunje ukuta unashauri wasubiriwe zimamoto!! (na hujui watafika lini). Vunja ukuta hata kama itasababisha nyumba ianguke na hao waliomo wauawe na vifusi. Fanya kitu kuliko kutofanya chcochote.
 
TrueVoter, chutama! Nyeti zote umezianika nje hadi watoto wanakucheka. Lazima sasa, kama Watanzania, tukiri kitu kimoja...hatuna uongozi!

Tunao walafi wanaokula kwa urefi wa kamba zao kama walivyoshauriwa na kiongozi wao mkuu hivyo ni wajibu wao na jukumu lao, kumtukuza!

Watanzania, hivi sasa tumefikia kiwango cha kutisha cha ujinga na nashangaa hajajitokeza mnafiki moja kuipa pongezi serikali ya CCM chini ya SSH!

Lucas mwashambwa, unatakiwa huku JF uanzishe thread ya kumtukuza kiongozi wa serikali kwa kuhakikisha Watanzania tunaishi kwa usalama zaidi!
 
Ni ukweli ulio wa wazi kabisa kuwa kazi inayofanya serikali yetu chini ya uongozi shupavu wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ni kubwa Sana na ya kutukuka, Ni serikali iliyotujengea moyo wa uzalendo ,upendo , kujitoa na kujitolea miongoni mwetu watanzania, Ni serikali ambayo imejenga umoja wa kitaifa na mshikamano wa kitaifa ,Ndio sababu unaona hata kwa tukio la Jana namna watanzania walivyojitolea kuokoa maisha ya watanzania wenzetu waliopatwa na ajari, lakini pia umeona namna mh Rais wetu alivyoguswa na suala Hilo na kuagiza kijana mtanzania mmoja apatiwe ajira haraka Sana, Jambo hili limepokelewa kwa shangwe na hisia Kali Sana za kumpongeza Rais wetu kwa uamuzi wake huo wa upendo na uzalendo wa kujali juhudi na uwezo wa mtu mmoja mmoja, lakini pia hatua za kiuchunguzi zinaendelea kuchukulia ili kubaini sababu ya msingi ya kutokea ajari Ile ili hatua ziweze kuchukuliwa ikibaibika Kuna mtu hakutekeleza wajibu wake ipasavyo, Tumwamini Rais wetu mpendwa mama Samia na Tumuunge mkono
 
Asante mkuu kwa sifa zisizo na kifani kwa mama yetu Samia Suluhu.
Lakini ninyi ndio mnapewa majukumu ya kufanya na mnawaachia wavuvi kufanya uokoaji huku mnaimba ngonjera za sifa.

 
Asante mkuu kwa sifa zisizo na kifani kwa mama yetu Samia Suluhu.
Lakini ninyi ndio mnapewa majukumu ya kufanya na mnawaachia wavuvi kufanya uokoaji huku mnaimba ngonjera za sifa.
Mimi Ni mkulima natekeleza wajibu wangu wa kulima ili wa mjini mpate chakula
 
Swali kwako Lucas mwashambwa, je vikosi rasmi vya uokoaji vilifika kwenye tukio baada ya muda gani?
 
Katika ripoti ya uchunguzi hayo yote yatabainishwa na yeyote aliyezembea atawajibishwa kwa uzembe wake, Najuwa walichelewa lakini huu si muda wa kutupiana lawama
Ripoti ya uchunguzi! isije ikawa kama ile ya benki kuu iliyotakiwa itoke mapema mwaja jana lakini hadi leo hata ule ujasiri wa kukiri uwepo wake umeshindikana.
 
Ripoti ya uchunguzi! isije ikawa kama ile ya benki kuu iliyotakiwa itoke mapema mwaja jana lakini hadi leo hata ule ujasiri wa kukiri uwepo wake umeshindikana.
Hapana mkuu haiwezi kuwa Kama hivyo, Tuiamini serikali yetu ya mama Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…