Hivi ushawahi kuibiwa wewe hata penseli???
Huwezi kuhisi mleta mada amechanganyikiwa hata kuileta tu taarifa hapa anastahili pongezi, pengine angekua amezimia,
Unayajua majambazi wewe hasa yakivamia ndani kwako,
Msipende ujuaji kwenye kila kitu, vingine mkiona vimekuzidi kimo mnakausha tu.
Kuna wapuuzi hapa hawajawai kukutwa na matukio.
Kuna kipindi niko na bibi mmoja ana hela na nyodo sana.
Ikafika siku mi nirudi kwake kutoka job.
Nampigia yupo bar sa nane usiku anacheza pool zamani hizo.
Hapo sa nane usiku.
Nafika pale bar e bana tuondoke aaah akawa mkali huyo kanipa key nenda nyumbani ntakukuta duh.
Mi nikajiondokea.
Sasa ile nafika home kwake nikakuta majambazi wamengoa dirisha zima wameweka pembeni wanahamisha kila kitu.
Jamaa walikua na mkokoteni bajaj hamna enzi hizo.
Wanasomba wanapeleka wanarudi wanasomba tv cm,hela chochote kinachobebeka .
E bana nilivyowakurupua mbinu sisemi wakatoka baruti na mkokoteni wao walikua wa4.
Nikaacha vile vile nikamrudia huyu mwanamke bar.
Namkuta bado anacheza pool.
Najaribu kumwambia huko home majanga twende ukaone.
Ndo kwaanza ananambia "we wivu tu unakusumbua"
Mama umeibiwa kila kitu pale kwako hapafai
Ndio anashtuka "unasema"
Namjibu"nimefika nimekuta wezi wamengoa dirisha lote wanatoa vitu pale.
E bana akatupa fimbo ya pool ingia kwenye gari twende.
Tukafika kweli kakuta kile nilichomwambia ndio kilivyo.
Ayayaya dem kaanza kilio,nikaanza kazi kubembeleza.
Yule mwanamke uchungu ule wa kuibiwa wakati ye ni mtoto wa mjini ilimuuma sana.
Nilikodi rum hotel wiki atulie kidogo maana alikua anaweweseka tu then kilio.
Ikabidi ahamie kwangu tu maisha yaendelee