Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Uchawi haunaga mlango mmoja aisee! Lengo la uchawi ama nguvu za giza ni kuvuruga kabisa mfumo wa dunia, kuwachanganya wanadamu, na kuwaangamiza. Sasa mbinu zinatofautiana. Watoto wanaweza kurithishwa uchawi, au kurushiwa uchawi na jamaa zao. Wanaweza pia kutolewa kafara.
Umeuona uchawi au Umeamini hivyo?

Mfumo wa dunia unavurugwa na uchawi mbona mfumo wa dunia ya ulaya na Asia kwa sehemu kubwa upo vizuri?

Mbona mifumo mibaya ipo zaidi Africa tu? Au uchawi sio Universal case?
 
Story za kusadikika hizo. Hata mimi naweza kuandika kisa hapa kuhalalisha uwepo wa uchawi ila haimaanishi kuwa hiyo story ni ya kweli. Story zote za uchawi ni hearsay, mtu anasimuliwa nae anaenda kusimulia by the time story inamrudia muasisi ishabadilika na kuongezewa chumvi zaidi.

Aidha sio kila kitu ambacho hakina rational explanation ni uchawi.

Uchawi ni story zinazoaminiwa na wavivu wa kufikiri na kuenezwa na wajinga.
 
Ukitulia utaelewa aisee. Hakuna tamaduni ama mfumo wa dunia usiotikiswa na nguvu ya giza. Mtu yeyote anaweza kutumika agent wa uchawi awe ni Mzungu ama Mwarabu au Afrika. Uchawi hauchagui, ni universal. Usidhani penye elimu na maendeleo na utajiri hakuna uchawi. Usikute sehemu kama hizo ndizo zenye uchawi uliokubuhu.
 
Uchawi kama uchawi hauonekana kwa macho, ila utendaji wake unaonekana jinsi watu wanavyoathirika na kuteseka na kufa pia.
Sasa hapo hujaona utendaji ni UMEAMINI TU

Sikiliza Mkuu, Imani yoyote inaweza kubadilisha dunia yako au maisha yako.

Unavyoamini ndivyo inavyokuwa katika akili na ufahamu wako.

Nakushauri kuanzia kesho katafute kitabu cha Lister Sumrall kinaitwa ''FAITH CAN CHANGE YOUR WORLD''

Kuna chapters zitakusaidia sana.
 
Story za kusadikika hizo. Hata mimi naweza kuandika kisa hapa kuhalalisha uwepo wa uchawi ila haimaanishi kuwa hiyo story ni ya kweli. Story zote za uchawi ni hearsay, mtu anasimuliwa nae anaenda kusimulia by the time story inamrudia muasisi ishabadilika na kuongezewa chumvi zaidi.

Aidha sio kila kitu ambacho hakina rational explanation ni uchawi.

Uchawi ni story zinazoaminiwa na wavivu wa kufikiri na kuenezwa na wajinga.
Ni hatari sana kukana kwamba nguvu za giza na uchawi haupo; hapo unakuwa katika uwezekano mkubwa wa kuathiriwa ama hata kudhuriwa na nguvu za ushirikina bila wewe kujua.
 
Ukitulia utaelewa aisee. Hakuna tamaduni ama mfumo wa dunia usiotikiswa na nguvu ya giza. Mtu yeyote anaweza kutumika agent wa uchawi awe ni Mzungu ama Mwarabu au Afrika. Uchawi hauchagui, ni universal. Usidhani penye elimu na maendeleo na utajiri hakuna uchawi. Usikute sehemu kama hizo ndizo zenye uchawi uliokubuhu.
''Ukisema usikute sehemu hizo ndizo zina....''

Hiyo kauli inadhihirisha kabisa kuwa huna uhakika kama sehemu hizo zina uchawi, ni unahisi tu hivyo kwahiyo si Universal Case

Ama la, Unaweza kunipa scenario moja ya uchawi uliotokea Ulaya au America?
 
Ni hatari sana kukana kwamba nguvu za giza na uchawi haupo; hapo unakuwa katika uwezekano mkubwa wa kuathiriwa ama hata kudhuriwa na nguvu za ushirikina bila wewe kujua.

Hivyo vitisho mnatoa sana ila tukiwaambia mturoge mnashindwa. Tuokoe nguvu na muda niroge au tafuta mchawi aniroge badala ya kunipa vitisho hewa.
 
Wewe unashindwa kutambua kuwa issue ya ukoloni kuna waafrica pia walikuwa wana wakamata waafrica wenzao na kuwa uza kwa wakoloni ..haulijui kabisa hilo ....then uchawi sio makalio kusema kila mtu anao au anaujua -- issue ya uchawi ni deep secret
Habari ya kuwakamata waafrika wenzao na kuwauza kwa wazungu (puppertism) ni contrary issue wala haihusiani na mada hii

Hakuna mahali nimesema uchawi upo kwa kila mtu hata Hawa wanaoamini kama upo hawajasema hivyo pia

Ila, hata kama upo kwa wachache kwanini walishindwa kuutumia kuua au kudhuru wakoloni mpaka watunyonye kwa karne nzima?

Jibu kinagaubaga tuendelee.
 
Hivyo vitisho mnatoa sana ila tukiwaambia mturoge mnashindwa.. Tuokoe nguvu na muda niroge au tafuta mchawi aniroge badala ya kunipa vitisho hewa.
Huko unaenda mbali sana. Wewe unajua kwa nini & umefikaje hapa duniani? Why kati ya mbegu zote countless za kiume moja tu iliyotunga mimba yako ndiyo imefanikiwa wewe ukapatikana? Sasa usiseme tu chochote maana hakuna mwanadamu anayeshi tu purely kwa uwezo wake mwenyewe.
 
Huko unaenda mbali sana. Wewe unajua kwa nini umefikaje hapa duniani? Why kati ya mbegu zote countless za kiume moja tu iliyotunga mimba yako ndiyo imefanikiwa wewe ukapatikana? Sasa usiseme tu chochote maana hakuna mwanadamu anayeshi tu purely kwa uwezo wake mwenyewe.

Unabadilisha magoli. Nimekwambia niroge au tafuta mchawi yeyote aniroge kama huwezi sema huwezi sitaki hizo ngonjera zako.
 
Back
Top Bottom