Nimehesabu, Polisi walimpiga Hamza risasi 19 baada ya kuwa ameanguka chini na sio tishio tena kwa usalama

Nimehesabu, Polisi walimpiga Hamza risasi 19 baada ya kuwa ameanguka chini na sio tishio tena kwa usalama

Ceremonial shooting...random shooting.. Shooting spree..
Mwaka 0202 kuna mama mmoja alisikika akisema "askali wao wakilenga moja huwa hawakosi" sasa jana sijui kilitokea nini..
Au haku maanisha askali hawa?
 
Nimeangalia video juu ya tukio la huyu mtu anaetuhumiwa kuua askari, na kuangalia kilichotokea.

Baada ya kuwa amemaliza risazi katika SMG ya pili aliyokuwa nayo na kunyoosha mikono juu, polisi walimpiga risasi ambayo ilimfanya aanguke chini.
Haja nyoosha mikono juu alikuwa anajipiga kifua
 
Haya matukio muachane nayo,hayasaidii chochote.kama kufa ashakufa,

Kuhusu weledi wa polisi kukabiliana na mtu kama huyu hili nalo tuwaachie polisi wenyewe.

Hebu fikiria polisi anafanya kazi zaidi ya miaka kumi ila hajawahi kupambana na jambazi ana kwa ana,licha ya kuwa na mafunzo

Tukumbuke:hakuna mafunzo Wala mazoezi kwenye kupigana/au kushambuliana,bali Kuna nafasi moja tu,ya kumpiga adui/mpinzani wako.

Wengi wanahoji kwanini asingekamatwa akiwa hai? Mimi nakataa....

Lazima askari wetu walikuwa makini kuhusu vilipuzi n.k.

Lakini pia,hebu fikiria...yaani wewe unayesoma hii comment unaona Askari wenzio wamepigwa risasi,wamelala

Bado tu una wazo la kumkamata akiwa hai?
Watanzania tuache unafiki,wengi hatuwezi.
 
Police wa Tanzania hawajui kwamba habari ni muhimu zaidi.. ni kweli baada ya kuishiwa risasi alikuwa si threat tena....kulikuwa hamna haja tena ya kumtwanga ya kichwa.

Adui akishanyoosha mikono juu na kuweka silaha chini, huyo muda huo huo anageuka na kuwa shahidi mkubwa mno tena wa thamani kubwa!!

Kwa mfano sasa hivi wangeshajua why ali-target askari tu na si raia.
 
Nimeangalia video juu ya tukio la huyu mtu anaetuhumiwa kuua askari, na kuangalia kilichotokea.

Baada ya kuwa amemaliza risazi katika SMG ya pili aliyokuwa nayo na kunyoosha mikono juu, polisi walimpiga risasi ambayo ilimfanya aanguke chini. Hakukuwa na haja tena kuendelea kumpiga risasi mtu ambaye amejeruhiwa kaanguka chini.
Duh! It is a pity.
 
Hili suala wala halihitaji uchunguzi wa polisi kama alivyoagiza Mh. Rais. Linahitaji TUME HURU japo simaanishi kwamba matendo ya marehemu ni ya kusifiwa. Linataka kufanana sura na lile la kina Zombe, tofauti ni kuwa huyu alipambana. Angekuwa gaidi, jambazi kama ambavyo tayari umma umemhukumu angeua wengi sana pale.
 
Yule anatakiwa kuchunguzwa inaonekana alitumwa kuhakikisha kwamba Hamza amekufa. Maana amefika tu na kuanza kupiga maiti Risasi.
 
Tushukuru Mungu huyu jamaa alikuwa sio gaidi alikuwa na shida na polisi ccm tu,angekuwa gaidi raia zaidi ya mia wangekufa,maana alitamba zaidi ya nusu saa akiwa amezungukwa na daladala kibao zenye abiria
 
Angalia wanavyotembea kwa kujimwambafy kishujaa utafikiri wametoka kwenye mapambano makali mstari wa mbele vitani, kumbe imechukua zaidi ya saa kukabiliana na mtu mmoja ambaye wamemuua baada ya yeye kuishiwa risasi na kujiweka peupe apigwe risasi. Pathetic incompetents.

1629970412312.png
 
Brother hamna excitement kama kupiga risasi mzee ndio Mana walifyatua nyingi kila siku wanatembea na machine. Hizo bila kutumia hivyo ni ile excitement yao tu lakini pia huwezi jua kutaka kupoteza maelezo kutoka kwa jamaa
 
Nimeangalia video juu ya tukio la huyu mtu anaetuhumiwa kuua askari, na kuangalia kilichotokea.

Baada ya kuwa amemaliza risazi katika SMG ya pili aliyokuwa nayo na kunyoosha mikono juu, polisi walimpiga risasi ambayo ilimfanya aanguke chini. Hakukuwa na haja tena kuendelea kumpiga risasi mtu ambaye amejeruhiwa kaanguka chini.

Alipokuwa amejeruhiwa na kuanguka chini, Polisi waliendelea kumpiga risasi akiwa amelala chini ambazo nimehesabu na kukuta walimpiga risasi 19. Ajabu ni kwamba kundi lote lile la Polisi walifanikiwa kumpiga pale tu alipoishiwa risasi na kuonyesha wazi alishaamua kufa - maana alijifanya target rahisi sana.

Sasa hili lina maana gani? Ni wazi kwamba polisi wetu hawana weledi katika matukio kama haya, kwa kuwa baada ya kuwa umeona ameishiwa risasi na si tishio tena, jambo la msingi inabidi kuwa ni kumkamata akiwa hai ili kuweza kupata habari zaidi atakapodhibitiwa.

Kwa hiyo Polisi walipaswa kumkaribia kwa umakini katika formation ambayo kunakuwa na askari wanamsogelea wakiwa na silaha tayari, na wengine waanawa-cover askari wanaomsogelea katika kitu tunaita "flanks".

Lakini pia, kuna upande wa pili, kwamba huenda kuna askari walikusudia kumuua ili huyu mtu asitoe taarifa juu ya ugomvi wake na askari, maana mfu haongei!

Kwahiyo kuna conclusion mbili tu hapa, kwamba polisi wetu wako very unprofessional, na pia walikusudia huyu mtu asitoke kwenye hili tukio akiwa hai.


View attachment 1909036
Askari angejuaje kama jamaa kaishiwa risasi
 
Back
Top Bottom