Nimeibiwa gari na majambazi nyumbani, msaada tafadhali

Mkuu mchoma dirisha hausiki....ninacho kiona tangu machinga kufurushwa na bobaboda na bajaji....haya matukio ndio yame gain momentum.
Acha uongo.
Matukio ya wizi yapo siku zote.
 
Kwahiyo mateller wanawapigia wao simu au straight kwa majambazi?
majambazi wanapewa michongo na watu wa ndani, either bank au mtu wako wa karibu alafu majambazi yanaomba ushauri kwa wazee ili likitokea la kutokea waweze kucover track na kupata backup ila wakifanikisha wanawatoa mchuz kidogo...Ndio mana me sikuiz nikitaka kununua kitu cha hela mingi, nachukua hela kwa timing sana, watu wanaweza wakawa wanakuwinda ila we hujui...
 
Kasema simu zote zimeibiwa ba hiyo picha katolea kwa tablet ya mtoto wake
bado hainishawishi kumuamini, siku hizi kuna mfumo wa ku-save images, documents, password nk. moja kwa moja kwenye server za google, apple na makampuni mengine.

kwa google mfumo huu huitwa google cloud, kwa apple mfumo huu unaitwa icloud.

leo hii ukiibiwa simu halafu ukataka ku-restore baadhi ya data zako muhimu, ni rahisi sana. unaweza ku restore hata kwa computer ya ofisini kwako au ya jirani yako,almradi tu iwe connected na internet.

nilitegemea huyo jamaa baada ya kuibiwa gari pamoja na simu(kama anavyodai), angefanya hivyo ili atulee picha yenye ubora inayoonyesha number plate ya gari lake
 
Walinifunga kamba wakaniuliza ufunguo ulipo, s imu, kad I za banki namba za siri bunduki ikiwa kichwani
Dah, pole sana ndugu..Muhimu zaidi wamekuachia uhai. Mali hutafutwa lakini uhai hautafutwi. MUNGU MWENYEZI akufanikishe na kupata mali zako walizoiba (au nzuri zaidi ya hizo walizochukua)
 
Duuuh...humu dunian inabidi ujiamin we mwenyewe tu!
 
Amesema ameibiwa simu na hiyo picha imetoka kwenye tablet ya mtoto wake inawezekana mtoto alipiga picha hiyo for fun tu wala hakujua kama kuna siku inaeza kutumika kama reference

,
Kama umewahi kukutwa na tukio lolote la ujambazi huwezi kusema hili ni la uongo
 
Big up umetisha sana mkuu.
 
Wewe ni mubishi kaweka huku Hadi RB yake ya police mkuu, na alipoanzisha Uzi yuko kwenye panic mode so kukumbuka hayo yote ya google sijui nini ni ngumu, pia wameondoka na simu zote, so usibeze majanga ya wengine shukuru Mungu ka hayajakukuta, na sioni sababu ya mtu kudaganya jambo sensitive Ili apate nini sasa!?
 
Tunawashauri Kila siku fungeni GPS laki tu ,Unajipa matumaini itazima njiani huyo mwizi si anajaza mafuta.
Kampuni gani inafungwa hizo gps.unalipa Laki moja kwa mda gani?tuelimishe tafadhali
 
Na unathubutu kueleza ujinga kama huu hapa? (kama siyo chai). Unakuta wezi wanaiba kwa mtu unayemfahamu, tena wanasombea walivyoiba kwenye mkokoteni, wewe unaona solution ni kwenda kumjulisha mwenyewe kwanza. Huna tofauti na yule jamaa aliyejitetea alijiriwa kulinda mlango wa mbele tu ndiyo maana wezi walipokuja kuvunja mlango wa nyuma hakufanya chochote.
 
Kikubwa uhai,gari na pesa vinatafutwa. Mshukuru Mungu hawajakudhuru wewe au familia yako.
Umenena vyema.
Kikubwa duniani UZIMA kikifuatiwa na makazi ya uhakika.
Kama huna sehemu ya kuishi au baba mwenye nyumba amesema lazima wiki hiyo uhame, na huna uwezo wa kulipa nyumba angalau miezi mitatu. Bro, hata miss tz awe hapo nusu uchi. Huangalii Wala huyu abduli Cha umbea hatasimama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…