Nimeibiwa gari na majambazi nyumbani, msaada tafadhali

Nimeshawahi kuibiwa gari najua machungu yake. Nilifuatilia sana nilitumia pesa mpk ningeweza kununua hata gari nyingine ndogo na nilichemsha. Mpaka leo sijaipata ila nilifanikiwa sanq kuuelewa mfumo wa wezi wa magari na ushirika wao na wazee
Wazee ni akina nani?
 
Ni gari aina ya pajero io nyeupe T893 DWT maeneo ya bahari beach wameiba vitu vingi atakayeona msaada tafadhali gari haina mafuta ya kutosha kwa hiyo itakuwa imezima njiani popote namba ya mawasiliano 0655385246

View attachment 1999715View attachment 2000213
Pole ndugu, tutashirikiana kwa hili wakipita anga zetu, na wanaosema watu kama hawa tuwapeleke polisi hawajuwi uchungu wa alieumizwa…
 
Pole sana ndo maana mm nikipak lazma nizime swichi ya waya ya pump ya mafuta ili hata ukiwasha utawasha adi ufe haliwaki
Kama ni gari ndogo ndogo tunaweka begani tunaondoka nayo [emoji1].

Anyway, tukirudi kwenye mada kwanza nampa pole madau aliyeibiwa. Inauma sana jasho lako la miaka kadhaa kupotea ndani ya dakika kadhaa.
Chakufanya: Omba msaada kwa jiirani wa karibu ambae amefunga cctv camera kwenye njia zinazoeelekea kwako. Hii itakupa picha kuwa ilielekea upande gani. Kisha anza kufuatikia upande huo ukiwaulizia walinzi wa magetini wa usiku. Kama ulikuwa na simu ndani ya gari au kama waliiba simu, ni starting point nzuri sana kujua ilipo au wahusika.
Kama walikuja na funguo zao, itakuwa walichongesha copy ya funguo zako na hao watakuwa ni watu wa gereji au carwash iliyo maeneo ya karibu na kwako(wanaofahamu unapoishi).
Kama una mlizi au kuna kijana alikuwa mfanyakazi wako na ukamfukuza au akaacha kazi kamata huyo abanwe vizuri.
Kama hujuwepo nyumbani wakati tukio linatokea, chunguza uliokuwa nao au anayefahamu ulikuwa wapi, inawezekana aliuza ramani.
 
Funguo niliwapa mwenyewe walitaka kunipiga risasi baada ya kukosa hela waliiba vitu vingine vingi wakatumia gari kama gateaway
Ilikuwa mida gani?

Siri ya kuwakamata majambazi au Mali zako ni wewe Kwa kusaidiwa na Polisi au hata mwenyewe kuweza kuichora ramani mzima ya tukio.

1. Walitumia usafiri gani kufika kwako(most likely pikipiki). Na waliingiaje ndani.

2. Walikuwa wangapi.

3. Walikubananisha vipi. Eleza tukio zima. Eleza angalau bastola ilikuwa ya rangi gani na ukubwa au shape ya silaha. Kama unajua model sema.

4. Pia ukiwaeleza Polisi, andika kiasi kikubwa cha fedha ulizoibiwa. Hii itasambaratisha kundi hasa kwenye mgao. Itasaidia snitching kama utaahidi zawadi.

5. Ulifanya transaction yeyote kubwa hivi karibuni? Ilimhusisha nani na nani?

Kuna makundi ya ujambazi yanayojulikana na Polisi. Haya makundi hufuatiliwa up to two years. Hutumia mbinu na silaha zilezile. Silaha nyingine ni za serikali. Ni vizuri kuelezea methodology yao, sauti zao, silaha, uharaka wao, ukatili wao etc...

Polisi watajua ni kundi gani na linatokea wapi.
 
Ili mwizi aondoke nalo inabidi aliwashe betri ikiwapo. Immobilizer is the way to go. Halafu nadhani hata ukiondoa betri, linaweza kua tracked Mpaka eneo betri ilipoondolewa (correct me if I am wrong)
Immobilizer za after market? Ni very expensive na very complex
Raha ya immobilizer iwe ni stock configured.
Lakini pia si kweli kuwa Gps inategemea battery ya gari , battery ya gari ipo pale kufanya top up tu , Gps zina built in battery ambayo huwa inatoa signal kwa wastani hata wiki mbili baada ya battery ya gari kutolewa

Tatizo kubwa la kufunga Gps module hapa kwetu ni location za kuficha hicho kifaa , hii ilitakiwa iwe siri kuu , ila watu wameshindwa kuweka miiko ya kazi , kila mtu ikiwemo wezi , wanajua ni location ipi kwa gari ipi ,Gps module inawekwa.
 
Mm sio mtaalam wa magari,naona umbie hii swichi ipo wapi?
Au umefanya modifications gari yako?

Naomba utusaidie na sie wengine tujue
Ni simple sana hiyo wiring, hata wewe mwenyewe unafanya !
Switch inayotakiwa ni ile ya waya mbili tu , kwenye gari yoyote unaweza kupata extra switch location, unachofanya unakata waya moja kati ya zile mnili zinazokwenda kwenye fuel pump ndo huo unaupitisha kwenye switch,
Kitakacho tokea ninkuwa pump haitawaka hadi hiyo switch iruhusu umeme .
 
Acha majigambo ndugu yangu ,mpaji Ni Mungu.Mimi nimepoteza FunCargo yangu inaniuma balaa.
Ahaaa pole ni uzembe huo unananua fun cargi let say milioni sita kufunga gos laki moja na nusu unashindwa?gps ni guarantee kupata gari yako kuliko hiyo comprehensive insurance
 
Ni sawa mkuu lakini haifai kudharau kile ambacho mtu anamiliki maana huo ndo uwezo wake.Uzembo kila mtu hufanya maana huwezi jua ya baadaye.
 
Ilikuwa mida gani?

Siri ya kuwakamata majambazi au Mali zako ni wewe Kwa kusaidiwa na Polisi au hata mwenyewe kuweza kuichora ramani mzima ya tukio.

1. Walitumia usafiri gani kufika kwako(most likely pikipiki). Na waliingiaje ndani.

2. Walikuwa wangapi.

3. Walikubananisha vipi. Eleza tukio zima. Eleza angalau bastola ilikuwa ya rangi gani na ukubwa au shape ya silaha. Kama unajua model sema.

4. Pia ukiwaeleza Polisi, andika kiasi kikubwa cha fedha ulizoibiwa. Hii itasambaratisha kundi hasa kwenye mgao. Itasaidia snitching kama utaahidi zawadi.

5. Ulifanya transaction yeyote kubwa hivi karibuni? Ilimhusisha nani na nani?

Kuna makundi ya ujambazi yanayojulikana na Polisi. Haya makundi hufuatiliwa up to two years. Hutumia mbinu na silaha zilezile. Silaha nyingine ni za serikali. Ni vizuri kuelezea methodology yao, sauti zao, silaha, uharaka wao, ukatili wao etc...

Polisi watajua ni kundi gani na linatokea wapi.
Mkuu kuna mambo mengine umetaja hapo haya apply kibongo bongo.
 
Mimi nachukia wezi sana sio siri, awe kibaka, mdokozi, jambazi n.k ilhali anafanya kazi ya unyang'anyi au kudhulumu hawa watu wa tabia hii nawachukia mpaka kufa..
 
Ili mwizi aondoke nalo inabidi aliwashe betri ikiwapo. Immobilizer is the way to go. Halafu nadhani hata ukiondoa betri, linaweza kua tracked Mpaka eneo betri ilipoondolewa (correct me if I am wrong)

Sawa ataliwasha battery ikiwapo... Vipi akifika sehemu akatoa battery na akaamua kulivuta?

Kwa mazingira ya Jamaa hata kama gari ingekuwa na Immobilizer ni kazi bure... Sababu walichukua funguo...

Immobilizer ni antitheft hivyo mtu hawezi iba ikiwa hana ufunguo wa gari unless awe na ufunguo...
 
Mimi niliibiwa simu nikaweuka sembuse gari, sijui sasa hivi utakuwa na hali gani? Polee.

Nenda kijiwe kilichopo karibu na wewe ongea private na watu wanao kaa pale watakupa connection.

Majuzi niliibiwa vifaa vya ofisi connection nilipewa na watu ambao sikuamini, nilivikamata viko police, hapo ni baada ya mwezi.

Polee sana
 
Ilikuwa mida gani?

Siri ya kuwakamata majambazi au Mali zako ni wewe Kwa kusaidiwa na Polisi au hata mwenyewe kuweza kuichora ramani mzima ya tukio.

1. Walitumia usafiri gani kufika kwako(most likely pikipiki). Na waliingiaje ndani.

2. Walikuwa wangapi.

3. Walikubananisha vipi. Eleza tukio zima. Eleza angalau bastola ilikuwa ya rangi gani na ukubwa au shape ya silaha. Kama unajua model sema.

4. Pia ukiwaeleza Polisi, andika kiasi kikubwa cha fedha ulizoibiwa. Hii itasambaratisha kundi hasa kwenye mgao. Itasaidia snitching kama utaahidi zawadi.

5. Ulifanya transaction yeyote kubwa hivi karibuni? Ilimhusisha nani na nani?

Kuna makundi ya ujambazi yanayojulikana na Polisi. Haya makundi hufuatiliwa up to two years. Hutumia mbinu na silaha zilezile. Silaha nyingine ni za serikali. Ni vizuri kuelezea methodology yao, sauti zao, silaha, uharaka wao, ukatili wao etc...

Polisi watajua ni kundi gani na linatokea wapi.
Tumia akili.
Amesema amewapa funguo mwenyewe wakaondoka nayo.
 
Mimi niliibiwa simu nikaweuka sembuse gari, sijui sasa hivi utakuwa na hali gani? Polee.

Nenda kijiwe kilichopo karibu na wewe ongea private na watu wanao kaa pale watakupa connection.

Majuzi niliibiwa vifaa vya ofisi connection nilipewa na watu ambao sikuamini, nilivikamata viko police, hapo ni baada ya mwezi.

Polee sana
Yeye hajaibiwa. Ameporwa huku anaona.
 
Back
Top Bottom