Nimeibiwa gari na majambazi nyumbani, msaada tafadhali


Amekuambia ameporwa vitu vingi ikiwemo simu zake....

Hili ni gumu kulielewa?

Kuna post ameonesha kabisa na RB Aliyopewa polisi....
 

Kama wewe Mungu amekubariki una uelewa na hayo mambo ya online storage isiwe ticket ya kuwadhihaki wengine....

Kuna msururu wa watu wengi hawana uelewa na hayo mambo....
 
Kama wewe Mungu amekubariki una uelewa na hayo mambo ya online storage isiwe ticket ya kuwadhihaki wengine....

Kuna msururu wa watu wengi hawana uelewa na hayo mambo....
Hawa vijana wanadhani kwa vile wao wanajua vitu sijui icloud na makorokoro mengine kwa hivyo kila mtu anao uelewa huo.

Sisi wengine tulizaliwa enzi za simu za kuzungusha kwa hivyo hayo mengine wala hatuyaelewi.
 
Nimecheka sana baada ya kuona hako kakaratasi ka RB.

Yaani miaka karibu 61 sasa ya Uhuru RB yaandikwa kwa mkono?

Hata hivyo nikupe pole sana mkuu kwa kuibiwa gari yako.

Lakini hii ndo hali halisi ambayo ndo yaendelea hapa nchini kwa sasa khasa jijini Dar.

Anza na makao makuu ya soko la vifaa vilivyoibwa vya magari Gerezani ila nakuhakikishia wizi huo waitwa "steal to order" yaani mteja tayari yupo standby.

Ila sikushauri kupoteza muda kwa hilo.

Wananchi twapaswa kuchukua tahadhari zaidi ili kuokoa maisha na familia zetu.

Pia tuwekeze zaidi kwenye ulinzi wa nyumba zetu kwa vifaa kama "alarm systems" za kutuamsha au ving'ora ambayo vitaamsha hata majirani.
 
hiki kijikaratasi hata mimi hapa nilipo naweza nikakiandika na kukituma jf. bado huja ni convince. acha chai kijana
Hebu kiandike chako ukiweke hapa kama ni rahisi hivyo.
Ungekuwa umewahi kuona na kesi yoyote ya kugushi nyaraka inavyokuwa ngumu wala usingerahisisha hivo
 
Hakuna kitu kinaumiza pia kama kupoteza ama kutibiwa simu.
Wewe acha ilikuwa bado mpyaaa nimeiwekea cover nzuri dah yule mwizi alikuwa na dawa, alinisalimia vizuri afu alikuwa smart ana simu kubwa mbili mkono, naongea na mtu simu ilipita sikioni niliumia sana, nikaenda police😂😂😂😂 na risiti na box la simu kilichoendelea ni historia sitokaa niwe na simu inayozidi laki nne ni matumizi mabovu ya pesa.
 
Nunua nyingine tu. Ikiwezekana hata mbili. Halafu ajiri Mmasai analala kwenye gsri 24 hours
 
Umeongea kitu kizuri kwasababu upo uwezekano wa mtu kuchongesha funguo endapo kama aliwahi kumpa mtu funguo ya gari
 
Halafu wakikamatwa na kuuawa Kuna watetezi wa haki za binadamu wanaanza kuleta ujinga
Kuuawa sio adhabu, kifungo kinacho ambatana na mateso ndio dawa yao
 
Umeongea kitu kizuri kwasababu upo uwezekano wa mtu kuchongesha funguo endapo kama aliwahi kumpa mtu funguo ya gari
Umeandika kinyesi (as long as thread hii inahusika).

Mtu ameshikiwa bastola, akafungwa kamba. Akapokonywa funguo Kwa nguvu. Watu wakasepa.

Halafu eti wewe unaleta story za kuchongesha funguo!! Pathetic
 
Kwani watu waliokua wanaokotwa kwenye viroba ulikua utawala wa nani?

Waliokua wanatekwa Mo,Roma nk ulikua utawala wa nani?
Lissu alipigwa risasi pale dodoma ulikua utawala wa nani?
Fact
 
Umeandika kinyesi (as long as thread hii inahusika).

Mtu ameshikiwa bastola, akafungwa kamba. Akapokonywa funguo Kwa nguvu. Watu wakasepa.

Halafu eti wewe unaleta story za kuchongesha funguo!! Pathetic
Umeni-attack badly as if mi ndo mwizi mwenyewe nimekutwa na hilo gari

Umesoma post ambayo nimeinukuu ina maelezo yeyote kuhusiana na kushikiwa bastola?

Main post yenyewe haina hayo maelezo ambayo we umeyaandika ya kushikiwa bastola, labda kama ulikua unazungumzia uporaji mwingine ambao umeelezwa kwenye comments za wadau na mimi sijausoma
 
Kwahiyo unakubali kwamba umedandia treni kwa mbele!!
 
Nimemshangaa sana mdau namna alivyoshupalia hilo suala la picha. Inashangaza mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…