Nimehesabu, Polisi walimpiga Hamza risasi 19 baada ya kuwa ameanguka chini na sio tishio tena kwa usalama

Nimehesabu, Polisi walimpiga Hamza risasi 19 baada ya kuwa ameanguka chini na sio tishio tena kwa usalama

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nimeangalia video juu ya tukio la huyu mtu anaetuhumiwa kuua askari, na kuangalia kilichotokea.

Baada ya kuwa amemaliza risazi katika SMG ya pili aliyokuwa nayo na kunyoosha mikono juu, polisi walimpiga risasi ambayo ilimfanya aanguke chini. Hakukuwa na haja tena kuendelea kumpiga risasi mtu ambaye amejeruhiwa kaanguka chini.

Alipokuwa amejeruhiwa na kuanguka chini, Polisi waliendelea kumpiga risasi akiwa amelala chini ambazo nimehesabu na kukuta walimpiga risasi 19. Ajabu ni kwamba kundi lote lile la Polisi walifanikiwa kumpiga pale tu alipoishiwa risasi na kuonyesha wazi alishaamua kufa - maana alijifanya target rahisi sana.

Sasa hili lina maana gani? Ni wazi kwamba polisi wetu hawana weledi katika matukio kama haya, kwa kuwa baada ya kuwa umeona ameishiwa risasi na si tishio tena, jambo la msingi inabidi kuwa ni kumkamata akiwa hai ili kuweza kupata habari zaidi atakapodhibitiwa.

Kwa hiyo Polisi walipaswa kumkaribia kwa umakini katika formation ambayo kunakuwa na askari wanamsogelea wakiwa na silaha tayari, na wengine waanawa-cover askari wanaomsogelea katika kitu tunaita "flanks".

Lakini pia, kuna upande wa pili, kwamba huenda kuna askari walikusudia kumuua ili huyu mtu asitoe taarifa juu ya ugomvi wake na askari, maana mfu haongei!

Kwahiyo kuna conclusion tatu tu hapa, kwamba polisi wetu wako very unprofessional, incompetent, na pia walikusudia huyu mtu asitoke kwenye hili tukio akiwa hai.


 
Duh

240336786_225284519596487_1634442739025882664_n.jpg
 
Ni uoga tu
Au kijimwambafy. Unajua kuna polisi hawajawahi kuwa katika mpambano wa risasi kwa hiyo wanakuwa na mchemko fulani wa excitement katika tukio kama hili na watapiga risasi ovyo hata isipostahili.

Lakini oia kama nilivyosema, huenda baadhi yao walijua kabisa lazima mtu huyu afe la sivyo atatuumbua!
 
Back
Top Bottom