Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Hizo ni imani tu na wenge lenu usiku

Hakuna kitu kama hicho (uchawi)
uyo mtoto aliyekuwa kipofu, kiziwi nk apelekwe hospitali utapewa chanzo na nini kifanyike
Sio imani tu mkuu, uchawi upo hata ulaya, uchawi upo mpaka kwenye vitabu vya dini umezungumzwa sana kuwa ulikuwepo, sasa ukisema haupo ni kama vile unajitoa ufahamu tu. Mimi niliwahi kuishi sehemu moja Kigoma, ili ufike kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani unapandisha ngazi kama kumi hivi, sasa ilikuwa ikifika mida ya kuanzia saa 4 usiku utasikia mtu anapandisha ngazi mpk anafika pale mlangoni, na anabisha hodi ukifingua hakuna mtu,tulikwenda mpaka tukazoea tukawa hatufungui.
Kuna usiku mmoja nakumbuka tulikuwa sitting room tunaongea usiku tukasikia vyombo vimedondoka jikoni kwenye sink la kuoshea vyombo, wote tuka pay attention kwenda kuangalia, cha ajabu tukakuta hakuna hata chombo kimoja kilichoguswa, kwahiyo ndugu hii kitu ipo sana.
 
Sio imani tu mkuu, chawi upo hata ulaya,uchawi upo mpaka kwenye vitabu vya dini umezungumzwa kuwa ulikuwepo, sasa ukisema haupo ni kama vile unajitoa ufahamu tu.
Wanaopinga, huwa wanakataa kwa maneno tu ya nje, lakini pengine hawajui wanachosema au wanaamua tu kufumba macho.
 
Mimi nilikuwa mtu nisiyeamini uchawi Tena ukiniambia nakuona tu muongo ulieshindwa na maisha Nakumbuka Kuna level ya maisha nilianza kuikalibia aisee nitiwa uchizi huo mpaka nikapenda! Hospital kwenda unapewa mavidonge tu ambayo hata wanao kupa hawana uhakika nayo.

Kufupisha tu story nilipelekwa kwa mtaalamu mwezi tu mmoja nikapona Tena hiyo midawa ya hospital nimetumia almost 3 year hakuna nafuu.

Aisee uchawi upo
 
Mimi nilikuwa mtu nisiyeamini uchawi Tena ukiniambia nakuona tu muongo ulieshindwa na maisha Nakumbuka Kuna level ya maisha nilianza kuikalibia aisee nitiwa uchizi huo mpaka nikapenda!! hospital kwenda unapewa mavidonge tu ambayo hata wanao kupa hawana uhakika nayo

Kufupisha tu story nilipelekwa kwa mtaalamu mwezi tu mmoja nikapona Tena hiyo midawa ya hospital nimetumia almost 3 year hakuna nafuu
Aisee uchawi upo..
Ni kweli inatokea. Ila watu wasikariri eti hospital wakikosa ugonjwa tu lazima ni uchawi, hapana. Kuna magonjwa mengine yanaweza yasijulikane, yasitambulike. Lakini huo "utaalamu" wa giza nao upo tangu enzi na enzi.
 
Uchawi hakuna hizo imani tu
Mkuu samahani, hivi uchawi nini. kuinga kitu usichokijua maana nao ni ujinga, maana leo hata Dunia ya walioelimika, wanajua uchawi upo, ispokua hawaupi kipaumbele, karika kufanikisha au kufelisha mambo yao.

Kitu ambacho hata huku, usipoupa kipaumbele kafanikisha ua kufelisha mambo yako, maisha yatasonga na wala hutosumbuka.
Ila uchawi upo, Kwa waumini wa Dini, haya mambo yameandikwa kwenye Vitabu vyao.
 
Sasa kama unajua wanawarithisha why unasema uchawi haupo? Acha kutania watu hapa mkuu.
Atakuwa anaamini kwamba upo ila hajawahi kukutana nao. But usiombe ukutane na hiyo balaa, afadhali usimliwe na jirani
 
Kama zilivyo nyanja nyingine zenye madaraja na viwango, na uchawi ndivyo, hawa wote wanaobisha ni wachawi katika madaraja yao, lengo lao nini wanapokataa? lengo lao ni kuuzuia kweli isijulikane. Ili nini? waendelee kuoperate kuwaminya na kuwakandamiza watu kwa uchawi bila vipingamizi, vipingamizi ni vipi? Vipingamizi kwao ni Kweli, ukiijua Kweli uko huru.
 
Hakuna uchawi.

Kama upo, nitoleeni mfano mimi.

Nirogeni.

Karibu miaka 10 sasa nishatoa challenge ya wachawi kuniroga lakini bado nipo tu.

Hahahaaa.

Hakuna uchawi.
Rudi kwa wamatumbi huku uoneshwe kazi.

Wanasemaga uchawi hauvuki bahari hio ndio falsafa pekee inayokulinda wewe. Vinginevyo ungekuwa ushatengenezwa chap.
 
Unatakiwa uwe na ujasiri wa Kimungu, hapo unashinda au angalau unakuwa katika mikono salama.

NB: Watu watambue kwamba hii kitu hainaga fomula moja. Ina nyanja kibao tu kama ilivyo idadi ya mashetani nadhani. Kwa hiyo usikariri kwamba mbona hivi, mbona vile. Hii nayo ni elimu ya giza kama zilivyo elimu zingine, na zina mtandao mpana.
Ujasiri wa kimungu haufungamani na mambo ya anasa. Unaweza ukaomba nguvu za kimungu ukazipewa ila the moment ume£øπb@na∆ au kufululiza pombe basi unarudi kwenye mikono ya watesi wako chap na nguvu zinakuwa zimefifia.

Hapo ndipo ugumu ulipo.
 
Mimi nilikuwa mtu nisiyeamini uchawi Tena ukiniambia nakuona tu muongo ulieshindwa na maisha Nakumbuka Kuna level ya maisha nilianza kuikalibia aisee nitiwa uchizi huo mpaka nikapenda!! hospital kwenda unapewa mavidonge tu ambayo hata wanao kupa hawana uhakika nayo

Kufupisha tu story nilipelekwa kwa mtaalamu mwezi tu mmoja nikapona Tena hiyo midawa ya hospital nimetumia almost 3 year hakuna nafuu
Aisee uchawi upo..
Mtaalamu gani huyo walikupeleka kwake? Mie nina ndugu anasumbuliwa na jini masauti. Anaongea mwenyewe tu.
 
Back
Top Bottom